Kama mimi ningekuwa Mkuu wa Mkoa/ Wilaya ningeanzisha utamaduni wa kutumia akili

GuDume

JF-Expert Member
Jan 18, 2015
6,652
14,247
Huu ungekuwa utamaduni wangu kuwa niwe natumia akili na si kiungo au sehemu nyingine ya mwili.

Kwa mfano, ningekuwa Mkuu wa Mkoa wa lile jiji ambalo vijana wale wanaobalehe walichoma bweni moto wala nisingehangaika na kwenda wachapa viboko hadharani.

Ningetuma watu wakachunguze na kuniletea report ya sababu ya tukio lile na adhabu kwa wahalifu. Halafu ningeita Wakuu wa Shule wote na wazazi pia wangealikwa. Tujadili report ile na madhaifu mbalimbali katika malezi, makuzi na elimu yetu kwa ujumla. Pamoja tungefikia sulihisho na kutoa hitimisho ambalo lingekuwa tamko la ushirikiano wetu sote.

Kama ningekuwa Mkuu wa Mkoa fulani pia nisingewaza kipuuzi kuwa watu ni lazima waoe na kuolewa na kama sivyo waadhibiwe. Ningefanya kongamano la wenye ndoa na wasio na ndoa kujadili changamoto zilizopo kwenye ndoa na masulihisho yake. Pia ningejadiliana na wadau nini sababu ya kutokuoa au kuolewa, tungepata majawabu ya kutusaidia kwa ujumla.

Ningekuwa Mkuu wa Mkoa nisingewaza kipuuzi kuwadhalilisha wanawake ambao walizalishwa na wanaume wakakimbia. Ningejisikia vibaya kuwadhalilisha wanawake na watoto wale, ningewaambia waende ofisi za ustawi wa jamii kila mtu kwa sehemu yake na wale wazazi waitwe yajadiliwe na sheria ifuate mkondo wake. Kesi zake ningezitumia katika kutafuta ufumbuzi wa matatizo mbalimbali. Lakini pia kutoa darasa suala la mimba zisizotarajiwa na athari zake.

Ningekuwa Mkuu wa Mkoa/ Wilaya fulani. Nisingeongea upumbavu kuwa wachawi wawaroge watu wakajiandikishe au kupiga kura. Ningejiuliza kwa nini watu hawataki jambo hilo? Ningefanya vikao na wenye viti wa mitaa, madiwani na wabunge. Ningefanya vikao na wananchi kupeana nao elimu na kuwasikiliza matatizo yanayowafanya wasitake kupiga kura.

Angalau hapo ningekuwa nimejenga kautaratibu kapya kakutumia akili kiasi fulani katika kutoa matamko. Naamini wenye akili zaidi yangu wangenishauri vizuri zaidi.
 
GuDume,

Ingependeza zaidi kama ungekuwa Rais usingeteua viongozi wa namna hiyo wala kuwapongeza kwa kutotumia akili zao kufikia maamuzi mbalimbali. Kutumbuliwa ingekuwa halali yao.
 
ungekuwa mkuu wa mkoa/wilaya ungekuwa dhaifu sana kwa kuogopa kufanya maamuzi kwa kuhofia macho ya watu. Uandishi wako unaonesha hivyo
 
Back
Top Bottom