Kama Mnataka Rais kutoka Zanzibar, Tupeni Dr Salim | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kama Mnataka Rais kutoka Zanzibar, Tupeni Dr Salim

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ibange, Feb 5, 2012.

 1. i

  ibange JF-Expert Member

  #1
  Feb 5, 2012
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 1,545
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kuna watu wanajaribu kupiga debe kwamba rais ajae atoke Znz. Ni kweli ili kudumisha muungano rais anaweza kutoka Znz lakini isiwe ni issue ya kisiasa. Ukweli katika wazanzibar wa sasa, hakuna mwenye uzoefu, hekima na maono kama Dr Salim. Wazanzibar kwa chuki zao hawamuungi mkono lakini hii ni lulu au jiwe walilolikataa waashi. Otherwise, bado chadema waweza ku compromise na CUF akapatikana mgombea mzuri kutoka znz halafu mwenza akatoka bara. Pamoja na kwamba ni kama ndoto, bado naamini CUF na Chadema wanaweza kufanya kazi pamoja na kushirikiana katika uchaguzi ujao
   
 2. B

  BMT JF-Expert Member

  #2
  Feb 5, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 570
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 45
  safi sana,namkubali sana hvyu mzee
   
 3. chuki

  chuki JF-Expert Member

  #3
  Feb 5, 2012
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,691
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  vp ile kashfa imesahaulika?
   
 4. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #4
  Feb 5, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Itawachukua waZanzibar zaidi ya miaka 50 kumpata mwanasiasa mwenye uwezo wa Dr Salim A Salim.
   
 5. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #5
  Feb 5, 2012
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,953
  Likes Received: 1,509
  Trophy Points: 280
  Hilo nalo neno SAS arudi,asije akwa Wade
   
 6. Kilasara

  Kilasara JF-Expert Member

  #6
  Feb 5, 2012
  Joined: Dec 21, 2008
  Messages: 578
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Uwezekano wa Tanzania kuwa na utaratibu wa Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar kupeana zamu za kutoa Rais, ulitoweka wakati Katiba iliporekebeshwa na kuwa na vyama vingi vya siasa mwaka 1992.

  Hata hivyo utaratibu wa sasa ambao unahakikisha kwamba, Zanzibar wanakuwa na Rais au Makamu wa Rais kila wakati ni upendeleo tosha kwa Wazanzibari. Ikumbukwe kwamba idadi ya Wazanzibari ni chini ya asilimia 5 ya population ya Tanzania; na wengi wetu tunatetea demokrasia ya kweli tungetaka Tanzania Bara ipate ma-Rais hata zaidi ya kumi kabla Zanzibar kupata zamu ya kutoa Rais.

  Licha ya kwamba Dr Salum ana sifa za kuwa mgombea, anaweza tu kuchaguliwa Rais kama vyama vyote vya siasa vitakubaliana kumteua. Uwezekano huo haupo; na CCM watakuwa wanajidanganya kudhani wataweza kuendelea kuchakachua kura ili mteule wao wa 2015 achaguliwe na Watanzania.

   
 7. h

  hargeisa JF-Expert Member

  #7
  Oct 4, 2012
  Joined: Jun 19, 2011
  Messages: 551
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  si mtasema muarabu.labda KAMBARAGE angekua hai.but huyu mzee ni mzalendo kweli
   
 8. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #8
  Oct 4, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  walomuita muarabu hawakukosea kwani walikuwa wote katika siasa zilizomuibua Ghaddafi na zilizoifanya africa ikiwepo tz kuvunja mahusiano na Israeli kwa upendeleo wa wapiga mabomu wa kipalestina.Ndio maana naye alishindwa jitetea.Na hiyo pia ndio ilimnyika kura UN.

  Kwa ujumla ni mdini na mbaguzi wa rangi akifichwa na ujamaa.

  Mkiendekeza story za vijiwe vya wavaa vinjiwa mtapata watu wenye busara wazee wa busara.Akina kinana,diria, salimu, dhaifu, karamagi,kigoda,Prf. kigoma malima, kagasheki, akina idrissa Rashid,Kova , manumba, shimbo Na wengine wengi waliotafuna nchi kwa kwenda mbele ila kwa walio wao wanaonekana kuwa wokozi wa nchi.

  Weka Lissu ujinga wa kufagilina kijinga ukatwe mizizi.Wajinga wote wanaitwa raia wanatetemeka wanasema sasa Lissu kaingia choo cha Kike ghafla unaona mzee wa busara ananywea huku akiomba ulinzi kwa speaker au kwa polisi.Hizi network za watu wa imani moja wanaoweza ongea mambo ya nchi kwenye hitma ni mbaya kwa afya ya taifa.Ndio huko uamsho wanapata nguvu kwani habari wanapata hukohuko.
   
Loading...