Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 40,333
- 72,796
Mkuu wetu alitembelea Muhimbili mara tu alipoapishwa na kuona kuambiwa kuna upungufu wa vitanda 200 naye alipoenda kukutana na Wabunge akafyeka fedha zilizochangwa na taasisi mbalimbali kwa sherehe ya bunge na kwa mbwembwe vikanunuliwa vitanda 270 na tukaambiwa kuwa sasa Muhimbili kulala chini ni historia.
Kukaja hekaheka bandarini kuhusu kontena za mizigo, mwanzo kwa mbwembwe vile vile tukaambiwa na mkulu ni mia tatu na kitu zimegunduliwa kuwa zimepotea na watu tuashika vichwa kwa hudhuni kuwa 380? Zote hizo? Lakini baada ya siku chache kumbe ni zaidi ya elfu kumi na moja hazijulikani zimepitaje. Na leo tena huko bandarini mafuta nayo kumbe hata mita hazifanyi kazi kwa awamu ya pili yote ya Kikwete na limejulikana hilo siku 100 za JPM.
Sasa nauliza jee kwa usanii huu hata hayo makusanyo ya TRA ya january tunayoambiwa ni Shilingi Trilioni 1.4 kweli kuna uhakika huo au nalo ni changa la macho? Maana kama kweli serikali imekusanya kiwango kikubwa zaidi ya makisio yake sii hata ingeonekana ina fedha na kuweza kulipa madeni yake yote ya wakandarasi, waalimu na hata wakulima walio kopwa?
Au ni cooked figure ili kumrizisha mzee tuu na hakuna kitu? Hili lichunguzwe, maana mficha nanihii huwa hazai.