Kama Nchi za ulaya zinadorora kiuchumi na kufilisika sisi huu ufisadi tutafika? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kama Nchi za ulaya zinadorora kiuchumi na kufilisika sisi huu ufisadi tutafika?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by harakat, Nov 11, 2011.

 1. harakat

  harakat JF-Expert Member

  #1
  Nov 11, 2011
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 2,908
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Italia ,Ugiriki na Nchi nyingine za ulaya ambazo huwa tunaziita Nchi wahisani
  zina hali mbaya sana kiuchumi sasa sijui kama sisi ambao tunawategemea
  wao kwa misaada kama tutatoboa na ishu zetu za kifisadi au itakua kimeo tu?

  Wasiwasi wangu ni kwamba kama waziri mkuu wa Italia amekubali kujiuzulu
  kwa nini viongozi wetu wasfanye hivyo kama wameshindwa hata kutokomeza
  ufisadi unaoonekana wazi je wataweza uchumi huu unaodorora?

  Nchi imekopa fedha nyingi kutoka kwenye Benk za kibiashara kama ilivyo
  kwa Ugiriki na Italia ambazo zenyewe zina limitation sijui sisi mwisho
  wa ukopaji ni kuuza Nchi au ni trilion ngapi na hizo trilion ni za madafu au Dola?

  NAWASILISHA........................
   
 2. s

  sanjo JF-Expert Member

  #2
  Nov 11, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Maadili hayo katika Tanzania hayapo.
  (1) Giza limesambaratisha uchumi nani kajiuzulu?
  (2) Meli ya Spice Islander imezama na kuua watu wengi nani kajiuzulu?
  (3) Wizi mbalimbali wa EPA, Meremeta, Tangold, BOT Twin towers, Mwanachi Gold etc nani kajiuzulu
  (4) Viongozi wa serikali kupeana nyumba za serikali nani kajiuzulu?
  (5) TCRA kutumia zaidi ya TZS2.3 bn kusomea watu 3 na ujenzi wa Mawasiliano Towers kutumia zaidi bilioni 45. Badala ya watu kuwajibika utasikia visingizi vingi mara malengo binafsi, fitna nk. Hutaona mtu anawajibika.

  Mapinduzi ya kifikra na kikatiba yanatakiwa ili kubadilisha mwelekeo huu.
   
 3. Daniel Anderson

  Daniel Anderson JF-Expert Member

  #3
  Nov 11, 2011
  Joined: Aug 7, 2011
  Messages: 879
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nchi hii inaendeshwa kienyeji tu. Hakuna cha debt ceiling wala nini. Kabla hatujaenda kwa politicians, ni vema tuwaangalie na wataalamu wetu.
  Hawa jamaa wamekua ni waoga kwa taaluma zao mpaka wanakera. Ni karibuni tu hapa nilienda CHC kuchukua data fulani kuhusiana na privatization tz, lakini jamaa muda wote wa mazungumzo yetu alikuwa akizungumza kama mwanasiasa na si mtaalamu.
  Hawa wanashindwa kuwaeleza wanasiasa ukweli, wanabaki kushabikia siasa. Nchi inasiku chache kabla haijatangaza mufilisi.
   
 4. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #4
  Nov 11, 2011
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,445
  Likes Received: 7,182
  Trophy Points: 280
  Fukara hafilisiki.sema kama watoa misaada wanafilisika.tanzania itakufa
   
 5. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #5
  Nov 11, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Watanzania tumeshakuwa sugu kwa matatizo. Hivi kuna shida yoyote itakayotokea ikawa ngeni kwa watanzania? Mbona naona tumeshapitia kila aina ya shida iliyopo hapa ulimwenguni!
   
 6. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #6
  Nov 11, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,529
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Kila siku makontena kibao yanaingiza bidhaa toka China na mashariki ya mbali; hizo hisia za kufilisika unazitoa wapi? Kila mtanzania anajitunza mwenyewe hakuna anayelipiwa matibabu zaidi ya watumishi wa serikali; kila mtanzania anatunza wazee wake hakuna anayesaidiwa na serikali; Kila mtanzania anajipangia utaratibu wake wa kupata makazi ya kudumu serikali haijawahi kuwajengea nyumba wakazi wake;

  Kwa maana hii serikali ikikosa pesa unazungumzia maisha ya kikundi kidogo sana cha Watanzania kisichozidi watu 1,000,000 wenye ajira serikalini na taasisi zake.

  Kule ulaya ni tofauti - kuna wazee wanatunzwa na serikali; wasio na kazi wanategemea kulipwa posho ya kuishi na serikali; makazi yanaandaliwa na serikali n.k.
   
Loading...