Kama mnaipenda bandari ya Bagamoyo ni bora tungejenga kwa hela zetu tunazoingiza bandari ya Dar es Salaam

Ni ushauri tu,
Sipendi ujuaji sana wa kusoma kwenye makaratasi ila huwa napenda kuchakachua ubongo wangu,

Kama kweli mnaipenda bandari ya bagamoyo ni bora tungejenga kwa hela zetu tunazoingiza bandari ya Dar es Salaam.
Nasikia Mwamba wa Bagamoyo ni mgumu sana hivyo hii Bandari ijengwe Mtwara na Reli ijengwe toka Mtwara kuunga na za kwenda Bara
 
Ni ushauri tu,
Sipendi ujuaji sana wa kusoma kwenye makaratasi ila huwa napenda kuchakachua ubongo wangu,

Kama kweli mnaipenda bandari ya bagamoyo ni bora tungejenga kwa hela zetu tunazoingiza bandari ya Dar es Salaam.

China kumejaa mkuu
 
Pesa za kujenga hatuna, kama zingekuwepo tungekwisha jenga ndani ya miaka 60 tokea tupate uhuru wa Tanganyika.

Kwa kifupi tuwape wachina
 
Hivi wanaosaini mkataba huwa tunajua Mali zao zisizohamishika? Au basi tuwatambue ndugu zao na Mali zao ili likitokea la kutokea tujue tunashika wapi.
 
Ni ushauri tu,
Sipendi ujuaji sana wa kusoma kwenye makaratasi ila huwa napenda kuchakachua ubongo wangu,

Kama kweli mnaipenda bandari ya bagamoyo ni bora tungejenga kwa hela zetu tunazoingiza bandari ya Dar es Salaam.
Ni ni kweli kabisa kwamba huwa "unachakachua ubongo wako", maana inaonyesha wazi.

Na huko kwingine inakotumika hiyo hela tufanyeje?

Lakini nakubaliana na wewe juu ya wazo la kujenga wenyewe, hata kama ni kwa mkopo.

Unauliza "kama tunaipenda"? Hili ni swali la kitoto sana. Utashindwaje kupenda bandari ya Bagamoyo?
 
Ni ushauri tu,
Sipendi ujuaji sana wa kusoma kwenye makaratasi ila huwa napenda kuchakachua ubongo wangu,

Kama kweli mnaipenda bandari ya bagamoyo ni bora tungejenga kwa hela zetu tunazoingiza bandari ya Dar es Salaam.
tujenge kwa hela zetu, una hela hizo? wacha wachina wajenge, sisi tutafaidika kwenye usafirishaji mizigo kwenda nchi za nje/landlocked na kwengine, na ajira. tena wajenge haraka sana ili bwagamoyo liwe jiji jingine east africa, na iwe mji wa viwanda kama huko china.
 
Yule Mzee alikuwa akiwadanya watu miradi tunajenga kwa fedha zetu, kumbe alikuwa anakopa kupitiliza
 
Ni ushauri tu,
Sipendi ujuaji sana wa kusoma kwenye makaratasi ila huwa napenda kuchakachua ubongo wangu,

Kama kweli mnaipenda bandari ya bagamoyo ni bora tungejenga kwa hela zetu tunazoingiza bandari ya Dar es Salaam.
Hatuna uwezo huo mkuu. Unajua gharama yake na mbwembwe zake? Tanzania tuna upugufu wa visionary leaders

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Huo ujenzi wa bandari hauna hasara zozote zaidi ya faida. Utaongeza biashara na ajira nyingi.

Kwa jinsi nilivyoelewa mimi hiyo bandari haijengwi kwa pesa ya mkopo. Wataitumia hela yao kujenga na wataitumia bandari kufanya biashara kwa muda fulani ili waludishe pesa yao na baada ya hapo wanatuachia bandari Yetu wao wanasepa. Kwa makubaliano hayo mimi sioni kama kuna tatizo
 
Mkuu kwa akili yako kubwa ya kuzaliwa unamaanisha wachina wana mahaba sana na watanzania ehhh. There is No free lunch in life. Mambo ya Bandari pia ugusa usalama wa Nchi. Kama kuna faida hivyo Kwanini wasitoe tu hela ya mkopo na Tz ikalipa kwa muda huo wa wao kufanya hiyo biashara. Tz ifanye. Nini kipo pale mpaka wachina Waje kwa mahaba hivyo. Je Kuna Gas. Kuna madini nk.
 
Huo ujenzi wa bandari hauna hasara zozote zaidi ya faida. Utaongeza biashara na ajira nyingi.

Kwa jinsi nilivyoelewa mimi hiyo bandari haijengwi kwa pesa ya mkopo. Wataitumia hela yao kujenga na wataitumia bandari kufanya biashara kwa muda fulani ili waludishe pesa yao na baada ya hapo wanatuachia bandari Yetu wao wanasepa. Kwa makubaliano hayo mimi sioni kama kuna tatizo
Mnauhakika mpo vizuri kwenye uhasibu, mtaweza kuwakagua kwamba tayari wamerudisha hizo fedha au la. Wakikataa kwamba bado hawajarudisha mtafanyaje??
Challenge ipo kwenye kuwakagua na sidhani kama wataruhusu kukaguliwa
 
Huo ujenzi wa bandari hauna hasara zozote zaidi ya faida. Utaongeza biashara na ajira nyingi.

Kwa jinsi nilivyoelewa mimi hiyo bandari haijengwi kwa pesa ya mkopo. Wataitumia hela yao kujenga na wataitumia bandari kufanya biashara kwa muda fulani ili waludishe pesa yao na baada ya hapo wanatuachia bandari Yetu wao wanasepa. Kwa makubaliano hayo mimi sioni kama kuna tatizo
Hahaàaaa Yale Yale ya kigamboni, tutakuwa watumwa ndani ya nchi yetu, maana watamiliki kila kitu, Serikali haitagusa ardhi ya bandari Hadi jamaa watakapo SEMA tumeshiba, kuanzia walinzi, watoza ushuru, mawasiliano n.k vyote vitakuwa chini ya wachina
 
Siku hizi mtu akiwa na mawazo tofauti anaonekana ana "chuki binafsi" mambo ya msingi kwenye mikataba lazima yajadiliwe, sio kulishana notes za darasani huku pakutoa hayo mapesa hapajulikani na jinsi ya kuyarudisha haijulikani, tusilazimishane kugeuzwa kichwa cha mwendawazimu.

Kuja na figure tu za gharama za mradi ni utoto, na kwanini pasitafutwe miradi mingine yenye gharama nafuu zaidi? au kuboresha iliyopo tuongeze uzalishaji badala ya kukomalia ya gharama kubwa ambayo hatuna uwezo nayo?

Wakati mwingine nahisi hata hao mabeberu wanatushangaa, kanchi masikini chenye viongozi walafi wanaokurupuka na miradi ya gharama kubwa wasiyo na uwezo nayo hata wa kuchangia 50%

Bajeti yetu ya ndani tu shida mpaka beberu atie mkono..!!!
 
Acha wajenge tukishindwa kulipa tutawapa wachina Chato airport wakamate kama Dhamana
 
Back
Top Bottom