Kama ni kufungia waamuzi miaka 3,basi mechi zote zipitiwe na wapate hukumu sawa

kibaravumba

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
6,635
7,005
Mechi zote zina makosa mengi ya namna hiyo.Kuna wengine wamenyimwa kufunga kwa kupigiwa kipenga cha offside wakati ukweli hawakuwa wamezidi.

Na inakuwaje kuwa mwamuzi anaona mpira umetoka nje(umevuka mstari) ila ukiwa ndani ya goli,halafu inakuwa kona?
Yaani hii ni maajabu ya kipekee utaweza kuyaona Tanzania.

Jiulizeni kwa nini wazungu walileta teknolojia ya VAR?
Ni kwa vile matukio yanafanyika haraka na kutokana na ubinadamu tu mtu anaweza asigundue mara moja,hadi apitie video.Sasa nashangaa kama adhabu itakuwa ni kufungiwa miaka mitatu sioni mwamuzi anayebaki salama,labda kama mmeamua kupendelea na kuongozwa na mihemko.

Mechi ya Simba na Yanga mwamuzi aliyetoa penalty badala ya adhabu ndogo na red card naye hastahili kuachwa.Huyu amekuwa akifanya makosa sana ya namna hiyo hasa katika mechi za Yanga na Simba.

Nawashauri tumieni teknolojia ya VAR mkianza na viwanja vikubwa kwanza.Msilete visingizio eti ni gharama kubwa wakati mnaingiza mabilioni kwa mwaka.Huu mkakati wa kufukuza waamuzi mtawamaliza kwani wanafanya kazi wana njaa na pressure kubwa nje ya uwanja.

Iwapo tu mwandishi wa habari anaogopa kusema ukweli kwa sababu ya kuogopa wahuni wa timu fulani tu hapa nchini,inakuwaje kwa waamuzi ambao hata hoteli wanazofikia ni huko huko wanakoishi wahuni?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom