Kama mwalimu wake na Nyerere Bado yu hai ......

Papa D

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
753
182
Majuzi kwenye habari ilielezwa kuwa Mwalimu aliyemfundisha Nyerere yu hai na ana umri wa miaka 122. World geinness book inaonyesha mtu mwenye umri mkubwa aliye hai hadi hii leo ana miaka 115 na siku 28[today's 24/09/2011 record]!
Kwa nini Serikali ya ccm isimfanyie mpango kwa kukusanya kumbukumbu zake ili aingizwe kwenye hicho kitabu angalau nasi jina la nchi yetu alitangaze?
HEBU JAMANI TUJADILI NAMNA YA KUMSAIDIA HUYU MZEE ANGALAU AAMBULIE HIYO HESHIMA YA KUTAMBULIWA NA DUNIA NZIMA!!
mNALIONAJE HILI?
 
Aisee, hii habari ni ya kuvutia! Kama ni kweli inabidi tufanye jitihada hata sisi wenyewe hapa JF kuweza kumpatia mzee huyu hadhi yake anayostahili kwenye vitabu vya kumbukumbu na rekodi mbalimbali, hapa Tz na duniani pote kwa umri huo!!
 
juzi kuna mtu mwenye miaka 135 alikufa kigoma TBC kigoma ilitangaza lakini kama kawaida tv yet haivioni vya msingi kama hivi ,TBC dar es salaam haikutangaza habari hii
 
Nadhani tatizo kubwa ni kuwa wazee wengi Wa zamani hawana vyeti vya kuzaliwa vilivyotengenezwa wakati alipozaliwa.

Wengi wanatengeneza vyeti wakishakuwa watu wazima au kuandikishwa shule na hivyo umri wao huwa wa makisio tu
 
Gaijini!
Kinachotakiwa ni ushahidi si lazima viwe vyeti vya kuzaliwa!
Tatizo mi naona ni ustawi wa jamii kutofanya kazi yake na kutojua umuhimu wa kuweka vitu kama hivi kwenye kumbukumbu za Dunia.
Vina mchango mkubwa sana kutathmini maendelea ya nchi husika na afya za watu wake!!
 
juzi kuna mtu mwenye miaka 135 alikufa kigoma tbc kigoma ilitangaza lakini kama kawaida tv yet haivioni vya msingi kama hivi ,tbc dar es salaam haikutangaza habari hii
kama vile sijaelewa? Kwani huko kigoma tbc ina habar tofaut na dar? Pole nataka elewa tu
 
juzi kuna mtu mwenye miaka 135 alikufa kigoma TBC kigoma ilitangaza lakini kama kawaida tv yet haivioni vya msingi kama hivi ,TBC dar es salaam haikutangaza habari hii

Mbona wapo wengi tu Mkuu! Shangazi yangu mwenyewe ana miaka 125 sasa hivi (ametengeneza ki-ukoo chake cha zaidi ya watu 300 sasa hivi) lakini hajulikani popote zaidi ya wanandugu.

Tatizo letu wa-TZ ni kuona kila kitu cha kawaida tu, utafikiri hatuna wasomi hii nchi.

Maana hizi habari zingekuwa zinasaidia sana kuwafikia hata hao wenye kitabu chao cha World Guiness Book.
 
Majuzi kwenye habari ilielezwa kuwa Mwalimu aliyemfundisha Nyerere yu hai na ana umri wa miaka 122. World geinness book inaonyesha mtu mwenye umri mkubwa aliye hai hadi hii leo ana miaka 115 na siku 28[today's 24/09/2011 record]!
Kwa nini Serikali ya ccm isimfanyie mpango kwa kukusanya kumbukumbu zake ili aingizwe kwenye hicho kitabu angalau nasi jina la nchi yetu alitangaze?
HEBU JAMANI TUJADILI NAMNA YA KUMSAIDIA HUYU MZEE ANGALAU AAMBULIE HIYO HESHIMA YA KUTAMBULIWA NA DUNIA NZIMA!!
mNALIONAJE HILI?

Guinness
 
Back
Top Bottom