Kama Mungu aliumba mbingu na dunia, sayari nyingine je?

maramia

JF-Expert Member
Jul 17, 2015
2,030
1,345
Vitabu vitakatifu, Quran na Biblia vyote vinasema Mungu wakati wa mwanzo wa uumbaji wake, aliumba mbingu na nchi (dunia).

Kuna jambo moja linalonisumbua kwa muda mrefu ambalo ningependa wajuzi wa elimu ya dini au yeyote mwenye uelewa anipe majibu.

1. Kama Mungu aliumba mbingu na dunia (nayo ni sayari), sayari nyingine kama Venus, Mars, Jupiter, Uranus n.k ziliumbwa na nani?

2. Kama sayari hizo zina viumbe hai wenye uwezo kama binadamu tulionao wanamuabudu nani, ni Mungu huyu wetu tunayemwabudu au wao wana Mungu wao?

3. Ilikuwaje uwepo wa viumbe (kama wapo) hai kwenye sayari hizi haukutajwa katika vitabu vitakatifu na manabii au mitume? mpaka binadamu waanze wenyewe utafiti?
 
Mungu aliumba mbingu na dunia labda tuanzie hapa katika kujibu maswali yako:
Vitabu vitakatifu vinapotaja neno "Mbingu" maana ake ni "Universe/ heavens" katika lugha ya kiingereza. Na neno Dunia ikimaanisha sayari kwahuyo Mungu aliumba mbingu/ universe na vyote vilivyomo kama sayari dunia ikiwa kiwakilishi.
Ukisoma vitabu hivyo kama Biblia kwa lugha ya kiingereza vinasema "At the beginning God created heavens and earth. Ukiendelea mbele Biblia inasema akaumba viumbe vinaovyoonekana na visivyoonekana. Mpaka hapo utaona kwamba Mungu huyo ndio Mungu mkuu "The creator"
Yawwzekana kukawa na viumbe vya kwajinsi yake (by its own kind different from human being au Carbonated beings ) ambavyo maisha yao sio ya kutegemea oxygen kama sisi na havionekani kwa macho yetu haya ya nyama, vikawepo either hapa hapa duniani au kwenye sayari zingine. Lakini according to the Holly books Mungu ndiye injinia, muumbaji wa vyote maanake hata vyenyewe vinamwabudu Mungu huyo kwa namna ambavyo vyenyewe vinajua.
 
Kama Mungu aliumba mbingu na dunia (nayo ni sayari), sayari nyingine kama Venus, Mars, Jupiter, Uranus n.k ziliumbwa na nani?

2. Kama sayari hizo zina viumbe hai wenye uwezo kama binadamu tulionao wanamuabudu nani, ni Mungu huyu wetu tunayemwabudu au wao wana Mungu wao?

3. Ilikuwaje uwepo wa viumbe (kama wapo) hai kwenye sayari hizi haukutajwa katika vitabu vitakatifu na manabii au mitume? mpaka binadamu waanze wenyewe utafiti?
1. Mungu aliumba ulimwengu, na ulimwengu si dunia wala nyota, dunia yetu ni moja ya familia ya solar yenye sayari 9 na baba wa familia hiyo ni jua, ambavyo vilizaliwa miaka milioni 4600 baada ya ulimwengu kuwapo, ukitaka kujua kwa usahihi kasome The Big Bang

2. Kutokana na ufinyu wa ufahamu wetu, wengi hudhani kuwa dunia ndio yenye viumbe hai peke yake hii si kweli, sola system iko ndani ya Milk way Galaxy, Milk way Galaxy hii inafamilia nyingi sana za kinyota ambazo kila familia ina viumbe hai, kwa ufupi Ulimwengu una zaidi ya Galaxies bilion 100, na kuna familia nyingi sana za kinyota zinazo kaliwa na viumbe hai

3. Uwepo wa viumbe hai ktk sayari nyingine haukutajwa na manabii wala mitume wanaodaiwa kuwa ni wa Kimungu kwa kuwa ufahamu wao ulikuwa mdogo sana kisayansi

Umeuliza kwamba km wapo viumbe hai kwenye sayari zingine wanamwabudu Mungu yupi?
wanatakiwa wamwabudu Mungu aliyeumba ulimwengu (Universe) ambaye anaitwa THE SUPER NATURAL POWER yaani nguvu ya asili, ina sikitisha kuona watu wa dunia hii hawaiamini nguvu ya asili, wana dini zao, kila dini ina kijimungu chake, wengine wanadai wanamwabudu Mungu wa Ibrahim, Isaka na Yakobo, wengine Ng'ombe, wengine Jua, wengine Mito, nk,
 
duru za utafiti zinaonesha kuna viumbe hai

na wewe nani aliyekuambia kuwa hakuna uhai huko?

una ushahidi?

Ushahisdi wangu ni kwamba hatujauona huo uhai. Sasa wewe sijui hizo duru zako za utafiti zimekuonyesha. Those are only speculations. There is a lot more to support life in a planet than mere soeculations.
 
Ushahidi wa kuwepo viumbe hai ni kwasababu ya kupatikana kwa:-
Methane, Amonia na Hydrogen ambazo ndio asili ya uhai
 
1. Mungu aliumba ulimwengu, na ulimwengu si dunia wala nyota, dunia yetu ni moja ya familia ya solar yenye sayari 9 na baba wa familia hiyo ni jua, ambavyo vilizaliwa miaka milioni 4600 baada ya ulimwengu kuwapo, ukitaka kujua kwa usahihi kasome The Big Bang

2. Kutokana na ufinyu wa ufahamu wetu, wengi hudhani kuwa dunia ndio yenye viumbe hai peke yake hii si kweli, sola system iko ndani ya Milk way Galaxy, Milk way Galaxy hii inafamilia nyingi sana za kinyota ambazo kila familia ina viumbe hai, kwa ufupi Ulimwengu una zaidi ya Galaxies bilion 100, na kuna familia nyingi sana za kinyota zinazo kaliwa na viumbe hai

3. Uwepo wa viumbe hai ktk sayari nyingine haukutajwa na manabii wala mitume wanaodaiwa kuwa ni wa Kimungu kwa kuwa ufahamu wao ulikuwa mdogo sana kisayansi

Umeuliza kwamba km wapo viumbe hai kwenye sayari zingine wanamwabudu Mungu yupi?
wanatakiwa wamwabudu Mungu aliyeumba ulimwengu (Universe) ambaye anaitwa THE SUPER NATURAL POWER yaani nguvu ya asili, ina sikitisha kuona watu wa dunia hii hawaiamini nguvu ya asili, wana dini zao, kila dini ina kijimungu chake, wengine wanadai wanamwabudu Mungu wa Ibrahim, Isaka na Yakobo, wengine Ng'ombe, wengine Jua, wengine Mito, nk,
unavyosema kwa uhakika kuwa kuna viumbe wengine, unauhakika!!???

Wazungu wenyewe wanatumia neno posibly !!
Ww unakuja na 100% kuwa wapo nani kakwambia !

Weka link inayosema kuwa kuna viumbe wengine!! Centauri proxima yenyewe ipo jirani bt unahitaji miaka zaidi ya 200 ya mwanga !! Acha porojo na tumia neno yawezekana.
 
Hakuumba mbingu na dunia aliumba mbingu na nchi na nchi siyo dunia tu
Na wewe " come down"ndo umeandika nini!? Nchi ni sehemu yaweza kuwa kavu na isokavu/kwa pamoja inayopatikana ndani ya dunia, mbingu ndio ina mjumuisho wa vitu anuwai. Usichanganyikiwe kijana.
 
hivi aliumba MBIGU na DUNIA au MBINGU na NCHI!?

Vitabu vitakatifu, Quran na Biblia vyote vinasema Mungu wakati wa mwanzo wa uumbaji wake, aliumba mbingu na nchi (dunia).

Kuna jambo moja linalonisumbua kwa muda mrefu ambalo ningependa wajuzi wa elimu ya dini au yeyote mwenye uelewa anipe majibu.

1. Kama Mungu aliumba mbingu na dunia (nayo ni sayari), sayari nyingine kama Venus, Mars, Jupiter, Uranus n.k ziliumbwa na nani?

2. Kama sayari hizo zina viumbe hai wenye uwezo kama binadamu tulionao wanamuabudu nani, ni Mungu huyu wetu tunayemwabudu au wao wana Mungu wao?

3. Ilikuwaje uwepo wa viumbe (kama wapo) hai kwenye sayari hizi haukutajwa katika vitabu vitakatifu na manabii au mitume? mpaka binadamu waanze wenyewe utafiti?
 
Mungu aliumba mbingu na nchi. Na kuna mahali kwenye Bible pia imeandikwa, "nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana, dunia na wote wakaao ndani yake." hapo unaona nchi na dunia zimetajwa tofauti. Hivyo Mungu aliumba zaidi ya dunia.
 
1. Mungu aliumba ulimwengu, na ulimwengu si dunia wala nyota, dunia yetu ni moja ya familia ya solar yenye sayari 9 na baba wa familia hiyo ni jua, ambavyo vilizaliwa miaka milioni 4600 baada ya ulimwengu kuwapo, ukitaka kujua kwa usahihi kasome The Big Bang

2. Kutokana na ufinyu wa ufahamu wetu, wengi hudhani kuwa dunia ndio yenye viumbe hai peke yake hii si kweli, sola system iko ndani ya Milk way Galaxy, Milk way Galaxy hii inafamilia nyingi sana za kinyota ambazo kila familia ina viumbe hai, kwa ufupi Ulimwengu una zaidi ya Galaxies bilion 100, na kuna familia nyingi sana za kinyota zinazo kaliwa na viumbe hai

3. Uwepo wa viumbe hai ktk sayari nyingine haukutajwa na manabii wala mitume wanaodaiwa kuwa ni wa Kimungu kwa kuwa ufahamu wao ulikuwa mdogo sana kisayansi

Umeuliza kwamba km wapo viumbe hai kwenye sayari zingine wanamwabudu Mungu yupi?
wanatakiwa wamwabudu Mungu aliyeumba ulimwengu (Universe) ambaye anaitwa THE SUPER NATURAL POWER yaani nguvu ya asili, ina sikitisha kuona watu wa dunia hii hawaiamini nguvu ya asili, wana dini zao, kila dini ina kijimungu chake, wengine wanadai wanamwabudu Mungu wa Ibrahim, Isaka na Yakobo, wengine Ng'ombe, wengine Jua, wengine Mito, nk,
Mungu anaitwa the super natural power? Sijakupata hapo mkubwa. Hebu fafanua kidogo. Pia kuna kitu Kizuri hapo umekiongelea the Big Bang!
 
Mambo ya biblia kaz ipo

Mie huwa najiuliza Sana.BIblia inasema siku ya kwanza mungu aliumba mchana na usiku..na pia inasema jua aliumba siku ya NNE..

Hapo kaz ipo sote tunajua mchana unatokana na jua ,sasa Siijui nuru aliyo iumba mungu siku ya kwanza ipo wapi??
 
Back
Top Bottom