Kama mwajiri, nakusudia kumfukuza kazi Rais tarehe 28, Oktoba kwa kushindwa kutimiza ahadi

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
39,702
71,013
Wadau wa JF,

Mimi ni Mtanzania mpiga kura halali na 2015 nilimsikiliza huyu mweshimiwa nilipompa nafasi ya kusema sera za chama chake na yeye binafsi atazifanyia kazi namna gani.

Alinishawishi kwa mengi sana katika Afya, Elimu, miundombinu, ulinzi wangu, Uhuru wangu kulingana na Katiba, furaha na amani pia heshima ndani na nje ya nchi kama Mtanzania.

Kutokana na ahadi zake, nikampa ajira ya Urais kwa miaka 5 under probation, ili kama atathibitisha ubora nitampa 5 nyingine.

Sasa ni tofauti, sio kwamba hajafanya kitu, la hasha! Amefanya ya kutosha kama mwajiriwa lakini mengi sio kwa mipango kama nchi bali ameamua kutumia kichwa chake (one man show) na kutuvuruga.

Pili ameshindwa kabisa katika mambo muhimu kama Uhuru wa habari na kujieleza, ulinzi wa raia, Elimu, Ajira, heshima ndani na nje, mahusiano nk.

Kwa kushindwa kwake kutimiza wajibu nataka nimfukuze kazi 28 Oktoba, 2020. Je, ni lazima kumuandikia barua ya kusitisha ajira yake au nimpige kimya kimya kwa sanduku la kura?

Je, kama atatumia vibaya madaraka niliyompa 2015 na kutoheshimu maamuzi yangu ya sasa na aka ng'ang'ania hatoki napaswa kufanyaje kama mwajiri?.
 
Factors for fall of CCM empire.

1. Corruption . Example kukopa Trilion 40

2. Bunning of opposition parties. Example CHADEMA

3. Absence of free mass media and freedom of speech.

Hizi baada ya miaka mi 3 tutaanza kuzisoma ata Roman empire ilikufa ivi ivi
 
Naam, jamaa anastahili kula 24 hrs notice, ameshindwa kutekeleza kiapo chake.
Na in haki ya mwajiri (mpiga kura) kumuwajibisha mtumishi asiyefikia malengo.
Haya Rais tulimpa mamlaka ya kutumbua watendaji wabovu, hivyo wapiga kura waweza nao kutumbua
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom