Kama ni kweli basi amekwisha! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kama ni kweli basi amekwisha!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by ifolako, Dec 11, 2010.

 1. i

  ifolako Member

  #1
  Dec 11, 2010
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 98
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  SMS ya kumuua Zitto yanaswa

  [​IMG]
  Na Luqman Maloto
  Ujumbe mfupi wa maneno (SMS) unaohusishwa na mpango wa kijasusi wa kumuua Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Zitto Zuberi Kabwe (pichani), umenaswa na Uwazi.

  Katika SMS hiyo, aliyeiandika alisisitiza kwamba Zitto atakufa kwa siri lakini kabla ya kutekeleza kifo chake, atanyang’anywa nyaraka zote alizonazo ambazo hazikufafanuliwa kwenye ujumbe.

  SMS hiyo, iliyonaswa kwenye simu ya mmoja wa makada wa CHADEMA (jina tunalo), ametajwa kama mmoja wa watakaotekeleza mpango wa kumuua Zitto, inasomeka:

  “Nawaarifu kwamba nipo Mara nimemaliza kukutana na viongozi wa Mwanza. Inaelekea hawakubaliani na hoja yetu ya kumfukuza Zitto, sasa nilikwisha kusema kwamba tuweke mkakati kwenye Media JF. Ni …, … na … (yanatajwa majina ya watu).”

  SMS hiyo inaendelea: “Ni …, … na … (majina mengine ya makada wa CHADEMA) watatekeleza kazi tuliyowapa na … (anatajwa kiongozi wa CHADEMA) atawapa mtu wa kuwaongezea nguvu.”

  Ujumbe huo hauishii hapo, unaendelea: “Kuweni makini, hakikisheni amewapa nyaraka zote alizonazo kabla ya kumuua, usiri unahitajika… atawasaidia kujua nyendo zake na hii tu ndiyo njia ya kukinusuru chama.”
  [​IMG]
  Uchunguzi unaonesha kuwa SMS hiyo ilizunguka kwa watu kadhaa ambao wanadaiwa wapo kwenye mtandao ulioandaliwa kutekeleza mpango wa kukatisha maisha ya Zitto.

  Gazeti hili limebaini kuwa mmoja wa wabunge wazoefu wa Viti Maalum (CHADEMA) alitumiwa kisha naye akaituma (kui-forward) kwa mwenzake ambaye ni memba mpya ndani ya bunge.

  Gazeti hili lilifuatilia mnyororo wa SMS hiyo na kugundua kwamba wakati ujumbe ukizungushwa kwa wanaodaiwa wana mtandao, uliingia ‘kirusi’ kwa kumfikia mtu ambaye hakukubaliani na wazo la kumuua Zitto.

  “Hapa hatari iliyopo ni kwamba kuna mtu ambaye hakubaliani na wazo la kumuua Zitto, ndiyo atakuwa amevujisha,” kilisema moja ya vyanzo vyetu.

  Chanzo chetu kilisema kuwa mtu huyo baada ya kupata SMS hiyo, aliituma kwa mama yake Zitto, Shida Salum ambaye naye ‘aliifowadi’ kwa mwanaye.

  Gazeti hili lilimpata Zitto na alikiri kupata SMS, ingawa alidai kuwa uchunguzi ndiyo utafanikisha kumnasa mhusika mkuu wa ujumbe huo.
  Zitto, akijibu bila uchangamfu, alisema wakati mwingine anahisi kuna watu wanatumiwa ili kukivuruga CHADEMA.

  “Nafsi yangu haisemi kama ni kweli. Inawezekana kuna watu wametuingilia, Mungu ndiye anajua,” alisema Zitto.
  Alipoulizwa kuhusu kuripoti polisi, Zitto alijibu:

  “Nikiripoti ni kwa ajili ya uchunguzi wa kipolisi tu. Sitaki kutoa kwenye vyombo vya habari, sihitaji mgogoro kwenye chama.”
  Kwa upande wa Mama Zitto, alikiri kupata SMS hiyo na kueleza kwamba tayari amesharipoti kwenye vyombo vinavyohusika.
  “Sitaki kuizungumzia hiyo SMS, inachunguzwa kipolisi,” alisema Mama Zitto.
  [​IMG]
  Gazeti hili lilizungumza na Mbunge wa Viti Maalum CHADEMA, Regia Mtema ambaye ni mmoja watu wanaodaiwa kutumiwa SMS hiyo ambaye alikiri.

  Hata hivyo, Regia aliye pia Ofisa wa Oganaizesheni wa chama hicho alisema: “Hiyo SMS sijatumiwa mimi peke yangu, kila mtu makao makuu anayo.

  “Nafikiri kuna watu wametengeneza lakini hakuna mpango wa kumuua na kwanini auawe?”
  Baada ya kuzungumza hayo, simu ilikatika na alipopigiwa tena hakupokea mpaka tuliapoamua gazeti kwenda mitamboni.

  Wakati Zitto akipuuza ufuatiliaji wa SMS hiyo, chanzo chetu kimoja ndani ya makao makuu ya CHADEMA, kilisema kuwa si vema kudharau vitu kwa sababu ujumbe huo una alama za hatari.

  “Mimi sipendi sana kuzungumzia mambo ya marehemu Chacha Wangwe (aliyekuwa Makamu Mwenyekiti CHADEMA), lakini naye kifo chake kilitokea akiwa na mvutano na viongozi wengine wa chama kama ilivyo kwa Zitto sasa,” kilisema chanzo chetu.

  Mpango wa kumuua Zitto, inakuja baada ya matukio kadhaa ambayo yalikaribia kuondoa uhai wake, ikiwemo kuwekewa sumu kwenye maziwa.

  Miaka minne iliyopita, Zitto alikunywa maziwa yenye sumu kwenye hoteli moja jijini Mwanza na kuokolewa na aliyekuwa mbunge wa Viti Maalum (CCM), marehemu Amina Chifupa ambaye alimpigia simu na kumueleza asiendelee kunywa.

  Hata hivyo, kutokana na wingi wa maziwa aliyokuwa amekunywa dakika chache baada ya kupokea simu ya Amina, aliishiwa nguvu na kukimbizwa kwenye hospitali moja jijini humo ambapo alipatiwa matibabu.
   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  Dec 11, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Magazeti ya kidaku yatabakia hivyo hivyo ya kidaku kwani ndivyo yalivyoandikishwa kuwa ya kudaku! Kwanza gazeti linafikiri kwamba watu hawajui kwa nini habari hizi zisiwemo katika magazeti mengine serious ambayo yanayofahamika? Nasikia wazushi wamejaribu kupeleka kwenye magazeti hayo serious wamawafukuza!

  Hivi hamkuaibika kuhusu Wangwe ambapo uwongo wenu ulikuja kulidhihirika?
   
 3. Job K

  Job K JF-Expert Member

  #3
  Dec 11, 2010
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 6,146
  Likes Received: 1,957
  Trophy Points: 280
  Uchafu mtupu!! Hamchoki? Kwanzo chanzo chenyewe eti Uwazi! Nalo ni gazeti hilo? Si wakaandike mambo yao ya kingono ngono!! Kwanza Magazeti ya Kada wa CCM yatakuwa na habari gani nzuri zaidi ya kuvuruga vyama vingine? Kazi kweli kweli kama bado unasoma magazeti ya Shigongo!
   
 4. leseiyo

  leseiyo Senior Member

  #4
  Dec 11, 2010
  Joined: Oct 25, 2007
  Messages: 116
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Huyu Mwandishi namfahamu,ni kilaza kupindukia hana elimu yoyote ya uandishi na kwa sasa ndiyo anasaka kacheti ka uandishi pale Dar School of Journalism (DSJ).Wakati wa kampeni alipewa gari la kutanulia na Amos Makalla akawa kila siku anamuandika kwenye magazeti ya udaku.Nadhani ana gawio lake la mafisadi.
   
 5. j

  julius Senior Member

  #5
  Dec 11, 2010
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 114
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Jamani suala zima la maendeleo ni pana mno na nchi zote zilizoendelea duniani zilibeba garama hzo za maendeleo hayo,,kwanini nasema hayo sisi watanzania ni watu ajbu sana ambao sijapata kuona dunia hii,,,nadhani ndio maan sisi ni maskini yaani mimi nawaewe msomaji...ehhhh ndyo ilivyoo...... sijui nimalezi mabaya sielewi, lakini nadhani ni mfumo mzima wa maisha yetu yaani siasa zetu za malezi, so back to the mjadala,,,tabia yetu mbaya sana nikutopenda jambo lolote linaloleta maendeleo ya jumla kwa watu wote,,chadema ni cha kinachokua ni chama kilicho leta mabadiliko ya fikra nchini, mabadiliko ya kutaka kulazimisha kupenda vilivyo vyetu na kushabikia vilivyo vyetu,,,,,ndyo hvyo na mataifayote dunuani ndivyo yalivyo...sasa hichi chama kinavyokua kinapata majaribu mbalimbali moja wapo nimipango mibaya ya wasiopenda maendeleo ya watanzania kutaka kukibomoa,,,sasas sijui wnatanka kuipeleka wapi nchi yetu,democrasia ya kweli lazima ijengwe na watanzania wote na kwa garama zote,,,,nchi hii aiweziwe endelea kamwe bila ya kua na chama kinacholeta changamoto kwa watawala wa nchi hii, ndyo kaka, ndyo dadad,,,,,,,habari usika ni ya kwenye gazeti la udaku gazeti la mmoja wa makada wa ccm,,,sasas sijui wewe msoaji unafikiriaje hapo...lazima mikakati ya kukialibu ama kukibomoa hipo .....................:teeth:
   
 6. The Planner

  The Planner JF-Expert Member

  #6
  Dec 11, 2010
  Joined: Dec 1, 2010
  Messages: 344
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  .........Habari kama hii tutaiona kwenye magazeti yanayomilikiwa na wakada wa CCM tu!
   
 7. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #7
  Dec 11, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,235
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Tulishajadili hii kitu zamani, na ilionekana ni ya kizushi, na Zitto mwenyewe alitoka hadharani na kuikanusha!
  Usiturudishe nyuma!
  Zitto sasa hivi tumeambiwa ni mgonjwa yuko hospitali, cha kufanya ni kumwombea!
  Aksante.
   
 8. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #8
  Dec 11, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,616
  Likes Received: 21,245
  Trophy Points: 280
  kuna kitu very fishy hapa......
  chadema i dont believe them
  ccm i dont believe them....

  yangu macho
   
 9. jessetz

  jessetz Member

  #9
  Dec 11, 2010
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mtaripoti mpaka mtu akienda chooni sasa, kama mtacover kila kitu yanayotokea kwa hawa wanasiasa, udaku waachie wadaku wenyewe
   
 10. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #10
  Dec 11, 2010
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,082
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 0
  Haya nyinyi wanazi wa Chadema, hichi ndio chama cha kiharamia mnacho-kishabikia. Siku zote nawaambia, what do you expect from a night club don and an ex padre who makes out with someones wife? UMAFIA tu.
   
 11. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #11
  Dec 11, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 1,991
  Likes Received: 889
  Trophy Points: 280
  ..Ifolako..next time ukisha-attach habari kama hii nawe weka maoni yako sio una-attach then unaingia mitini. so what do you say? title yako inasema'kama ni kweli basi amekwisha', sasa husemi nani amekwisha? na pia husemi kama ni uongo, nani atakwisha? yoyote anayeleta habari toka magazeti ya udaku (Kiu, Uwazi, Sani, Risasi, Ijumaa nk), pls Mods toeni! Hivi hamjakubali hadi sasa kwamba watanzania wameshawatambua mnachofanya dhidi ya CDM? wateja wenu wanataka habari kama 'X na Y wala denda live', 'kigogo wa ....afumaniwa na denti', nk, mkianza kuleta habari za siasa, tena siasa chafu, mbaya zaidi dhidi ya Chama kipenzi cha watanzania, mtapoteza wateja.
   
 12. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #12
  Dec 11, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,914
  Likes Received: 101
  Trophy Points: 160
  Ninavyojua mimi ktk mpango wa mauaji kama huo, sio rahisi kutaja majina ya watu(ktk sms) kama mwandishi alivyotueleza hapo.
  Vinginevyo hao walioandaa huo mpango ni wehu.
   
 13. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #13
  Dec 11, 2010
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,817
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  UMENENA, nakuunga kwa hii hoja yako.
   
 14. Zipuwawa

  Zipuwawa JF-Expert Member

  #14
  Dec 11, 2010
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 3,047
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Hivi vyombo vya habari wakati mwingine vya weza kutuchanganya.......
   
 15. m

  matawi JF-Expert Member

  #15
  Dec 11, 2010
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 2,058
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Yaani upupu mpaka jumamosi imeharibika. Sasa uwazi unapokaribishwa kwa ma great thinker tutafika kweli?? uwwwwi
   
 16. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #16
  Dec 11, 2010
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,674
  Likes Received: 732
  Trophy Points: 280
  Huu ndiyo wakati wa kuipunguza nguvu CHADEMA nani asiyejua kuwa Dr. Slaa alipata asilimia 44 ya kura zote? Bila propoganda kama hizi 2015 CCM itapotea kama KANU.
   
 17. Babkey

  Babkey JF-Expert Member

  #17
  Dec 11, 2010
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 3,954
  Likes Received: 1,659
  Trophy Points: 280
  Habari yenyewe inaonyesha ni ya kihuni. Hakuna mipango ya kumua mtu maarufu kama Z inayofanyika kwenye simu kwa uwazi namna hiyo. Nadhani mwandishi angejaribu kuanza kutunga hadithi za watoto na baada ya miaka 30, labda atakua ameweza kutunga nzuri zaidi.
  Nadhani pia ni muhimu vyombo vya dola kufanya kazi yake
   
Loading...