Kama na Makampuni ya Tanzania nayo yangeiga hivi basi leo hii nami ningekuwa nafukuzana na Dangote

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
59,949
119,214
Ni kwamba Mahakama moja huko jijini Accra nchini Ghana imeamuru Kampuni ya Johnsons & Johnsons kumlipa Mama mmoja jumla ya dola za Kimarekani Milioni Mia Moja ( USD 100 Million ) kwa Kosa la kumsababishia Mwanae Mtoto mchanga kupata Saratani ( Kansa ) ya Ngozi baada ya kutumia Powder yao ambayo inasemekana ilikuwa na madhara ya Kiafya kwa Watoto kutokana na Kemikali zake.

Hapa ndipo nami sasa nimeanza kujiuliza maswali mengi sana kwamba kumbe na Mimi pengine nilipokuwa nafungua Soda fulani nakutana na Mende ndani ningeenda kushtaki Mahakamani basi leo nami ningekuwa Tajiri au kama hivi majuzi tu nimetoka kununua Godoro la Kampuni moja hivi lakini sasa ni wiki ya pili sipati usingizi na nahisi labda kuna Kemikali ambayo imeniingia mwilini na kuweza kumaliza usingizi wangu wote kwani cha kushangaza nikisema nilale tu chini ya Sakafu nasinzia ' fasta ' tu au kuna aina fulani hivi ya dawa ya Viatu ambayo kiukweli kila nikipakaa tu katika Viatu vyangu basi vinaanza ' kubabuka ' ngozi na ni jana tu usiku nimetoka kununua Chakula katika moja Kampuni fulani hivi ambayo kila uchao inajitangaza redioni, runingani na hata katika mitandao ya Kijamii lakini tokea nile chakula chao jana naona ' spidi ' yangu ya kuelekea ' Maliwatoni ' imeongezeka ' maradufu ' na sasa naanza kukosa nguvu hali ambayo nahisi labda kile Chakula kilikuwa kibovu.

Hivi jamani kwa haya matukio mabovu na ya hatari yaliyotokea baada ya Mimi kutumia au kupata huduma kutoka katika hizo Kampuni nne ( 4 ) hapo juu nikisema nami ' nikawashtaki ' siwezi kulipwa ' Matrilioni ' ya Pesa kiasi labda cha kubadilisha umasikini wangu huu ' uliotukuka ' na kunifanya nianze kushindana Kiutajiri na Tajiri Aliko Dangote?

Mwisho nitoe tu Wito kwa Makampuni ya Kibiashara yaliyopo hata nchini Tanzania kuwa hebu basi na nyie igeni huo mfano mzuri kabisa wa hiyo Kampuni ya Johnsons & Johnsons inayotengeneza Baby Powder kwa kulipa fidia kwa Mteja wao baada ya ' kudhurika ' na bidhaa yao kwani ni ukweli usiopingika kwamba Makampuni mengi ya Tanzania bidhaa zenu ni ' hatarishi ' mno na zipo zingene ambazo pengine zimeshasababisha ama Vifo au Ulemavu wa kudumu kwa Wateja wenu.

Nawasilisha.
 
Sue them...lkn lazima upate scientific proof ....juu ya hilo godoro kwamba lina kemikali zenye madhara
 
Dah! hiyo mimaji ya sumu wanayoporomoshewa wakazi wengi wa dar wangeuaga umaskini
 
Ukicopy habari uwe unakumbuka kuacknowledge source plz.Hiyo habari ishaandikwa tayari bongo5.com na millardayo.com wewe unakuja humu kutujazia thread tu .

Pathetic
 
Ninafikiri hill linawezekana kama mkemia mkuu akiwa muungwana, na asipokee rushwa.
Swali kama utalipwa eg 10,000 usd kampuni ikaona bora watoe 1,000 usd kwa mkemia kubadili matokeo. Huoni utakua umepoteza muda bure na aibu juu?. Aaaah inakera sana. Ila jaribu ushindwe, kuliko kutojatibu ukafaniiwa.
NIMTAZAMO TU.
 
Watatuma mafia wa kukodi wakuue.Uliza wako wapi wakemia waliochoma unga wa ngano, yuko wapi mkemia wa awamu ya nne.
Kuna mambo hapa TZ inabidi usiwe na ufahamu ndio upambane nayo.
 
Back
Top Bottom