Kama Mugabe aliweza kunyang’anywa Degree ya heshima, sitashangaa hilo likitokea hapa nchini!

.... jamaa aliweweseka sana na ni mwoga sana kupambana na challenge. Kama mtakumbuka alipohutubia ...

JK kuweweseka ni kawaida yake.. .. aliweweseka na kuanguka bila hata kuguswa akiutubia jangwani, na kuna wakati alidundwa, akaweweseka na kuanguka chali akihutubia kirumba mwanza. Inatia huruma
 
Acha kutetea ujinga kwani unawakatisha tamaa watu kufanya tafiti za kutumia akili eti kuongea tu umeshapata udoctor?huo ni upuuzi mtu akae darasani miaka minne na zaidi kusomea we usimame jukwaani dakika tano uwe dr.?shame kama ni hivyo hata mi ni dr kwani nasuluhisha mambo yangu ya ndani na familia yangu mi mwenyewe.
 
Nilipata nafasi kulizungumzia jambo hili kipindi kilichopita ingawa siyo vibaya kurudia tena kwa faida ya watu wengi zaidi. Utambulisho huu wa mtu kuitwa Daktari ama Doctor kwa Kiingereza huwa unakuja kwa namna tatu. Namna ya kwanza ni kuwa mtu unaweza kuitwa Daktari ikiwa umesoma Chuo Kikuu na kufuzu Fani ya utabibu wa magonjwa ya Binadamu ama wanyama wewe unastahiki kuitwa Daktari kama alivyo Dakt Ali Mohamed Shein, namna ya pili mtu anaweza kuitwa Daktari ikiwa amesoma Shahada ya kwanza na ya pili ya Uzamili na ya tatu ya Uzamivu katika fani yoyote ile iwe Sheria kama alivyo Dakt Harrison Mwakyembe ama Dakt Festus Limbu mwenye Shahada ya Uzamivu katika mambo ya Uchumi ama Dakt John Pombe Magufuli alie na Shahada ya Uzamivu katika fani ya Kemia na namna ya tatu mtu anaweza kuitwa Daktari ikiwa Chuo Kikuu chochote ulimwenguni kimeamua kuutambua mchango wa muhusika katika kuisaidia jamii na kumtunuku Shahada ya Udaktari wa Heshima na ndiyo kwa namna hii ya tatu tunampata Dakt Jakaya Mrisho Kikwete mimi sioni tatizo lolote la msingi kwa nini Dakt J M Kikwete awe na hofu ya kutumia utambulisho huu ambao umeonwa na Chuo Kikuu kilichomtunuku Shahada hiyo ya Udaktari. Tujitahidi kuwa waelewa maana kila kukicha ni kumzodoa Mheshimiwa Raisi kwa mambo ambayo yako wazi aachwe atumie utambulisho wa Daktari kwa kuwa kesha tunikiwa watu tunalalama kwa vitu ambavyo hatuvijui ila kwa kuwa fulani kasema basi nasie tufuate mkumbo tu hapana! Mimi nasema ni haki kwa Daktari Kikwete kutumia utambulisho huo tuache fitna ambazo hazitusaidii tunachekwa na wanaofahamu!
Hatukatai jk kuitwa dr, lakini je anasitahili kuitwa dr?
 
Back
Top Bottom