Hakika asingehama CCM ila angejitokeza hadharani na kumpigia kamapeni Dr.Slaa. Na hili lingewashangaza wengi ila ukweli ndo huo kwa sababu alikuwa anapenda watu wenye uzalendo na nchi yao. Na ndipo hapo maneno yake ya kusema Chadema ndicho chama upinzani makini kinachoweza kuendesha dola yangetimia.
Mi nadhani angelikuwa ameisha anzisha chama kingine chenye kuzingatia maslahi kwa Taifa letu. Nahisi hali ya kisiasa isingekuwa kama ilivyo sasa maana angelimuunga mkono mgombea wa CHADEMA na angekuwa amewashawishi Wananchi wa vyama mbalimbali kumuunga mkono na kumpigia kura DR. Slaa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 2010- 2015.
KAMA MWALIMU NYERERE ANGELIKUWA HAI LEO
Kwa Tanzanite peke yake ,kila mtanzania angesoma hadi chuo kikuu kwa gharama ya zawaidi hii(TANZNITE) MUNGU alioipa Tanzania peke
yake duniani.Jamani tuseme tu ukweli hata kama ni kufa,Nyerere pekee ndie mkombozi wa kweli kama Yesu, aliwahi kuwepo,na kwa mwendo huu wa sasa hakuna dalili ya ukombozi labda MUNGU afanye mabadiliko katiika uongozi wa nchi hii.MUNGU tunakuomba mabadiliko.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.