Kama nchi inakuthamini, urafiki unakuwa wa kudumu

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,034
1632577704784684.jpg

Na Fadhili Mpunji

Niliposoma maoni ya Rais Xi Jinping kwenye barua aliyoiandika tarehe 14 Septemba kukumbuka mchango wa Bw. Edgar Snow, Bw. Shafick George Hatem, Bw. Louis Eli, na Bw. Israel Epstein nilifarijika sana. Kilichonifanya nifarijike ni kwamba bila kujali wewe ni nani, uliotoa mchango kwenye sekta gani, au ni lini ulitoa mchango huo, taifa la China halitakusahau.

Barua hiyo pia inatia moyo kwa kuwa sio tu watu waliotoa mchango kwa China ndio wanakumbukwa, hata familia zao zinakumbukwa. Na kuwepo kwa wawakilishi wa familia hizo, ni ushahidi ulio wazi.

Baadhi ya tulioko hapa ni wawakilishi wa wageni waliotoa mchango kwa maendeleo ya China, na wale wanaoendelea kutoka mchango kwa China. Kwa hiyo barua kama hiyo ya Rais Xi Jinping, sio kama tu inaonyesha kwamba China inawajali marafiki zake, lakini inawakumbuka hata miongo kadhaa baada ya kuondoka hapa duniani. Lakini zaidi sio wao tu, inawakumbuka pia ndugu wa watu hao. Hili ni jambo la kutia moyo, na linaonyesha kuwa unapokuwa rafiki wa China, na unapotoa mchango kwa maendeleo ya China, basi una nafasi kwenye moyo wa China.

Leo tunakutana hapa wakati dunia inakabiliana na changamoto mbalimbali. Kuna janga la COVID-19 ambalo linaendelea kusumbua dunia nzima, na kuna changamoto kubwa za kiuchumi zinazotokana na changamoto hiyo. Hizi ni changamoto zinatotukabili binadamu wote, tulioko hapa China leo hii, na walioko nje ya China.

Huu ni wakati muhimu kuliko wakati wowote ule kuonyesha moyo wa urafiki, kuungana mkono zaidi, na kutoa mchango zaidi katika kukabiliana na changamoto hizo. Na sio kuchochea tofauti, zitakazofanya utatuzi wa changamoto hizi uwe mgumu.

Baadhi ya watu waliotoa mchango kwenye maendeleo ya China, kama waliotajwa na Rais Xi kwenye barua yake, inawezekana hawakujua kama China ya leo itakuwa na maendeleo kama iliyonayo sasa. Lakini ni wazi kuwa, wataona fahari sana kwa mchango waliotoa kwenye kuifikisha China hapa ilipo, kwani China ya sasa pia inatoa mchango mkubwa kwenye maendeleo ya duniani, iwe ni kwenye sekta ya uchumi, usalama wa dunia na hata kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Dunia tunayoishi ni ndogo sana. Changamoto zilizopo zinaonyesha kuwa hatma yetu inafungamana. Kwa hiyo ni kwa kuimarisha urafiki uliopo ndio tunaweza kuondoa changamoto hizo kwa pamoja na kuwa na siku nzuri zaidi za baadaye.
 
Kitendo cha Muafrika kumkataa Mzungu na Kumbabaikia Mchina ni Upumbavu. Si mchina Si Mzungu wote ajenda yao ni moja ya Kuchuma mali Afrika kwa Manufaa yao wenyewe. Waafrika tuamke.
 
Back
Top Bottom