Kama Nape, Mwigulu, January na sasa Kigwangalla wameathiriwa na siasa chafu basi "huyo" aliyeko nyuma ya Pazia ni mtaalamu haswa!

Kigwangala suala la Idriss sultan lazima likuondoe mana kawekwa ndani na mtoto pendwa ukatoa makauli yako baada ya hapo umempeleka mbuga ya Ruaha huwez pona hata urukeruke vipi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe utakuwa shabiki wa Mbumbumbu fc maana umezunguuuka weee kumbe uliumia sana kumkosoa huyo GABACHOLI wenu aliyetekwa kisha akavalishwa kangamoko then Vijana wakajitafunia 0713
Kigwangala anakurupuka sana kama mwanamke mjamzito. Juzi kaanza kuongelea maswala ya Dewji na simba, kama hana akili vile. Sasa waziri unaanza kuongelea mambo ya watu binafsi ambayo hayahusu wizara yako kwanini? Mara ajibizane na kina babu tale, debe tupu huyo jamaa. Mi nilimuona hamna kitu awamu ile ya Spika Makinda, akaanza kumnanga mama watu mitandaoni kama punguani. Akikosa ubunge yule ndo kwisha habari yake, mikopo itamuua. Kijana mdogo ameng'ang'ania mambo ya kizee. Ukiwa na mdomo sio lazima uongee. Hamna anaemtuhumu Kigwangala mdomoni, yanini yeye aanze kujibizana na watu na kutafuta ugomvi usio na maana?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe utakuwa shabiki wa Mbumbumbu fc maana umezunguuuka weee kumbe uliumia sana kumkosoa huyo GABACHOLI wenu aliyetekwa kisha akavalishwa kangamoko then Vijana wakajitafunia 0713

Sent using Jamii Forums mobile app
nawewe ni mja mzito? mbona vijana mnapenda kukurupuka sana? Soma hapa 👇
Tokea mwanzo mimi nilisema ' kina Kilomoni hawako sahihi kubania nyaraka za mali za Simba lakini potelea mbali, if I had to choose I'd choose the lesser evil of not letting Dewji anywhere near those documents".

Dewji ametulaghai na mbwembwe nyingi na kina Hans Pope za usajili wa makelele mengi wakati hauna matunda.

Simba ni timu ya watanzania, hapa ndipo wachezaji wazuri wote wa Tanzania walitakiwa wazaliwe na wachezee. Sasa Simba imekuwa sehemu ya kwenda kula hela. Wachezaji wangapi pale wanajitoa kwasababu ya jasho la wanasimba? Hakuna.

Na laana iwafikie wote wanaosema tunajenga Simba kwa matokeo ya baadae, mpira haupo hivo. Timu za mpira wa miguu zinajengwa na wachezaji wenye umri mdogo ili waje kutawala baadae. Usajili wetu wa kutulaghai kuona hatukamatiki umejaza wachezaji wenye miaka 25 na zaidi. Angalieni timu kama Madrid, Mazembe, Barcelona na timu nyingine zote kubwa. Mafanikio ya timu hizi yametokana na usajili wa vijana wadogo. Huwezi kufanya usajili wa wachezaji kutoka India utegemee utasaidia timu kukua.

Tena bora Serikali imegundua na kusema kama ni mgeni aje akiwa ana nafasi timu yake ya taifa au anacheza ligi ya juu nchini kwao.

Ulaghai wa usajili wa fujo ili tumuonee huruma awe na masifa huko FORBES kwamba anamiliki timu yameanza kuthibitika, Mo Dewji ni tapeli na hajui anafanya nini na simba. Wazee walimpa nafasi aweke US 1 million kama alivoahidi wampe nyaraka akagoma kwasababu hana nia ya dhati ya kuipaisha Simba zaidi ya kutaka sifa tu.

Ubunge wa Singida ulimshinda kwasababu ya misifa, alijidai ataibadilisha Singida lakini wapii, Singida ina hali mbaya vile vile tangu na tangu.
Jamaa anapenda sifa tu, hawezi kufanya la maana lolote.

Mimi Simba siwezi kuacha kushabikia, ila mzuka wa kwenda uwanjani kuiangalia umepungua kwa kiasi kikubwa. Sasa hivi nahisi kama Simba sio sehemu yangu tena, imekua kama ni mali ya mtu hivi.

Simba haijawahi kuwa mali ya mtu, ni timu ya wanaSimba.

NAPENDEKEZA TUWE NA MFUMO WA RAISI WA SIMBA NA SIO MMILIKI, KAMA AMBAVYO MADRID IPO.

Unasajili wachezaji kutoka India ambako hakuna mpira kabisa ili kutupumbaza watu ionekane umesajili vitu vya maana. Bahati nzuri njia ya muongo fupi, anataka sifa za kua anamiliki timu wakati sisi washabiki tunateseka. Mali za Simba hazitakiwi kuguswa na mikono ya nuksi ya Dewji.
Mlaghai mkubwa wewe.
 
Watu wanajaribu Kumshusha ila ukweli utabaki kuwa hakuna mtu aliyesoma Muhimbili asiwe na akili kichwani...

Tena kipindi hicho huwezi ingia Muhimbili bila kuwa na Div 1or 2 ya Mwanzoni tena iwe Pcb ...

Sent using Jamii Forums mobile app

Akili au busara haziambatani na div 1, au kuwa na elimu kubwa. Reasoning na kufikiri kabla ya kunena ni vipawa tofauti na elimu kubwa
 
Watu wanajaribu Kumshusha ila ukweli utabaki kuwa hakuna mtu aliyesoma Muhimbili asiwe na akili kichwani...

Tena kipindi hicho huwezi ingia Muhimbili bila kuwa na Div 1or 2 ya Mwanzoni tena iwe Pcb ...

Sent using Jamii Forums mobile app
Wabongo wengi exposure ni zero kuna watu we gi tu wamesoma muhimbili na UDSM wamepta division 3 form 6,ulikuwa huingii muhimbili au UDSM bila dvsn 1 au 2 kama unafadhiliwa na bodi ya mikopo ila kama ulikuwa unajisomesha mwenyewe ulikuwa unaweza kusoma hata kama ulipata division 3 form 6.
 
Ndio Johnthebaptist nasema kama hawa almaaruf wanne wametendewa hivi huko CCM basi ni hakika huyo Producer aliyeko nyuma ya Pazia ni mtaalamu kweli kweli.
Nape ,Mwigulu na January wameponzwa na siasa za kitoto haswa tamaa ya urais
Kigwangallah anaumizwa na siasa za ulaji wizarani
Majangili yanajipenyeza ili kunchafua waziri kwa kuwa amezidi unoko,Tembo wanafungwa GPS,doria ni kwa kutumia ndege isi na rubani,ukikutwa porini hutoki siku hizi ndio maana wanamchukia Hamisi
 
Nape ,Mwigulu na January wameponzwa na siasa za kitoto haswa tamaa ya urais
Kigwangallah anaumizwa na siasa za ulaji wizarani
Majangili yanajipenyeza ili kunchafua waziri kwa kuwa amezidi unoko,Tembo wanafungwa GPS,doria ni kwa kutumia ndege isi na rubani,ukikutwa porini hutoki siku hizi ndio maana wanamchukia Hamisi
Na alivyowapa akina Steve Nyerere na Mpoto hela zetu za kodi je

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani sipati picha Ngugai ndio mkuu wa chuo,hao wasomi wanaotoka hapo watakuaje,wakifata mawazo yake
Hapi, Gambo, Makonda, shilole, Harmonize, hawa wanaingia mjengoni na Bashe atakua waziri kamili wa kilimo huku tulia akiwa spika kamili wa Bunge na Ndugai atakua mwenyekiti wa bodi au mkuu wa chuo mark my words


Sent from my iPhone using JamiiForums

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wabongo wengi exposure ni zero kuna watu we gi tu wamesoma muhimbili na UDSM wamepta division 3 form 6,ulikuwa huingii muhimbili au UDSM bila dvsn 1 au 2 kama unafadhiliwa na bodi ya mikopo ila kama ulikuwa unajisomesha mwenyewe ulikuwa unaweza kusoma hata kama ulipata division 3 form 6.
Bado napingana nawe katika hili....Si Suala la bodi ya mikopo ila ni uhalisia Muhimbili hasa Md sio nyinginezo walitaka sana div 1&2 Hata mfumo tu wa Tcu (Tanzania central university)ulikuwa ukidahili sana wenye Point kubwa...

Udsm na Muhimbili kuna kozi nyingi sana unasoma hata ukiwa na div 3 ila Md na baadhi ya kozi za Engineering ushindani ni mkubwa sana!!


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom