KAMA MMBWAI NA IWE MMBWAI , Wanasimba wenzangu , Ni nani hasa aliyesababisha Amis Tambwe aachwe ?

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
125,703
239,277
Tukimjua , huyo ndiye adui mkubwa wa timu yetu .

Haiwezekani na wala haitawezekana kuvumilia jambo hili .

Kumuacha mchezaji kama huyu na kuchukua galasa kama Kiongera na wengine wa aina hiyo haikubaliki na itafsiriwe kama hujuma .

Hakuna msamaha kwa mtu kama huyu , au ndani ya simba kumepandikizwa wana Yanga ?

Uchunguzi uanze leo .
 
sababu zilizotumiwa na simba kumwacha tambwe ndo hizo hizo zitatumiwa na yanga pindi watakapomwacha huyo huyo tambwe. hahaha hilo ndo soka la bongo full figisufigisu.
 
Tambwe alitemwa na Hans Pope akasingizia kocha Patrick Phiri amesema ha-fit kwenye mfumo wake.Akamleta Serunkuma akachemsha Kibaya zaidi tangu Tambwe atue Yanga anafunga magoli kila mechi
Kweli kabisa mkuu Hans pope na kundi lake wapo kwa manufaa yao tu sio mpira yeye ndo chanzo cha kuachwa kwa Amis Tambwe
 
Habari ya kubebwa yanga aliisha mwishoni mwa ligi.Leo tunazungumzia kujenga timu yetu upya.Hivyo hapa hatuangalii habari za yanga.Tunataka mapandikizi yenu yaondoke .
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom