Subira the princess
JF-Expert Member
- Mar 3, 2018
- 2,462
- 2,633
Mkuu tangu lini mwizi amkamate mwizi mwenzie? TafakariWana Jf,
Shahidi wa kwanza ambaye alishuhudia wizi mkubwa wa EPA yupi na ametaja kusikitishwa kwake na kitendo hiki. Ili asemehewe inabidi waliohusika na wizi huu wakamatwe kesi ianze upya. Shahidi wa pili no Dr. Balozii Slaa ambaye aliwatuhumu watu kadhaa bunge likawafanyia kazi, pia list of shame nayo ihusishwe ili wote waliochezea Mali za umma wazijejeshe au wafungwe
Kwa ufupi mzee wetu anapenda kuomba msamaa kwa yaliyotokea, lakini akumbuke kuwa ukienda kutubu kanisani unaambiwa urudishe ulichoiba na kuomba samahani. Kama ulizini basi unapigwa faini pale pale, kama uliua unapigwa faini pale pale, lakini matendo ya kuchukua kisicho chako lazima ukirudishe.
BWM anaweza kuja kuwa mtakatifu wa baadaye kama ameanza taratibu za kutubu, lakini pia matusi yake pia ayatubu maana kuita wapinzani ni kokoto, ni marofa haya hayavumiliki maana kuwaita watu wamungu majina mabaya hayaleti utukufu. Japokuwa kabla ya upinzani yeye alipewa support kubwa kuleta maendeleo ya kila sehemu.
Roho 22 zilizopotea pesa za manunuzi ya kitabu hiki wapelekewe wazazi, au familia zilizopotelewa na ndugu zao. Mwisho namtakia kutubu kwema na namwomba asitumike tena kwenye siasa, aache vyuma viumane vyenyewe kwani Muda wa kukutana na mhusika mkuu aliyetuumba unakaribia.