Kama namuona dr. W. Slaa siku matokeo ya uchaguzi yatakapotangazwa mwakani 2015

msumeno

JF-Expert Member
Aug 3, 2009
2,833
2,000
Sipati Picha Siku matokeo ya Uchaguzi yatakapo tangazwa na tume ya uchaguzi mwaka 2015.

Najiandaa kwa kauli nilizozizoea kama hatumtambui, hatukubali,, tunakwenda kwa wananchi na kauli kama hizo,maana sioni maadalizi murua yenye malengo ya kubadili dola iliyopo.

Heri mh. Lipumba yeye kashazoea.
 

Mkya

JF-Expert Member
Dec 15, 2013
667
0
Slaa hatagombea mwaka huuu ukawa utampitisha mwenyekiti Mbowe makamu seifu
 

Gsana

JF-Expert Member
Aug 28, 2010
4,399
1,500
nadhani ni bora kwa dr slaa ambaye anajulikana kuwa anaweza kugombea tena, sio kama wale wengne kama wamechanganyikiwa hawajui atapita nani! chama kimoja kina wagombea zaidi ya 5 na wote hawaaminiani na kupeana onyo kila mara, kwao urais umekuwa rahisi kwa sababu ya uongozi uliopo sasa!!
 

singsong

Member
May 7, 2014
78
0
Hahaha kwa hiyo kujitokeza kwa wagombea wengi ni kuchanganyikiwa ? Ndugu hapa napata wasiwasi na kufikiri kwako . Hiyo ni fursa na demokrasia lazima iruhusu kila mwenye haki kugombea na baadaye kumpata aliyechaguo la watu. Sasa wewe unaweka mtu mmoja tena ambaye aligombea akakosa hivi unafikiri waliomkataa 2010 wamekufa au ? Amkeni achani kulala na kuota ndoto za mchana.
 

msumeno

JF-Expert Member
Aug 3, 2009
2,833
2,000
Lipumba hatakubaliwa na wanachama wake wahafidhina akae pembeni hali kadhalika Dr slaa.. hapo ndo Moto unapowaka kwa NCCR wao hawana neno wao wanaangalia upepo ila sidhani kama Kafulila atakaa kimya maana bado anadukuduku na CDM kwa issue yake ya kitambo na ya mshikaji wake ZZK.... wakati haya yatapokuwa yakitokea Kinana atakuwa anaendelea kuvuna wanachama wapya kama kimbunga..... tuombe uzima
 

king kan

JF-Expert Member
May 6, 2011
1,504
2,000
Leo nimecheka kwa mara ya kwanza nikiwa Jukwaa la Siasa. Ni vigumu sana UKAWA wakatoa mtu kwa sababu itamaanisha aidha watengeneza chama kimoja au wapeane sapoti katika uchaguzi kitu ambacho utekelezaji wake utakuwa mgumu sana. Vyama vyote vinatofautiana itikadi na sera kukubaliana vyote viwe na itikadi moja na sera zinazofanana ni swala litakaloacha mgogoro kwa wahafidhina. Na wakisema wasapotiane wakubali kuwa kuna sehemu kama Kigoma huo ndio utakuwa mwisho wa CHADEMA na mwanzo mzuri kwa NCCR, bado equation ya Kawe. Yangu macho. Pamoja na yote Dr. Slaa hawezi kuwa Rais wa nchi hii. Niwatakie mwaliko tukutane Uwanja wa Taifa Novemba ya 2015 tukashudie kuapishwa kwa Mh. Edward Ngoyai Lowassa Rais mteuli wa awamu ya tano.
 

singsong

Member
May 7, 2014
78
0
Ndugu king kan mimi sina tofauti sana ila ukawa ndio sanduku la kuzikia upinzani Tanzania kwenda kuungana bungeni bila ridhaa na hakuna katiba inayoonyesha ni mambo yapi tunashirikiana ni bomu la uchaguzi 2014 na 2015 kwa upinzani
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom