Kama mitandao ya kijamii ingekuwa inapiga Kura basi CHADEMA ingekuwa madarakani vinginevyo acheni CCM itawale

RNA

JF-Expert Member
Mar 27, 2013
978
1,558
Habari JF,

Hivi kama watu, hasa vijana hampigi kura nini mnategemea? Katika Uchaguzi mkuu wa 2020 watanzania waliojiandikisha kupiga Kura ni milioni 29.8 , lakini ambao hawakupiga kura ni milioni 14.8.

Sasa kama watu milioni 14.8 hawakupiga kura, si ndio hawa wanaojaza mikutano ya CHADEMA na kusumbua Social media ?Maana kwa Uzoefu wangu Wana CCM mambo ya Chama na Uchaguzi wako serious nayo sana hivyo hilo ni kundi kubwa la Upinzani.

Watu hawajapiga kura ,wameshindwa Uchaguzi ,hawatambui matokeo mambo mengine kama Bunge inabidi yaendelea JPM angefanyaje ? Hivyo nyie wenyewe ndio chanzo cha kina Halima na wenzake .

CHADEMA na vyama vingine anzeni kuelimisha wananchi umuhimu wa kupira kura muache kulialia kwenye media , mimi siku ya Uchaguzi nlikutana na vijana kama watatu hawajapiga Kura wote sababu kwamba kura Yake 1 itabadilisha nini?

Hizi kelele za mitandaoni ni watu wachache sana.​
 
WALOLA VUNZYA

JF-Expert Member
Nov 20, 2020
1,836
1,424
Ule uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019 ulitoa dira nini kinaenda kufanyika 2020 hivyo usiwalaumu CHADEMA kwa upumbavu wa Magufuri na Mahera.
 
John7371

JF-Expert Member
Apr 29, 2018
2,778
6,000
Habari JF, Hivi kama watu ,hasa vijana hampigi kura nini mnategemea? Katika Uchaguzi mkuu wa 2020 watanzania waliojiandikisha kupiga Kura ni milioni 29.8 ,lakini ambao hawakupiga kura ni milioni 14.8...​
Mkuu unaonekana ulikimbia umande shule 🤣 🤣 🤣 umejuaje hiyo 50perc. ambayo haijapiga kura ni vijana? what if ni wazee?

What if ni vijana wa CCM,ACT.TADEA, au independents? hiyo conclusion ya kwamba ni vijana wa CDM huoni ni kama unafanya UGANGA au RAMLI sababu claim yako haina foundation yoyote 😁😁🤣🤣
 
WALOLA VUNZYA

JF-Expert Member
Nov 20, 2020
1,836
1,424
Ukija kujua kuwa chadema walipeleka majina then wakaja kuzinguana badae sijui utasema nn
Hizo ni mbinu za Spika Ndugai na yule jamaa wa Chato kwa vile tu Serikali ni yao,nakukumbusha wale waliotolewa usiku mahabusu na kusafirishwa usiku kwenda kuapishwa Bungeni kwa siri Dodoma ni Chadema walifanya mchongo huo?

Hata kama huipendi Chadema lakini tuwe wakweli mambo tunayoyaona kwa macho na tuepuke kutunga story za uongo zisizo na msingi,Tangu lini Mbowe na Ndugai au Magufuri wakawa marafiki?
 
Tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
48,805
84,002
Habari JF ,Hivi kama watu ,hasa vijana hampigi kura nini mnategemea ? Katika Uchaguzi mkuu wa 2020 watanzania waliojiandikisha kupiga Kura ni milioni 29.8 ,lakini ambao hawakupiga kura ni milioni 14.8...​

Kwa vyovyote ww utakuwa ni mzee, nyie ndio huwa mnakuja na logic za hivi. Sitaki nikupunguzie uzee wako, ila acha nikuamshe tu. Watanzania tunakaribia 60m, inawezekana vipi watu 29+m wajiandikishe kupiga kura? Kwa maneno marahisi kila watanzania wawili, mmoja alijiandikisha kupiga kura. Kwa akili ya kawaida inawezekana vipi Idadi ya watu wazima ikawa sawa na idadi ya watoto? Huo ni ujinga namba moja ukutoke.

Kwa taarifa yako na wapiga kura uchaguzi wa 2020 hawakufika 10m, baada ya watu kupuuza ule ukhanithi uitwao uchaguzi. Waliopika idadi ya wapiga kura, ndio waliopika idadi ya kura, na kuamua nani atangazwe mshindi. Inshort ule haukuwa uchaguzi, bali maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura.
 
RNA

JF-Expert Member
Mar 27, 2013
978
1,558
Kwa vyovyote ww utakuwa ni mzee, nyie ndio huwa mnakuja na logic za hivi. Sitaki nikupunguzie uzee wako, ila acha nikuamshe tu. Watanzania tunakaribia 60m...
Kumbe umegundua watu mnapuuza halafu mnakuja mnalialia huku
 
samurai

JF-Expert Member
Oct 16, 2010
11,454
23,780
Kwa vyovyote ww utakuwa ni mzee, nyie ndio huwa mnakuja na logic za hivi. Sitaki nikupunguzie uzee wako, ila acha nikuamshe tu. Watanzania tunakaribia 60m...
Hahahahaha "Ukhanithi" Tindo nilijua hii mada lazima ufike tu...

Mtazamo wangu ni tofauti kidogo....
KWA USALAMA WA NCHI HII, NI LAZIMA CCM ITAWALE KWA MIAKA MINGI SANA...haijalishi nani anashinda uchaguzi...

Hili unaweza tu kuliamini kama ukifree up kichwa chako na kuuvaa Utanzania..
Nje ya mfumo unaotawala hakuna jamii yenye akili inayoweza kuhakikisha usalama wa nchi hii "jamii serious bado haijazaliwa"
 
WALOLA VUNZYA

JF-Expert Member
Nov 20, 2020
1,836
1,424
hahahahaha "Ukhanithi" Tindo nilijua hii mada lazima ufike tu...

Mtazamo wangu ni tofauti kidogo....
KWA USALAMA WA NCHI HII, NI LAZIMA CCM ITAWALE KWA MIAKA MINGI SANA...haijalishi nani anashinda uchaguzi...

Hili unaweza tu kuliamini kama ukifree up kichwa chako na kuuvaa Utanzania..
Nje ya mfumo unaotawala hakuna jamii yenye akili inayoweza kuhakikisha usalama wa nchi hii "jamii serious bado haijazaliwa"
Mawazo mgando hayo,Usalama wa nchi bila taratibu maalum ni uhaini.
 
Bejamini Netanyahu

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
64,645
68,584
Habari JF ,Hivi kama watu ,hasa vijana hampigi kura nini mnategemea ? Katika Uchaguzi mkuu wa 2020 watanzania waliojiandikisha kupiga Kura ni milioni 29.8 , lakini ambao hawakupiga kura ni milioni 14.8.

Sasa kama watu milioni 14.8 hawakupiga kura, si ndio hawa wanaojaza mikutano ya CHADEMA na kusumbua Social media ?Maana kwa Uzoefu wangu Wana CCM mambo ya Chama na Uchaguzi wako serious nayo sana hivyo hilo ni kundi kubwa la Upinzani.

Watu hawajapiga kura ,wameshindwa Uchaguzi ,hawatambui matokeo mambo mengine kama Bunge inabidi yaendelea JPM angefanyaje ? Hivyo nyie wenyewe ndio chanzo cha kina Halima na wenzake .

CHADEMA na vyama vingine anzeni kuelimisha wananchi umuhimu wa kupira kura muache kulialia kwenye media , mimi siku ya Uchaguzi nlikutana na vijana kama watatu hawajapiga Kura wote sababu kwamba kura Yake 1 itabadilisha nini?

Hizi kelele za mitandaoni ni watu wachache sana.​
Weka tume huru ya uchaguzi uone
 
mangikule

JF-Expert Member
Jun 11, 2012
5,228
4,199

Uchaguzi mkuu wa 2020 watanzania waliojiandikisha kupiga Kura ni milioni 29.8 , lakini ambao hawakupiga kura ni milioni 14.8.
Uchaguzi upi? Ulikuwepo uchaguzi kweli are you serious. Ndiyo kweli CCM huwa wako serious na wizi, na ujambazi wa kura wakishirikiana na polisi kuteka na kuua wapinzani!
Tunajua na wananchi wanajua CCM hawajawahi kushinda uchaguzi wowote toka 1995 hadi leo.
Hebu ona Jiwe alivyogaragazwa na Lowasa hadi akajipanga siyo kuiba kura bali kuiba mchakato wa uchaguzi 2020.
CCM na polisi hadi jeshi la wananchi na TISS wanashirikiana kufanya ujambazi wa kura kwa namna tofauti!
Tenganisha CCM na majeshi yetu tuone kama watatoboa!!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

1 Reactions
Reply
Top Bottom