Kama ni hivi basi Katiba ichomwe moto

dustless

JF-Expert Member
Oct 21, 2016
796
709
Katiba ni kitu ama utaratibu uliowekwa ili kuwaunganisha watu pamoja. Kwa mantiki hivyo basi wanapaswa waishi, waijali, waitunze na waiendeleze.

Ziko katiba nyingi duniani ila asili ya katiba zote ni watu wawili tu, Adamu na Hawa. Hawa watu walikuwa na katiba waliyopewa na muumba, cha ajabu pamoja na katiba yao kuandikwa kupitia kitabu kitakatifu wao ndo walikuwa watu wa kwanza kuivunja kufuatia external force iliyotumika ili kutimiza haja ya kiumbe kingine kabisa na si muumba wao.

Kuanzia hapo katiba zikawa zinatengezwa na wanadam na wanadam hao hao wanazikataa na kuzivunja tena. Hufikiri suluhu ni kupanga na kupangua. Ila ukwel utabaki pale pale kuwa hakuna katiba yoyote duniani itakayo kidhi kiu ya binadam wote kwa wakati husika.

Worse part of constitution ni kuegemea upande mmoja na kukandamiza upande wa pili. Na huwa zinatengenezwa na tabaka fulani lenye nguvu huku upande wa pili ukibaki kuburuzwa ama kulazimishwa kushangilia ndoto za watu fulani fulani zikitimia.

Ikitokea kiongozi akafuata katiba na ikawa kama msahafu wake, kimsingi atakuwa amekonga nyoyo za tabaka nufaika na kizazi chake chote huku akicha simanzi kwa tabaka jingine lisiloguswa na utaratibu huo.

Na ikitokea mwingine akaweka pembeni katiba au anaichungulia kidogo na kutoka, wapo naamini watakao kunwa mioyo yao kwa kuwa yanayotekelezwa pengine walihitaji kabisa yawemo kwenye katiba ila kwa bahati mbaya ama kwa maksudi hayakuwekwa. Hivyo kiongozi wa aina hiyo anakuwa anatekeleza unwritten constitution ambayo nayo kimsingi ina wadau wengi tu.

Hivyo basi, kwa kuwa hakuna na hapatatokea katiba itakayounganisha wadau wote kwa wakati husika, basi kusiwepo kabisa kirusi hiki kandamizi ili watu waishi maisha huru.

Tichukulie mfano mdogo wa ndoa, hakuna maandishi yoyote yanayowaunganisha wawili hawa lakini wanatambua kitu kibaya na kizuri katika mahusiano yao. Na mmoja akikengeuka kuna hatua wanazochukuliana na mambo yanasonga wakati kutengana inabaki kuwa option ya mwisho kabisa kwao.

Kama ni hivyo basi tuchomeni katiba ili tuishi maisha huru na tupunguze na kama sio kuondoa kabisa minong'ono ya chini chini, nawaza tu lakini....
Karibun sana watu wa aina zote.
 
1480237053603.jpg
 
Katiba ichomwe moto, maana Magufuli anaongoza nchi Kwa hisia zake binafsi na hafuati katiba aliyoapa kuilinda.
Alisema wazi kuwa anainyoosha nchi wakati kwenye katiba hakuna kipengele cha kunyoosha nchi, kila kitu kinaendeshwa kisheria.
Hahahaha
 
umewaza vyema mkuu, ila uliwaza na upande wa madhara ukishaichoma??.
Nimawazo kama yako tu.
 
umewaza vyema mkuu, ila uliwaza na upande wa madhara ukishaichoma??.
Nimawazo kama yako tu.
Siku zote ukiwa uwanjani mbinu huja zenyewe, kama tumeyakabili haya hatushindwi hayo mengine..
 
Siku zote ukiwa uwanjani mbinu huja zenyewe, kama tumeyakabili Haya hatushindwi hayo mengine..
Ni kweli ila, ninamashaka na jibu lako kwani kama limekaa kimtago vile??.
Ukinielewa watakua wameelewa wengi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom