Elections 2010 Kama Mume Kama Mke: Angalia Jeuri ya Salma Kikwete Ktk Twitter

Mzalendo_Mwandamizi

JF-Expert Member
Dec 12, 2007
1,117
4,764
5bnqdz.jpg


Dharau inayoonyeshwa na mgombea wa CCM Jakaya Kikwete kuendelea kutoa ahadi zaidi ilhali nyingi ya alizotoa mwaka 2005 hazijatimizwa,sasa imehamia kwa mkewe.Katika ukurasa wake wa Twitter (@salmakikwete),mke huyo wa Rais ameandika ""Tuwasikilize,tupembue chuya zikae upande wake,chenga upande wake na mchele ukae upande wake,tuseme lililo lililo la kweli,kama serikali haitatoza kodi,itaendeshaje shughuli zake?" Kauli hiyo pia inapatikana kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Kwanza,pamoja na kumheshimu kama First Lady lakini ilipaswa huyu mama akae kimya.Anatumia raslimali za taifa kumkapeni mumewe wakati anafahamu fika yeye (Salma) si mgombea.Huu ujasiri wa kinafiki wa kutetea kodi sijui unatoka wapi kwa vile tatizo letu kama taifa sio tu kwenye uzembe katika ukusanyaji kodi bali pia matumizi mabaya ya hata hiyo kodi ndogo inayokusanywa baada marafiki wa watawala kupewa misamaha ya kido kifisadi.

Hivi huyu mama anafahamu kuwa mumewe alipofanya ziara ya ghafla Bandari ya Dar es Salaam alitamka waziwazi kuwa anawafahamu watu wanaofanya ufisadi bandarini hapo?Na miongoni mwa ufisadi mkubwa sehemu hiyo ni dili za kukwepa kodi.

Sasa kama kweli ana uchungu na mapato ya serikali kwanini asimkumbushe mumewe kuhusu majina ya mafisadi wa Bandari ambao hadi dakika hii hajawataja au kuwasilisha majina yao kwa wahusika?

Kama unadhani namsingizia Kikwete hebu soma habari ifuatayoiliyochapishwa na gazeti la Nipashe la Machi 3 mwaka huu

Nawajua wanaosaidia kukwepa kodi TRA- Kikwete
2009-03-03 10:59:53
Na Joseph Mwendapole

Rais Jakaya Kikwete amesema ana orodha ya wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) wasio waaminifu ambao wanashirikiana na wafanyabiashara kukwepa kodi kwenye Bandari ya Dar es Salaam.

Alisema anaifanyia kazi orodha hiyo na akishamalizana nayo atamkabidhi Kamishna Mkuu wa TRA, Harry Kitilya, ili achunguze na kuwafukuza kazi wafanyakazi watakaothibitika kujihusisha na vitendo hivyo.

Aliyasema hayo jana wakati akizungumza na viongozi wa Mamlaka ya Bandari (TPA) na wadau wa bandari Tanzania alipotembelea Bandari ya Dar es Salaam ikiwa ni ufuatiliaji wa agizo alilotoa mwezi uliopita kupunguza msongamano wa makontena.
Alisema serikali haiwezi kuvumilia watu wanaoikosesha mapato.

Akitoa mfano namna wizi huo unavyofanywa, Rais Kikwete alisema wanaweza kuendesha zoezi hilo kwa simu ambapo mtu aliyeko Dubai anapewa maelezo namna atakavyojaza fomu ili mzigo wake usipite kwenye scanner, hali inayoweza kupitisha mizigo haramu kama dawa za kulevya.

Alisema wafanyakazi na wafanyabiashara hao wanatumia udanganyifu kuwa kontena hizo zimebeba mitumba, kumbe ndani ya mitumba hiyo wakati mwingine inatumika kufunika magari.

``Ninayo orodha ndefu na nitaikabidhi kwa Kamishna Mkuu wa TRA, Kitilya ili awafuatilie na ahakikishe anawatimua kazi mara moja wale watakaobainika wanahusika na mchezo huo ili tuanze upya,`` alisema.

Alisema serikali haiwezi kuvumilia kuwa na wafanyakazi wanaokula njama za kuipotezea mapato.
Kikwete alisema bandarini kuna uzembe mkubwa ambao hauvumiliki na aliuagiza uongozi kuondoa matatizo yaliyopo badala ya kukaa na kunung`unika.

Alisema msongamano wa makontena umekuwa ukiisababishia serikali kukosa mapato mengi na alisisitiza kuwa bandari ni sehemu muhimu ambayo serikali haiwezi kuiacha iwe ya hovyo.
Akiwa katika kitengo cha kuchunguza bidhaa katika kontena, Tiscan, Rais Kikwete alisema maelezo aliyopewa na TPA yanatofautiana na yale aliyopewa na viongozi wa Tiscan.

``Hapa mbona mimi sielewi naomba mnieleweshe, hawa Tiscan wanasema wana uwezo wa kuchunguza hata makontena 200 kwa siku ila wanasema tatizo ni nyinyi hamleti kontena za kutosha... Jamani fanyeni kazi na muachane na visingizio na malalamiko,`` alisema Kikwete.

Aliagiza mamlaka hiyo impe taarifa ya maendeleo ya utekelezaji wa upunguzaji wa makontena ndani ya wiki mbili zijazo na aliahidi kutembelea tena bandari hiyo.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Wakala wa Forodha, Otieno Igogo, alimweleza Rais Kikwete kuwa wadau wa Bandari ya Dar es Salaam walikubaliana kulipa dola 30 ikiwa ni gharama za kuhamishia kontena moja katika bandari kavu.

Igogo alimweleza Rais kuwa ingawa wadau wote wamekuwa wakichangia, Kampuni ya Kimataifa ya Kupakua Kontena Bandarini (TICTS), imegoma kutoa fedha hizo.

Alisema dola 30 ambazo TICTS walipaswa kulipa kwa kila kontena linalohamishiwa bandari kavu kama wanavyolipa wadau wengine, zimekuwa zikitolewa na TPA.

Baada ya kauli hiyo ya Igogo, Rais alisema anashangaa kuona jeuri hiyo ya TICTS na kusema kuwa TPA ina mamlaka, lakini haitaki kuyatumia.

Kikwete alisema TPA imefanya vizuri kulipa gharama ambazo TICTS imekataa kuzilipa, lakini aliagiza mamlaka hiyo ihakikishe TICTS inazirudisha mara moja.

``Nyinyi mnashangaza sana, mna mamlaka, lakini hamyatumii... Sasa hizi gharama lazima walipe na wakiwashinda mwelezeni waziri na waziri akishindwa niambieni mimi,`` alisema.

Wakati huo huo, Kikwete alikataa maelezo marefu ambayo Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Ephraem Mgawe, alitaka kuyasoma mbele yake na badala yake akamtaka amweleze sababu za msongamano kutoma lizika.

Baada ya kuelezwa hivyo, Mgawe alimweleza Rais Kikwete kuwa kikosi kazi kilichoundwa kufuatia agizo lake kinaendelea kujitahidi kuondoa msongamano uliopo.

Alisema Mamlaka inatarajia kuwa utekelezaji wa mikakati iliyowekwa itafanikisha kupunguza hali ya msongamano mwezi Machi mwaka huu.

Mgawe alisema katika kipindi cha mwaka 2007/08, TPA ilihudumia tani milioni 6.239, ambalo ni ongezeko la tani 227,222 au asilimia 3.8 ikilinganishwa na tani milioni 6.003 zilizohudumiwa mwaka 2006/07.

Alisema katika kipindi hicho mamlaka ilipata ziada ya Sh. bilioni 37.879 kutokana na mapato ya Sh. bilioni 168.789 na matumizi ya Sh. bilioni 133.909.
SOURCE: NIPASHE
Wito wangu kwa Salma Kikwete ni simple: kama alikuwa anataka kugombea uongozi angegombea lakini sio kuendelea kutumia raslimali za taifa kumkampenia mumewe.Anapaswa kutambua kuwa raslimali hizo zinagharamiwa na walipa kodi ambapo wengi wao si wana-CCM (takwimu za karibuni zinaonyesha wanachama wa CCM ni takriban milioni 5 tu kati ya Watanzania takriban milioni 45).

Tunatambua kuwa Salma anataka kuendelea kuwa First Lady lakini asifanye hivyo kwa kuwabebesha gharama Watanzania wote hata wasio wana-CCM.Anaweza kuitumia WAMA kumfanyia kampeni mumewe lakini Watanzania hawataki kuona ufisadi wa mchana mweupe unaofanywa kwa misingi ya kifamilia.

Naamini mwanamama huyu anafuatilia habari za kimataifa,na hivyo amesikia yaliyomkumba Vera Chiluba,mke wa aliyekuwa Rais wa zamani wa Zambia,Frederick Chiluba,aliyehukumiwa kwenda jela kwa ufisadi.

Ni vema Salma akasoma alama za nyakati ili pindi mumewe atakapokabidhi madaraka kwa Dokta Wilbroad Slaa hapo Novemba familia ya Kikwete isianze "kutafutana".

Na hiyo "tweet" yake ya kuchambua pumba na mchele nadhani ni vema akiielekeza kwa mumewe ambaye so far anaonekana kunogewa na "ugonjwa" wa kutoa ahadi.Mara uwanja wa ndege Kigoma,mara kuboresha kilimo cha kakao,mara atawapatia akinamama chanjo ya cervical cancer,mara vijiji 11 vya Mkinga vitapatiwa maji,mara hili mara lile alimradi ni "vurugu mechi ya ahadi".Kwani Rais wa Tanzania 2005-hadi sasa alikuwa nani kama sio Jakaya Mrisho Kikwete?Kwanini hayo anayoahidi sasa hakuyatekeleza katika awamu yake ya sasa?Na kwani tuamini kuwa atayatekeleza katika awamu yake ya mwisho-kipindi atakachokuwa bize kujitengenezea mazingira ya "kumpumzika kwa amani" kama Mkapa?

Blogu hii inawakumbusha tena wapiga kura kwamba Kikwete hayuko serious ndio maana ameamua kurejea nyingi ya ahadi zake za 2005 bila aibu wala kuwaomba msamaha Watanzania kwa kutozitekeleza.Kumrejesha tena Ikulu itakuwa ni kosa kubwa kupita kiasi kwani katika awamu yake ya mwisho atairejesha nchi yetu kwenye zama za mawe.

TANZANIA BILA UFISADI INAWEZEKANA
TANZANIA BILA CCM INAWEZEKANA
TANZANIA BILA KIKWETE,SIO TU INAWEZEKANA,BALI NI MUHIMU LAZIMA KWA USTAWI WA TAIFA LETU.
CHAGUA DOKTA SLAA KWA UKOMBOZI NA "UHURU WA PILI",CHAGUA CHADEMA KWA TANZANIA YENYE NEEMA.

KULIKONI UGHAIBUNI: Kama Jakaya Kama Salma: Soma Jeuri ya Salma Kikwete Ktk Twitter
 
Mkuu wangu labda nifahamishe vizuri.. ni chama gani kimesema hakitatoza Kodi?..
 
Mr. Sam Sitta a.k.a Mzee wa standards and speed au Six naye ameongelea kuhusu hili kuwa hakuna serikali duniani isiyotoza kodi. Mimi nafikiri hawa akina Sitta na Salima Kikwete hawajaelewa concept na context ya Dr. Slaa. Dr. Slaa alisema atapunguza kodi na kuondoa zile za manyanyaso. Sasa CCM wanataka kuongeza kodi na kuendeleza zile za manyanyaso. Miaka ya nyuma (1980 - 2000) kulikuwa na development levy (kodi ya kichwa) ambayo ilikuwa inanyanyasa sana wazazi wetu kule vijijini baadae ikaondolewa, je serikali hii hii ya CCM ilishindikana kuendeshwa? Dr. Slaa ni innovative na creative, anajua wapi atapunguza, wapi ataondoa kabisa, na wapi ataongeza!! Ndio maana hata waraka wa maaskofu walishindwa kuuelewa!!!!

Kwanza tumwuulize Sitta nini kwa nini Dodoma sio kama Abuja wakati yeye alikuwa mwenyekiti wa CDA? Je, alipata wapi zile fedha alizojengea ghorofa lake kule Urambo in 1980s wakati akiwa waziri wa ujenzi?
 
duh huyu jamaa wa kulikoni ughaibuni anapiga ngumi za uso noma

Unajua, Kikwete hana kumbukumbu nzuri. Anaweza kuongea jambo leo asubuhi, akakanusha jambo hilo hilo jioni yake, ndo sababu huwa mara nyingi anaonekana kituko. Sasa kama anadai anawafahamu wakwepa kodi, pamoja na kuwa na jeshi la polisi na vyombo vingine vya usalama, anadhani nani mwingine atawakamata? Huwa hafanyi analysis ya kutosha kabla hajatamka jambo.
 
Unajua, Kikwete hana kumbukumbu nzuri. Anaweza kuongea jambo leo asubuhi, akakanusha jambo hilo hilo jioni yake, ndo sababu huwa mara nyingi anaonekana kituko. Sasa kama anadai anawafahamu wakwepa kodi, pamoja na kuwa na jeshi la polisi na vyombo vingine vya usalama, anadhani nani mwingine atawakamata? Huwa hafanyi analysis ya kutosha kabla hajatamka jambo.
Wanasema ukiwa mwongo usiwe msahaulifu.......
 
"Anatumia raslimali za taifa kumkapeni mumewe wakati anafahamu fika yeye (Salma) si mgombea"

hapa rasilimali za taifa ni twitter au facebook au haina uhusiano na kuandika kwake kwenye twitter na facebook?

naomba ufafanuzi manake uandishi wako kidogo umenikwaza :confused2:
 
Kwa AFYA ya JK ilivyo na CCM "hawana" mtu mwingine zaidi ya JK tuache tu huyu mama amsaidie mumewe kututawala. Mama Salma wewe, kuliko mtu mwingine yeyote ndiye unayejua mumeo anaumwa nini, uwezo wake wa kuchapa kazi, msaidie tu mama hadi CCM ya akina Makamba, Msekwa, Kinana watakapozinduka.
 

Unajua, Kikwete hana kumbukumbu nzuri. Anaweza kuongea jambo leo asubuhi, akakanusha jambo hilo hilo jioni yake......

Kila anapokula mueleka na kuzimia, anapoamka tena huwa amefuta memory yote.
 
Jamani mwacheni Salma ajilie zake bata. Hata ningekuwa mimi nisingejivunga loh! Yaani mume anagombea kuendeleza mambo yazidi kuwa safi halafu nijiweke nyuma nyuma sababu gani? Nenda mama, sema mwenzetu, jiweke mbele huo ndio wajibu wa mwanamke kwa ampendae.
 
hapa hoja sio mama salma kuzunguka kupiga kampeni, hii ni haki yake ya kikatiba kufanya hivyo akiwa kama mtanzania
mwingine yeyote, hoja ni yeye kutumia rasilimali za serikali kuyafanya hayo, kama gharama hizi ni za chama mimi sina
tatizo lolote na mke huyu wa Rais, kimsingi anaweza pata jeuri ya kutokusikia maana mumewe yupo madarakani, ila ajue
hatakuwepo pale maisha yake yote, siku yake yaja pale watanzania watakapomuhoji kuhusu matumizi haya kama kweli
anatumia hela yetu ya kodi kwa shughuri binafsi.......
 
Jamani mwacheni Salma ajilie zake bata. Hata ningekuwa mimi nisingejivunga loh! Yaani mume anagombea kuendeleza mambo yazidi kuwa safi halafu nijiweke nyuma nyuma sababu gani? Nenda mama, sema mwenzetu, jiweke mbele huo ndio wajibu wa mwanamke kwa ampendae.

Nini mama Salma hata vimada wake wanaruhusiwa kumpigia kampeni ili mambo yawaendee safi. Cha msingi watumie rasilimali binafsi za mgombea au za chama chak lakini sio kutumia rasilimali za umma. katika rasilimali za umma hakuna ushosti, mahaba wala malavidavi. hekima, nidhamu na kufuata sheria katika matumizi yake kunatakiwa hivyo first lady aache ufujaji wa mali za umma kwa manufaa binafsi au ya kifamilia.aonewi wivu au kijicho afumbue macho na kuuona ukweli, watanzania wanaumia fedha anazofuja zinatakiwa kwa sana ajili ya wanawake wenzake wanaojifungulia barabarani badala ya hospitali tokana na ukosefu wa fedha
 
"Anatumia raslimali za taifa kumkapeni mumewe wakati anafahamu fika yeye (Salma) si mgombea"

hapa rasilimali za taifa ni twitter au facebook au haina uhusiano na kuandika kwake kwenye twitter na facebook?

naomba ufafanuzi manake uandishi wako kidogo umenikwaza :confused2:

we hujasikia akienda huko mikoani anavyopokewa na viongozi wa serikali na wanatumia magari ya serikali kwa shughuli zake za wama na kumpigia kampeni mumewe?na mikutano yenyewe anayoitisha ya kumsaidia prezidaaa haiko kwenye mtiririko unaotambuliwa na nec, yaani ni ufisadi tuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu
 
Licha ya dk slaa kumtisha mama salma kumfungulia mashtaka lkn mama salma hajibu, harudi nyuma anasonga mbele tu. nadhani chadema nao wangalitumia ushawishi wa viongozi wanawake (mama shida - mama zito) Bi halima Mdee na wengine ambao wazunguruke kupambana na mama salma kihoja , kwani swala la kumzuia nadhani litagonga mwamba huku mama huyo akionyesha ushawishi mkubwa kwa akinamama

Lakuvunda halisikii --------------------
 
Katika ukurasa wake wa Twitter (@salmakikwete),mke huyo wa Rais ameandika ""Tuwasikilize,tupembue chuya zikae upande wake,chenga upande wake na mchele ukae upande wake,tuseme lililo lililo la kweli,kama serikali haitatoza kodi,itaendeshaje shughuli zake?" Kauli hiyo pia inapatikana kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Anatumia raslimali za taifa kumkapeni mumewe wakati anafahamu fika yeye (Salma) si mgombea
Hii mpya! Toka lini Tweeter na Facebook zimekuwa raslimali za Taifa? Jaribu kuacha ulimbukeni mkuu.
 
Licha ya dk slaa kumtisha mama salma kumfungulia mashtaka lkn mama salma hajibu, harudi nyuma anasonga mbele tu. nadhani chadema nao wangalitumia ushawishi wa viongozi wanawake (mama shida - mama zito) Bi halima Mdee na wengine ambao wazunguruke kupambana na mama salma kihoja , kwani swala la kumzuia nadhani litagonga mwamba huku mama huyo akionyesha ushawishi mkubwa kwa akinamama

Natamani nicheke kwani huo ushawishi mkubwa wa Salma anao anashindwa hata kumshawishi jamaa asiwe na vimada nje ya nyumba sembuse ataweza ataweza kushawishi watu wazima na akili zao? Niliwasikia akinamama fulani walioenda katika mkutano wake Kawe wanasema wao wanaishangilia damu damu CCM (kwasababu ya ulaji) ila hawana mpango wa kupiga kura wako pale kiulaji tu!!!! Ndio ushawishi wa FL
 
Natamani nicheke kwani huo ushawishi mkubwa wa Salma anao anashindwa hata kumshawishi jamaa asiwe na vimada nje ya nyumba sembuse ataweza ataweza kushawishi watu wazima na akili zao? Niliwasikia akinamama fulani walioenda katika mkutano wake Kawe wanasema wao wanaishangilia damu damu CCM (kwasababu ya ulaji) ila hawana mpango wa kupiga kura wako pale kiulaji tu!!!! Ndio ushawishi wa FL
Unasound ka Santuri...
 
Sijui kama hii pointi imegusiwa, lakini kwani katiba haimruhusi mke wa raisi kumsapoti Mmewe kisiasa? To what extend does the law /constitution limits the first lady's involvement in political campaign?

Disclaimer: I do not support CCM, nor do I belong to any party. But if I was around during the independence struggle, I would have been a Mao Mao, a member of PAC (Pan Africanist Congress) , Or Malcom X!!
 
Back
Top Bottom