HIZI NI SERA ZA CCM, ARUMERU AU KUNADI MGOMBEA?
Benjamin William Mkapa, Rais Mstaafu wa Tanzania, akaacha kando mambo ya kampeni na kukimbia kimawazo na maneno hadi katika familia ya Mwasisi wa Taifa hili, Hayati Mwalimu Julius K. Nyerere na kusema, Vicent Nyerere, si mtoto wa Mwalimu Nyerere; huku akisisitiza yeye sio mwizi wa Ardhi.
Wassira: katika kampeni ameenda kusema Dr. Slaa anatafutwa kwa kuliibia Kanisa tangu mwaka 1990. Yeye pia hakutaja Serza za Chama.
Jana Lusinde; Mbunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ananukuliwa na vyombo vya habari Jumatatu hii akiwataka wananchi wamchague Sioi kwa sababu ili eti wamfute machozi kwa kuwa alifiwa na baba yake; Jeremia Sumari aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo! Lusinde hakuona lingine jema la kuwahamisha wananchi hao wamchague Sioi Sumari ili pengine ashirikiane nao kukabiliana na changamoro za maendeleo ila yeye anawaambia wamchague ili kumfuta machozi kutokana na kifo cha baba yake! Huo ndio msisitizo wake badala ya kujikita kuangalia changamoto za umaskini, elimu duni, huduma duni za maji na mengine, Lusinde anataka Sumari apewe ubunge kama rambirambi!Hivi hilo ndilo tatizo la watu wa Arumeru Mashariki? Nani alimwambia Mbunge Lusinde kuwa ubunge unatolewa kama salamu za rambirambi? Hiki Chama kumbe kimeishiwa hivi kwanini tunaendelea kuwaamini mbona tutaumia