Wakudadavuwa
JF-Expert Member
- Feb 17, 2016
- 17,506
- 15,999
Takriban miaka mitatu iliyopita tulibahatika kuwa na kambi ya upinzani iliyosheheni watu wenye ueledi na uzalendo mkubwa. Laana ya kula 'matapishi' yao imewafanya watumwa na sasa wamegeuka kuwa adui namba moja wa nchi yetu Tanzania. Dhambi ya kufunika midomo na gundi imewafanya kuwa kama mazuzu na sasa wameamua kumtumikia kafiri.
Ukiangalia sasa ni fujo, sijui nini kimewapata. Wapo radhi nchi iingie vitani kuliko wananchi kunufaika na rasilimali zake eti kisa sifa zitamwendea Rais. Hapa ndipo ninapopata mashaka, kuna msemo unasema 'ukizoea kupinga au kubisha kila kitu mwishowe akili yako inaingia sumu na kuanza kujipinga au kujikana mwenyewe', sasa ndipo tulipo, wapinzani wanajikana.
Ukiangalia leo, Lema,Tundu,Msigwa,Mnyika ambao walishawishi wanchi waandamane ili rasilimali zisitoke bila masilahi yao kuzingatiwa leo wanapiga debe rasilimali hizo zitoke tu huku wakiweka vitisho na kuungana na makaburu,bure kabisa. Nikikumbuka jinsi kambi ya upinzani ilivyojipatia sifa zama za gesi ya Mtwara kwa kuungana na wananchi lakini leo wanawakana wananchi nawaonea huruma.
Wito, lazima mjue wananchi wanawaona vituko mnavyofanya mwaka 2020 sio mbali na hawatawaacha, mtapigwa ngwara kali kisiasa itakayowaacha hoi. Endeleeni kutumika na mabepari huku wakiwalipia kupata fursa ya picha zenu kukaa ukurasa wa mbele wa magazeti.
Nawasilisha