Kama ndo hivi,AJARI hazitapungua hapa Tanzania

Alexism

JF-Expert Member
Aug 14, 2011
3,423
2,045
Leo niko Ubungo Terminal hapa najiendaa kwenda kwa akina Ta Muganyizi kula senene ila kwakua ni wajibu wangu kuna mambo ambayo nimejaribu kuangalia hapa Ubungo Terminal.
Kwanza nimefatilia kama kweli magari huwa yanafanyiwa service ilo angalau wanajaribu.
Pili nikaangalia usafi wa stendi hii na kweli ni chafu kama dumpo la takataka,vyoo vichafu,mifereji michavu na maji taka yamezagaa mpaka sehemu kunakopatikana vyakula na vinywaji.
Pia nimetembelea sehemu kama baa au grocery huku ndo nikakuta mijamaa takribani sita wakiwa wanazibua moja baridi moja moto.
Nimenasa mazungumzo haya,mmoja kasema naendesha hiyo (bus) kesho Musoma mjini saa kama ngapi ndani ya nyumba.Wakaendelea kila mtu akiwa anatamba hiyo kesho na wote wako chakali.Basi kama kawaida nikamuuliza jirani yangu kwamba hao wote ni madereva jamaa akasema ndio ninawajua,nikauliza sasa kesho wanasafari alafu wamelewa jamaa kasema,acha wapige maji kwani nchi hii na serikali si unaona inavyokwenda,basi sikuwa na swali tena wakuu.
Nikarudi zangu kule gereji kuangalia usafiri ambao nitasafiri na kama unafanyiwa service,nikakuta kazi inaendelea vizuri ila nusura nilewe kwani alufu ya bangi ni kama kuna tanuru.
JE HAPA KWELI TUTAPUNGUZA AJARI ZINAZO TOKEA NA KUUA WATANZANIA AU KUWAACHA NA VILEMA.?
Ukiingia kwenye sehemu ya kulala wasafiri basi utadhani ni zizi kabisa(nimekosa neno la kutumia hapo) Nikajiuliza hivi jiji au halmashauri inazifanyia nini kodi za watu wanaolipa kila siku au ni wizi halali wa wakuu wa nchi hii.NAWASILISHA.
 
Twambie kama na wewe umevuta maana kiherehere chako kwani wewe ni nani hapa Tanzania?
 
Kanyaga twende, mbaya zaidi hata abiria kwani tunafikiria hayo, ndio kwanza tunafurahia madereva wa namna hiyo, ajali ikitoke ndio kelele mingi utadhani tulikuwa hatuyaoni.
 
Back
Top Bottom