Kama mwalimu wa Rais Samia anapata uteuzi 2022, Vijana twafwa!

Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
21,563
50,406
Vijana wa nchi hii yatupasa tuungane pasipo kujali vyama vyetu tupiganie haki zetu kwa umoja wetu.

Pamoja na utofauti wa itikadi zetu lakini kuna masuala yafaa tupaze sauti kwa pamoja

Inakera na kuudhi kuona vijana tunakosa ajira halafu wastaafu wakiteuliwa kushika nyadhifa kila uchwao. Sitaki kutaja majina lakini kila mmoja wetu afuatilie.

Funga kazi ni uteuzi wa huyu mwalimu wa mhe Rais SSH. Kama Rais SSH ana miaka 62 vipi umri wa mwalimu wake?? Vijana ni lini tutateuliwa??

Mhe Samia alikuwa form 2 mwaka 1974

Screenshot_20220521-221644.png
 
Hakuna kitu ambacho huwa sipendi kama vyeo vya kulipa fadhila, hivi ndio vinatuharibia Nchi yetu tulitawaliwa na watu wabovu na tutaendelea kutawaliwa na wabovu, Utasikia fulani Kikwete, mara Mwinyi, Karume, mara Nape, mara Makamba, mara Kinana.....etc
 
Vijana wa nchi hii yatupasa tuungane pasipo kujali vyama vyetu tupiganie haki zetu kwa umoja wetu.

Pamoja na utofauti wa itikadi zetu lkn kuna masuala yafaa tupaze sauti kwa pamoja

Inakera na kuidhi kuona vijana tunakosa ajira halafu wastaafu wakiteuliwa kushika nyadhifa kila u hwao. Sitaki kutaja majina lkn kila mmoja wetu afuatilie.

Funga kazi ni uteuzi wa huyu mwalimu wa mhe rais SSH. Kama rais SSH ana miaka 61 vipi umri wa mwalimu wake?? Vijana ni lini tutateuliwa??
 
Funga kazi ni uteuzi wa huyu mwalimu wa mhe rais SSH. Kama rais SSH ana miaka 61 vipi umri wa mwalimu wake?? Vijana ni lini tutateuliwa??
Pole yako mkuu, nasimama nawe, lakini nakusihi usiishie hapo pa kulalama tu! Jihoji ni kwa nini inakuwa hivi lakini; vijana ni sehemu ya tatizo?

Tazama huko kwa makini sana.

Lisingekuwa "sehemu ya tatizo", nina hakika nchi hii ingekuwa ni tofauti sana na ilivyo sasa.
 
Nina uhakika kwa asilimia zote kwamba kama aliyeteuliwa angekuwa baba yako au ndugu yako usingelalama hapa
 
Vijana wakipewa nafasi wanaaza kuteka na kutisha watu...
hii awamu ni ya wazee awamu yenu ilishapita, watu washa umwa na nyoka wakiona jani tu wanashtuka.
 
Kichwa cha mwenda wazimu nasikia saiv power button ime toka, controller ana pata shida kuhamisha channel
 
Back
Top Bottom