Kama misikiti inaweza kujengwa mitaani kwa uhuru, kwanini kujengwa kwa makanisa kuwe kero Zanzibar?

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
10,115
35,129
Nimeshuhudia taarifa na video mtandaoni ikionyesha kanisa dogo la TAG maeneo ya Zanzibar likivunjwa na greda kwa amri ya wakuu fulani wa serikali wa Zanzibar.

Sababu za kimsingi za hayo kutokea ni kukosekana kwa uvumilivu wa kidini kwa baadhi ya wakazi wa Zanzibar dhidi ya imani zingine, jambo ambalo linalindwa na watawala wa Zanzibar kwa miongo yote. Japokuwa wakuu wa serikali huko Zanzibar wamekuja na sababu nyingine duni na kijinga (wanadai wamevunja kanisa hilo kwa sababu za taarifa za kitisho cha hali ya hewa kuhusu mvua inayoweza kuleta mafuriko maeneo hayo!).

Tunapaswa kutambua haya.
1. Karibu mitaa yote ya Zanzibar kuna misikiti mikubwa au midogo.

2. Karibu misikiti yote ya Zanzibar ina vipaza sauti (horn speaker) zinazopiga adhana kila siku kutwa mara tano.

3. Karibu misikiti yote ya Zanzibar imejengwa kwenye makazi ya watu au jirani kabisa na makazi ya watu.

4. Mpaka sasa Zanzibar haina maeneo rasmi ya wazi yaliyotengwa mahususi kujenga nyumba za Ibada tu na kujulikana kwa watu wote.

5. Serikali ya Zanzibar na serikali ya Tanzania kikatiba zote hazina dini na hazipaswi kufuata mlengo wa imani yoyote ya kidini zaidi ya kuheshimu na kulinda uhuru wa imani zote.

MAMBO MUHIMU YA KUTAFAKARI
-Kwa nini kuwe na shida kila mara dhidi ya taasisi za Kikristo zinapotaka kujenga makanisa, kuabudu kwa uhuru au kueneza imani yao maeneo ya Zanzibar?

-Kwa nini Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na serikali ya muungano zinashindwa kulinda uhuru wa kuabudu kwa wakristo waliopo Zanzibar?

-Kwa nini jamii za imani ya Kikristo zionekane kama ni wavamizi, wapitaji na wageni waliokosa mwenyeji kila mara huko Zanzibar?

TAFAKARI
 
Naona kuna tatizo hapa ; masharti, vigezo, desturi, imani na tamaduni haikuzingatiwa.

Unaweza kumiliki eneo lakini kuna masuala mtambuka ambayo mnunuzi hakuyazingatia akayaona ni mepesi, kumbe kuna mengine hayaandikwi lakini yanafuatwa na jamii husika wakaazi wenyeji wa mwanzo kabisa .


Serikali inaongozwa na watu, ila watu hao wana imani, desturi, tamaduni pia taratibu zao hivyo mtu makini hawezi kupuuza yale ambayo hayajaandikwa katika katiba.

Afrika itaangamia ...

31 Dec 2020 — Utamaduni usio dhibitiwa na unao sambaa kiholela ni hatari sana kwa kesho ya Afrika.
Utamaduni ni muhimu kwa wanasosholojia kwa sababu una jukumu muhimu na muhimu katika uzalishaji wa utaratibu wa jamii, ambayo inahusu utulivu wa jamii kulingana na makubaliano ya pamoja ya sheria na kanuni ambazo zinaruhusu sisi kushirikiana, kufanya kazi kama jamii, na kuishi pamoja (kwa hakika) kwa amani na maelewano.

Mfano hai wa babu zetu wanaelezea umuhimu wa utamaduni wao na unavyowasaidia kuishi wao kama jamii kwa amani


 
Nimeshuhudia taarifa na video mtandaoni ikionyesha kanisa dogo la TAG maeneo ya Zanzibar likivunjwa na greda kwa amri ya wakuu fulani wa serikali wa Zanzibar...
Hili Swala inabidi tuliendee bila kutumia hisia,nani hajui KERO ya makanisa ya kilokole yaliyotapakaa kila Kona ya nchi hii,kwa wakazi wa Dar,pale kawe Kuna makanisa kila Kona,yamefunga maspika makubwa,yaani yakiachia mziki mpaka mtaa wa saba masikio yanauma,Hawa wachungaji wa jasiliamali wao ni kuanzisha Kanisa kila Kona na mziki usiokoma.

Adhana ya waislam hai haichukui hata nusu saa,wakati ibada za kilokole ni siku nzima kuanzia saa sita na kuendelea.yule taperi mfalme zumaridi aliyekamatwa mwanza ni kwa sababu ya KERO,angekuwa amekamatwa Zenj,ingekuwa story nyingine.

Kwa Zenj,na nchi nyingi zenye wakristo kama minority group,kuwa na Kanisa au kuabudu kwa uhuru ni shida kidogo,hili serikali inabidi iliweke vzr.sasa kuhusu hilo Kanisa huko Zenj,lilijengwa kwa vibali?au ndio kama huku Bongo,yanaanzishwa kama uyoga Ili kupiga sadaka
 
Nimeshuhudia taarifa na video mtandaoni ikionyesha kanisa dogo la TAG maeneo ya Zanzibar likivunjwa na greda kwa amri ya wakuu fulani wa serikali wa Zanzibar...
Mimi naona huyo jamaa aliyejenga kanisa hapo hakufanya sawa. Kwasababu asilimia 98 ya wazanzibar ni waislam. Ni hatari hata kwa maisha yake japo gharama ya ukristo ni zaidi ya uhai na mali. Kuna vitu vingine unatumia tu common sense na kupotezea.
 
Hili Swala inabidi tuliendee bila kutumia hisia,nani hajui KERO ya makanisa ya kilokole yaliyotapakaa kila Kona ya nchi hii,kwa wakazi wa Dar,pale kawe Kuna makanisa kila Kona,yamefunga maspika makubwa...
Kero za kelele za magari, viwanda, matangazo ya simu, ndege kama KLM, kelele za masokoni, mafundi vyuma zote hizo huzisikii mitaani uje ukwazwe na kelele zilizokuwepo miaka na miaka 600 iliyopita ambapo hata kuzaliwa kwa Babu mzaa Babu yako hakuwepo hukuziona na hukerwi nazo lakini za Makanisa yazungukayo mtaa wako tu ndizo zikukere?

Ayseee kufa haraka ukaishi peponi kwenye bikra 72 na mito ya pombe ndipo hutakutana na kero hizo sababu hii dunia ni ya wote wala si ya dini flani pekee.
 
Nimeshuhudia taarifa na video mtandaoni ikionyesha kanisa dogo la TAG maeneo ya Zanzibar likivunjwa na greda kwa amri ya wakuu fulani wa serikali wa Zanzibar...
Aliekwambia serekali haina dini nani ? Zanzibar wakaazi wake wa kiislamu lakini skuli zinafuata kalenda ya kikristo na wala hawajalalmika miaka yote wakati wao ndio majority.

Tumeondoshewa lugha ya kiarabu ambayo inaendana na uislamu sasa imekuwa kiengereza ili watu wafahamu biblia vizuri. Bado waislamu wa Zanzibar wamekaa kimya.

Mie nadhani huo uvumilivu unaotaka wewe utakuwa labda ni woga. Serekali lazima ina dini kwa maana serekali ni watu. Na watu wote wana dini zao!

Wacha wakristo wajaze hayo makanisa walioyo nayo kwanza kabla hawajajenga mengine!

Maasalaam,
 
F
Hizi dini faida yake kubwa ni ukifaulu kuingia huko zilikoahidiwa!

Hapa duniani kumzuia mwemgine asieneze dini yake, huo ni upumbavu wa jinsi dini ilivyoegemea dunia kuliko kuleee ilikoelekezwa watu wake wafike!

Huu upuuzi unaletwa na ujinga mwingi usio malizwa na elimu dunia!
Mimi staki dini lako, kwa nini usiniache niwe na Uhuru wa dini yangu.??

Upuuzi mtupu
 
Kuna sababu sio bure.. Nadhani itakuwa ni noise pollution si unajua tena walokole FULL KUPIGA MAKELELE, MZIKI MNENE KAMA DISCO.

Makanisa ya kistaarabu kama Catholic mbona yanahudumia wakristo wa Zanzibar bila tatizo lolote tokea enzi za Sultan..?

Fundisho:
Ukienda kwa mamwinyi kuwa na ibada za kistaarabu, watu washatoka kupiga urojo, gahwa wamepumzika wewe unawapigia makelele? Wengine wanamabusha.. teh teh
 
Back
Top Bottom