Kama Mkapa amekiri Majambazi ya EPA yapo, Rais wetu Magufuli aanze na hawa hata wajukuu wasitumie pesa hizi

Subira the princess

JF-Expert Member
Mar 3, 2018
1,966
2,000
Wana Jf,

Shahidi wa kwanza ambaye alishuhudia wizi mkubwa wa EPA yupi na ametaja kusikitishwa kwake na kitendo hiki. Ili asemehewe inabidi waliohusika na wizi huu wakamatwe kesi ianze upya. Shahidi wa pili no Dr. Balozii Slaa ambaye aliwatuhumu watu kadhaa bunge likawafanyia kazi, pia list of shame nayo ihusishwe ili wote waliochezea Mali za umma wazijejeshe au wafungwe

Kwa ufupi mzee wetu anapenda kuomba msamaa kwa yaliyotokea, lakini akumbuke kuwa ukienda kutubu kanisani unaambiwa urudishe ulichoiba na kuomba samahani. Kama ulizini basi unapigwa faini pale pale, kama uliua unapigwa faini pale pale, lakini matendo ya kuchukua kisicho chako lazima ukirudishe.

BWM anaweza kuja kuwa mtakatifu wa baadaye kama ameanza taratibu za kutubu, lakini pia matusi yake pia ayatubu maana kuita wapinzani ni kokoto, ni marofa haya hayavumiliki maana kuwaita watu wamungu majina mabaya hayaleti utukufu. Japokuwa kabla ya upinzani yeye alipewa support kubwa kuleta maendeleo ya kila sehemu.

Roho 22 zilizopotea pesa za manunuzi ya kitabu hiki wapelekewe wazazi, au familia zilizopotelewa na ndugu zao. Mwisho namtakia kutubu kwema na namwomba asitumike tena kwenye siasa, aache vyuma viumane vyenyewe kwani Muda wa kukutana na mhusika mkuu aliyetuumba unakaribia.
Mkuu tangu lini mwizi amkamate mwizi mwenzie? Tafakari
 
mhanila1

JF-Expert Member
Dec 15, 2017
1,030
2,000
Yaani viongozi wetu wanashiriki kwenye wizi wa fedha za umma wakiwa wamekula kiapo cha kulitumikia taifa halafu wana gut ya kuandika hadi vitabu kutueleza jinzi walivyoibia nchi wakiwa madarakani na huku wakituita malofa tukitaka kuhoji hayo maovi yao. Mimi ndiye najisikia aibu kwa haya yaliyotenhenezewa kitabu.
 
Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
14,954
2,000
Waziri Mkubwa na Mzito aliemnyeshwa Sumu Kipenzi cha Wanyonge Jana hakupewa Mwaliko wakati alikuwa Mtu muhimu kwenye utawala wa Mzee Mkapa wa miaka yote 10 na aligombea Urais 2005 but hakufurukuta

Huyo huyo Waziri alimkosa kosa Mkwere 2003 kule Znz kwenye Nec
Ni yule anayetoka jimbo moja na Mama Mary Nagu?. Basi ni mtu hatari sana.
 
Titicomb

JF-Expert Member
Jan 27, 2012
9,529
2,000
soma hapa

Mkuu umewahi kuchukua muda wako na kutaka kujiridhisha Nyerere alisema Ujamaa ni mbaya na ulivurunda au kuharibu uchumi?

Umetumia makala ya Mwandishi wa Mwananchi ndugu Elias Msuya ambayo hata yeye nadiriki kusema hakuandika kwa weledi kwa kuweka nukuu, na kuonyesha rejea ya chanzo chanzo cha hizo nukuu ili kuthibitisha yale aliyo yaongea.

Nyerere aliandika TUJISAHIHISHE mapema sana mwanzoni mwa uongozi wake mwaka 1962 hata kabla ya Azimio la Arusha lililokuja kuimarisha sera za ujamaa zinazo tuhumiwa kuuwa au kuvuruga uchumi.
Pili uchumi wa Tanzania uliingia ktk misukosuko mikubwa sana na kudorora miaka mingi takribani zaidi ya miongo miwili(miaka 20) baada ya andiko la tujisahihishe. Na sio baada ya kuyumba uchumi, hivyo sio sahihi kutumia maelezo yaliyo ktk kitabu hicho kuhitimisha Nyerere alikili makosa ya Ujamaa ktk andiko hilo.

Eliasi Msuya ameonekana kuweka maoni yake binafsi ambayo hajayatetea kiataalamu kwa utafiti wenye kuweka vielelezo na viambatanishi.

Inavyoonekana huyo Ndugu Eliasi Msuya hakusoma au alisoma hakuelewa kuhusu andiko la Nyerere la TUJISAHIHISHE, na vilevile wewe umemnukuu vibaya Eliasi Msuya na kuweka hitimisho kwa mambo ambayo hajasema hivyo.

Tuna shida kubwa sana ktk uandishi wetu wa habari hapa Tanzania, kuna wakati tunaweka maoni binafsi na kuhukumu bila kufanya uchunguzi na kuweka mjadala ujadiliwe huku tukiwa na vielelezo sahihi.

Kwa kukusaidia wewe na wengine wengi nakuwekea kiunganisho au 'link' ya kupata andiko husika la NYerere ili usome mwenyewe kisha uje utoe maoni na hitimisho sahihi.
TUJISAHIHISHE-JK_Nyerere_May-1962
TUJISAHIHISHE-Kama ilivyo chapishwa katika Jamhuri Media
 
Prince Kunta

JF-Expert Member
Mar 27, 2014
18,681
2,000
Kinga ya urasi iondolewe, haiwezekani watu walipigia kelele suala la EPA kumbe wezi wanajulikana na walikuwa na baraka zote toka kwa raisi ambae chama chake CCM ni moja ya majizi yaliyofaidika
 
Sumve 2015

JF-Expert Member
Jun 16, 2013
3,806
2,000
Umeandika nini, hao kwani amewaua yeye, izo ela za kitabu hujasikia zinaenda wapi?
Hawa wachekeshaji vituko sana, kitabu chenyewe hajakisoma afu anaandika upupu, kuhusu mauaji mwenyewe yalimuumiza na yanamuumiza the way analaumiwa wakati wala hakuwepo, hicho ndo alichokisema.
 
Bungua

JF-Expert Member
Jul 28, 2018
925
1,000
Uhusiano ni Mkapa ndio aliruhusu wizi wa EPA kwa ahadi kwamba chama kitanufaika pesa za kampeni za uchaguzi mkuu uliyomuingiza Kikwete madarakani.

Mkapa kwenye kitabu chake ameandika kwamba anahisi alitumika na kusalitiwa. ( Na Daud Balali?)
miaka yote hii bado anahisi? wapelelezi wetu mahiri wako wapi? au napo kuna ule wimbo pendwa: upelelezi haujakamilika! hakuna sehemu kaongelea kifo cha huyo msaliti? au naye alizikwa baharini kama osama. ajabu mangwea anafia nje, maiti yake inaletwa na kuzikwa nyumbani kwao. balali anazikwa na maji! nchi ya vi-wonder.
 
wakurochi

JF-Expert Member
Dec 4, 2017
2,499
2,000
Ameona kumbe kwenye ft 6 ataingia yeye kama yeye na kuna utawala mwingine huko anahitaji kuweka mambo sawa kabla hajafik huko
 
mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
12,984
2,000
Kinga ya urasi iondolewe, haiwezekani watu walipigia kelele suala la EPA kumbe wezi wanajulikana na walikuwa na baraka zote toka kwa raisi ambae chama chake CCM ni moja ya majizi yaliyofaidika
Hili ndilo litakuwa suruhisho, waliohusika wafilisiwe kwani nao hawataona noma kwa kuwa mali haikuwa yao ni ya kiwizi wizi
 
AggerFirminho

JF-Expert Member
Sep 17, 2019
1,145
2,000
Msajili wa vyama kwa nini mpaka sasa hajakifuta hiko chama cha CCM maana rais wa amekiri wametumia hela kwa WIZI kwenye kampeni yao.
 
Matola

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
41,964
2,000
Hawa wachekeshaji vituko sana, kitabu chenyewe hajakisoma afu anaandika upupu, kuhusu mauaji mwenyewe yalimuumiza na yanamuumiza the way analaumiwa wakati wala hakuwepo, hicho ndo alichokisema.
Una uelewa wowote kuhusu command in chief ni nini? Au umeamuwa tu kujambajamba?

Wale wanaohukumiwa kwenye mahakama za uhalifu wa kimataifa walishika bunduki kuuwa? Omar Bashir alishika bunduki kuuwa waandamanaji?

Puumbavuu kabisa.
 
mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
12,984
2,000
Hawa wachekeshaji vituko sana, kitabu chenyewe hajakisoma afu anaandika upupu, kuhusu mauaji mwenyewe yalimuumiza na yanamuumiza the way analaumiwa wakati wala hakuwepo, hicho ndo alichokisema.
Hakuna haja ya kukisoma wakati alitakiwa awe amejipeleka mwenyewe mahakamani baada ya kuandika, alafu aombe adhabu yeyote kutoka kwa akimu aliyejitolea kumhukumu. lakini kinga ndizo uwapaviburi, miaka yote alikana ANNBEN, KIWIRA, RAMDA Hotel, RADA ya Chenge, Ndege yake Ilimfunga Basil Mramba, Profesa Mahalu na Pesa za Ubalozi wa Ital hadi kaitwa kutoa ushahidi kumnusuru. dhambi nyingi tu hata akikiri lakini taifa liliumia san hasa alipouza TBL na Nyumba za serikali.
 
Pohamba

JF-Expert Member
Jun 2, 2015
24,095
2,000
TUNASUBIRI KITABU CHA KIKWETE, SIJUI ATASEMA NINI

Akiwa fair akaeleza kila kitu kuanzia mwanzo mpka mwisho kitavutia sana

Jk ana historia ya aina yake kwenye Siasa zetu na akiacha diplomasia akaweka kila kitu hewani kitakuwa gumzo sana
 
sweettablet

JF-Expert Member
Nov 16, 2014
7,589
2,000
Wana Jf,

Shahidi wa kwanza ambaye alishuhudia wizi mkubwa wa EPA yupi na ametaja kusikitishwa kwake na kitendo hiki. Ili asemehewe inabidi waliohusika na wizi huu wakamatwe kesi ianze upya. Shahidi wa pili no Dr. Balozii Slaa ambaye aliwatuhumu watu kadhaa bunge likawafanyia kazi, pia list of shame nayo ihusishwe ili wote waliochezea Mali za umma wazijejeshe au wafungwe

Kwa ufupi mzee wetu anapenda kuomba msamaa kwa yaliyotokea, lakini akumbuke kuwa ukienda kutubu kanisani unaambiwa urudishe ulichoiba na kuomba samahani. Kama ulizini basi unapigwa faini pale pale, kama uliua unapigwa faini pale pale, lakini matendo ya kuchukua kisicho chako lazima ukirudishe.

BWM anaweza kuja kuwa mtakatifu wa baadaye kama ameanza taratibu za kutubu, lakini pia matusi yake pia ayatubu maana kuita wapinzani ni kokoto, ni marofa haya hayavumiliki maana kuwaita watu wamungu majina mabaya hayaleti utukufu. Japokuwa kabla ya upinzani yeye alipewa support kubwa kuleta maendeleo ya kila sehemu.

Roho 22 zilizopotea pesa za manunuzi ya kitabu hiki wapelekewe wazazi, au familia zilizopotelewa na ndugu zao. Mwisho namtakia kutubu kwema na namwomba asitumike tena kwenye siasa, aache vyuma viumane vyenyewe kwani Muda wa kukutana na mhusika mkuu aliyetuumba unakaribia.
Badala ya kuulizia au kutueleza namna gani tunaweza kukipata hicho kitabu na kinauzwaje wewe unaandika pumba tu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom