Kama mpenzi amekukimbia, kinachokuuma ni kitu gani…………..! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kama mpenzi amekukimbia, kinachokuuma ni kitu gani…………..!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Nov 2, 2011.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Nov 2, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Tunapopatwa au kuingia kwenye hali ambapo tunajikuta tumeshindwa kufanikiwa au kupata matokeo tuliyoyataka, kuna njia kadhaa katika kuitazama hali hiyo ili isituumize.

  Kwanza inabidi tujiulize kama hakuna namna nyingine ya kulitazama jambo au hali inayotukabili. Je, kama mpenzi ametukimbia ni lazima tutazame jambo hilo kama tatizo au tunaweza kulitazama kama mabadiliko ya kimaisha yasiyoepukika?

  Pili inabidi tujiulize kama hali hiyo iliyotokea haina faida yoyote kwetu. Ni lazima tutafute aidha katika hali hizi zenye kutuumiza au kutuvunjwa nguvu. Hakuna jambo au tukio lenye upande mmoja tu maishani. Kama wapenzi wametukimbia hatuwezi kuona kuwa huenda wametuepushia matatizo makubwa zaidi, wametupatia nafasi ya kutafakari upya maisha yetu na wametuonyesha kwamba tunahitaji kujikagua upya?Tukitafuta upande mzuri kwenye tukio tunaloliona baya ni lazima tutaupata na huo ndiyo wa kuupa nuvu.

  Tatu ni lazima tujifunze kujiuliza kama tukio hilo halijatupatia elimu fulani maishani. Kila tunapopatwa na tatizo au hali yenye kuvunjwa moyo ni lazima tutafute tulichojifunza. Kwa kutafuta tulichojifunza na kukipata, tunakuwa tumepunguza pia uzito wa tatizo tunajihisi kwamba angalau tumejifunza jambo au kitu fulani.

  Nne ni vizuri tukajiuliza, ingekuwaje, kama ni rafiki yangu ndiye aliyeingia kwenye tatizo au hali kama hii, ningemshauri nini? Kwa kutafakari jinsi ambavyo ungemshauri, unaweza kujikuta ukiwa umepata ufumbuzi au ahuweni fulani.

  Kwa hiyo ni uchaguzi wa mtu mwenyewe kwani ni suala la kuamua tu. Kama tutaamua kuyatazama matatizo yanayotupitia kwa jicho la kujipa moyo, kwa kuwaza vizuri na kuamini kwamba kila ndani a anguko fulani kuna faida tusiyoiona, tutafika mbali. Tukifanya kinyume chake, tutaanguka na hatutaweza kusimama tena.
   
 2. Chauro

  Chauro JF-Expert Member

  #2
  Nov 2, 2011
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 2,969
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  inauma bana hata ufanyaje!
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Nov 2, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Shida ni kwamba ukiweka kwenye mzani faida za upande wa pili wa kukimbiwa, na kukimbiwa kwenyewe mzani unalalia kwenye kukimbiwa!

  [​IMG]
   
 4. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #4
  Nov 2, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Chauro itauma kama utaangalia upande mmoja wa tukio hilo la kukimbiwa....................... mara nyingi sisi huwa tunaangalia upande mbaya wa tukio ambapo hutuumiza`sana...............
   
 5. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #5
  Nov 2, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  hata hivyo unayo nafasi ya kupuuza kule mzani ulipolalia..................
   
 6. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #6
  Nov 3, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Uyasemayo ni kweli kabisa; kuna haja ya kujifunza kuwa na mitazamo yote miwili tunapoyakabili matatizo; yaaani mtazamo hasi kwamba ni kweli tumepta hasara kwa kukimbiwa na pia mtazamo chanya kuwa tumeepukana na tatizo ama hta janga kubwa huko mbeleni; lakini pia tumejifunza kuwa hatukuwa makini kwenye uchaguzi wetu wa wenzi na wakati mwinine pia sisi wenyewe tumechangia kukimbiwa huko kwa kiasi gani..............nakushukuru kwa tafakuri
   
 7. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #7
  Nov 3, 2011
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Ni kweli kbs baba,sema tu tatizo ni kwamba maumivu huwa yanachukua nafasi kwan unakuwa hujajiandaa kukimbiwa na unakuwa na mipango mingi na mtu kumbe mwenzio anakung'ong'a na kukulia timing tu ila unapokubaliana na situation na kujipanga upya ndio unakuja kuziona zile faida za kukimbiwa baada ya kuumia sn na hata unakundua ulijitesa bure na hata some time unataman hata umtafute na kumshukuru kwa kukukimbia kwake.
  Hapa kwa vile maumivu hayakwepeki inabidi tu tujifunze kupokea matukio no matter ni mazuri au mabaya na kumshukuru tu mungu linapotokea km hili na kuamini ana mpango mwingine mzuri zaidi juu ya maisha yako.
   
 8. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #8
  Nov 3, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Kabla hujakimbiwa, kimbia wewe
   
 9. M

  Malova JF-Expert Member

  #9
  Nov 3, 2011
  Joined: Apr 21, 2011
  Messages: 777
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  maumivu yanategemea na mtu. mimi itaniuma kwasababu itanibidi nianze kumzoea mtu mwingine upya wa kuwa nae hata nitakuwa ninaongeza marafiki wengu zaidi
   
 10. F

  FUSO JF-Expert Member

  #10
  Nov 3, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,889
  Likes Received: 2,346
  Trophy Points: 280
  lazima niumie hasa nikikumbuka mambo yote nilimfanyia naye - jamaa mwingine atakuwa anafaidi pia.. lazima roho iumie
   
 11. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #11
  Nov 3, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  kweli kabisa hapo kuna ujanja wa kuwai
   
 12. lolyz

  lolyz JF-Expert Member

  #12
  Nov 3, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 333
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Nimefurahi kukuona tena Kaka Mtambuzi hope umepona ..na uko fit..
   
 13. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #13
  Nov 3, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 722
  Trophy Points: 280
  mtambuzi big up.....kumbe tayari unawea kunyoonsha mwandiko vizuri namna hii!!!
   
 14. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #14
  Nov 3, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  mwanangu umebadilisha avatar yako bila hata kunishirikisha?..............lol

  halafu nimependa hili neno lako, haiyumkini mada hii ilitokana na huu ujumbe wako.....................


  "Don't worry about the people in your past,There 's a reason they didn't make it to your future"

   
 15. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #15
  Nov 3, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  fuso, hata kama itakuuma, lakini, je, waweza kuubadili ukweli huo?
   
 16. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #16
  Nov 3, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,682
  Trophy Points: 280
  Unajua unapopatwa na jambo ambalo jamii imekufundisha kuwa ni baya haya ya kujilaani huja japokuwa mara nyingi jamii imekua na uongo mwingi,tatizo la pili ni kuwa mara nyingi tunapopata changamoto hizi huwa hatuzikubali,matokeo yake kuchanganyikiwa huja na fahamu ukishachanganyikiwa kufikiri wa njia chanya hutoweka pia hapo ndipo kujinyonga au kukata tamaa huja!
   
 17. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #17
  Nov 3, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  Shida kubwa tumeegemea kwenye mapenzi pekee! Na hata huko kwenye maenzi hatuangalii scenario nyingine. Hebu fikiria hili la huko huko kwenye mapenzi. Kwamba Mwanaume/mwanamke kakukimbia kisa umekataa kushiriki nae ngono zembe. Siku mbili baadae unasikia alipata mchumba na walioenda kupima, ili waoane, amegundulika kuwa na ngwengwe. Nadhani maumivu ya kuachwa hapa ni matamu zaidi kuliko yale ambayo ungeyapata kwa kukubaliana naye.

  Mtambuzi uko very right!
   
 18. F

  Fmewa JF-Expert Member

  #18
  Nov 3, 2011
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 294
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  nimekuelewa japokuwa ni ngumu kufanya hivo ila ni lazima kujitahidi kutazama mambo yanayotutokea ktk macho mawili.
  Thanks
   
 19. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #19
  Nov 3, 2011
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Haaaa haaa,sijabadilisha baba,ni ile ile tu ila nimedadilisha mavazi na pozi lol!
  Wala hujakosea umepita humo humo!
   
 20. F

  Fmewa JF-Expert Member

  #20
  Nov 3, 2011
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 294
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Ni kweli mie ilinitokea my ex gf alinikimbia baada ya kuona nimeyumba kiuchumi akasepa. alimpata jamaa mwingine ambae alikua analelewa na jimama lenye fulani la mitaa ya bandari ya pweza (oysterbay) lakini cku moja lile jimama liliwafumania na likaamuwa kuwaweka lupango kwa muda km wa siku tatu. baada ya hapo jamaa akamkataa binti na lile jimama nalo likaamua kuachana na yule jamaa. kwa hiyo yule ex akabaki iddle. ni kweli iliniuma sana baada ya yeye kunikimbia ila sikuwa na jambo la kufanya ilibidi nivumilie japo nilijifunza kuwa alikuwa na mimi kwa maslahi zaidi. nakubaliana katika hilo
   
Loading...