Kama ni gari ya chini kwa Mzee Mwinyi, kwanini isiwe IST au Fun Cargo za bei rahisi?

Mzee Mkapa ana nyumba lakini ameongezewa nyingine na serikali ili awe nazo nyingi kwa mujibu wa Biblia.

Mzee Mwinyi ana gari lakini anaongezewa lingine ili awe nayo mengi kama Biblia ilivyosema.

Mzee Kikwete ana nyumba lakini ameongezewa nyingine na serikali ili neno la Mungu litimie.

Na kisha kila mmoja atatoa hesabu mbele ya Mungu siku itakapofika.

Basi Yesu akasema, Kila aliyenacho ataongezewa na awe navyo vingi na yule asiyenacho atanyang'anywa hata kile kidogo "anachodhani" anacho - Kitabu cha Mathayo (25:29)

Mungu wabariki Watanzania!
 
Acheni tafsiri potofu! Marko 4:25 ni hitimisho la Sura nzima ya 4 ambapo Bwana Yesu alikuwa amemaliza kuwafundisha wanafunzi wake kwa mifano kadhaa! Mstari huo unalenga moja kwa moja tafsiri ya kiroho naona "washenzi" mnataka kuutumia kuhalalisha uporaji wa rasilimali za taifa!
 
... acheni tafsiri potofu! Marko 4:25 ni hitimisho la Sura nzima ya 4 ambapo Bwana Yesu alikuwa amemaliza kuwafundisha wanafunzi wake kwa mifano kadhaa! Mstari huo unalenga moja kwa moja tafsiri ya kiroho naona "washenzi" mnataka kuutumia kuhalalisha uporaji wa rasilimali za taifa!
Ndio maana hata wewe umeongezewa MATUSI ili uwe nayo mengi!
 
Sheria nzuri kama hizo za kuwalinda na kuwatunza viongozi wetu ni nzuri sana. Tanzania Inaweza kuwa mahali pazuri pa kuishi kama tutarekebisha zile chache mbovu
 
Kiukweli wengi wetu leo, hatukuwa tunajitambua wakati wa utawala wa Mwinyi.

Mzee Mwinyi anaonekana ni mtu asiyejali kuhusu wananchi wengine, as long as yeye kapata.

Huyu Mzee haheshimu wala haoni umuhimu wowote kuhusu sheria wala katiba ilimradi ziko upande wake.

Kina Warioba ingawa hawajazeeka sana lakini at least wanaweza kusimamia wanachosema.

1- Wakati wa utawala wa Magu alishawishi zaidi ya mara mbili kuhusu katiba ivunjwe ili Magu aendelee na madaraka.

Binafsi nilidhani ni kwasababu ya uzee, ila baada kuandika kwenye kitabu chake kujutia kuliachis uhuru bunge kuhusu kundi la G55 nimegundua ni hulka yake

2- Mzee Mwinyi rafiki yake ni yule mwenye nacho, mwenye uwezo wa kumpa anachotaka.
Hapa naweza kusema hana tofauti na Sheikh wa Mkoa wa Dar. Mwinyi alimkana kabisa January Makamba baada ya January na familia yake kukosana na Jiwe.

Kwa mantiki hii, sioni ni kwa namna gani tungesalimika kama Mwinyi angekuwa na maamuzi enzi hizo. Maana anaonekana siyo mzee mwenye kuridhika kabisa.
 
Ni kweli haka kazee uwezo wake wa kupambanua mambo ni mdogo sana.

Wakati wa mwendazake kalikuwa na mtazamo wa kuvunja katiba eti mwendazake afie madarakani.

Kwahiyo hata kwenye utawala wake kama kangekuwa na kofia mbili kasingetoka madarakani. Lkn Nyerere alikanyuma uenyekiti kakawa powerless.
 
Ni kweli haka kazee uwezo wake wa kupambanua mambo ni mdogo sana.

Wakati wa mwendazake kalikuwa na mtazamo wa kuvunja katiba eti mwendazake afie madarakani.

Kwahiyo hata kwenye utawala wake kama kangekuwa na kofia mbili kasingetoka madarakani. Lkn Nyerere alikanyuma uenyekiti kakawa powerless.
Mwinyi ni mzee ambaye huwezi kusikia anatetea kundi la watu wasio na faida kwake kabisa.

Siku zote anapambania familia yake tu. Mwanaye kasimikwa urais huko Zanzibar baada ya kuua watu wengi sana.
 
Ni kweli haka kazee uwezo wake wa kupambanua mambo ni mdogo sana.

Wakati wa mwendazake kalikuwa na mtazamo wa kuvunja katiba eti mwendazake afie madarakani.

Kwahiyo hata kwenye utawala wake kama kangekuwa na kofia mbili kasingetoka madarakani. Lkn Nyerere alikanyuma uenyekiti kakawa powerless.
Bwashee umezaliwa mwaka gani?

Nyerere alimnyima Mwinyi uenyekiti?!!!
 
Ni hulka yake hakana msimamo. Ndiyo maana Nyerere alijutia ikawa too late. Akawa anamponda kuwa mwenye kufanya maamuzi ni mkewe mama Sitti.

Mwalimu alisema kakilala na mkewe usiku kanapewa maamuzi ya kufanya na kanaamka nayo asubuhi. Siwezi kuisahau ile hotuba ya mwalimu nilitizama pale mnazi mmoja mubashara kupitia screen kubwa iliyokuwa ikiwekwa pale na the late Mengi.

Kama sikosei ilikuwa projector ile na bado hakukuwepo na kituo rasmi cha TV.
 
Back
Top Bottom