Kama mimi ningekuwa kiongozi wa cdm ningefanyia nini 90 millions? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kama mimi ningekuwa kiongozi wa cdm ningefanyia nini 90 millions?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Goldman, Feb 15, 2011.

 1. Goldman

  Goldman JF-Expert Member

  #1
  Feb 15, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 1,261
  Likes Received: 852
  Trophy Points: 280
  My take, kama mimi ningekuwa ni kiongozi wa cdm ktk hizo 90 mil, ningewaamuru wabunge wote wa chama changu wanunue magari yasiyozidi 40 mil (yapo mengi new & used, nami ningewashauri wanunue used) maana gari ni muhimu kwa mtu yeyote, pia mwenye kutamani gari la anasa bado wabunge wana mishahara & marupurupu mazuri atajiongezea anunue hata (hummer) akitaka! Hela nyingine inayobaki 50 mil, wafungue ofisi za chadema saccos watoe mikopo kwa wajasiriamali yenye riba ndogo na endelevu.
  Mimi naamini viongozi wa cdm ni makini na wana uwezo wa kupata wafanyakazi makini ktk hizo cdm saccos zitazoanzishwa kila jimbo waliloshinda, 50 mil siyo hela nyingi lakini mkiwa na wafanyakazi makini lazima mtaendelea. Ni kitu kinachowafanya tujue kwamba nyinyi si kama ccm, maana wananchi wataona matokeo japo kwa mtaji kidogo ila tatizo kubwa ktk hili kusiwepo na bureaucratic. Ni kitu ambacho kikiwa well handled ni kitu endelevu, hela itaendelea kuwepo kuliko kuinunulia gari ya anasa wakati wananchi wana hali ngumu kimaisha. Ni mradi unaoweza kukua sana mkaja baadae mkaziunganisha! Lakini kwa kuanzia ni vizuri zikawa independent. Cha msingi ni watu wenye nia ya kuwatoa wananchi japo kwa uchache kutoka hali waliyopo kuwa endelevu. I was thinking aloud out of the ccm box, if you have progressive ideas post them. Sijataka kuzungumzia fedha za ruzuku etc, nimezungumzia hela wanayopewa ya kununulia magari tuu, Nawakilisha.
   
 2. Rwamuhuru

  Rwamuhuru Member

  #2
  Feb 15, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ni ushauri mzuri na wa kijamaa zaidi. mabepari wa zama hizi watathubutu kweli? anyway, hope wamekupata maana wapo humu
   
 3. W

  WildCard JF-Expert Member

  #3
  Feb 15, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Kwenye matumizi ya pesa hakuna "mwalimu" wa mwingine. Tuendelee tu na michapo.
   
 4. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #4
  Feb 15, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hebu fanya utafiti kwanza kabla ya kuzungumza. Hizo sio ruzuku kwa wabunge, ni pesa za mkopo ambapo hukatwa kwenye mishahara yao kila mwezi. Sasa hapo ana hiari kwani hizo ni pesa zinatoka kwenye jasho lake mzee
   
 5. D

  Domo Zege JF-Expert Member

  #5
  Feb 15, 2011
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 687
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Umefikir kitu amacho ni unique sana. Nafikiri wakikaa na kujadiliana vizuri hili linawezekana kabisa.
  Sababu baadhi yao ni wadau wa hili jukwaa nafikiri ujumbe utakua umefika
   
 6. Halfcaste

  Halfcaste JF-Expert Member

  #6
  Feb 15, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 973
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Hizo Saccoss unajua jinsi zinavyoendeshwa au umekurupuka? uhasama wa saccos na wateja unaujua? confiscation!nimefanya kazi za mikopo for more than 3years kwenye kampuni moja kubwa hapa nchini,acha its not a joke.Kukopa si tatizo kulipa mkuu!Disbursement is not an issue but loan realization.kwanza kabisa Watanzania wengi hawajui nn maana ya mkopo,mtu anakopa hela za Vibiashara(micro-credit) anaenda kununulia nguo,sofa,kabati...etc.mwisho wa siku lazima umfilisi tayari uhasama kati ya Mbunge na wapiga kura wake.uliza wapi Mabiloni ya JK???????

  Ndugu wabunge kama umebakiza viela kwenye hizo 90, nunueni madawati na changieni miradi mingine!nawasilisha mkuu:A S crown-1:
   
 7. Goldman

  Goldman JF-Expert Member

  #7
  Feb 15, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 1,261
  Likes Received: 852
  Trophy Points: 280
  I was thinking aloud out of ccm box! Ni kweli hela ni ya mkopo na wana uwezo wa kuilipa hiyo mikopo na bado wakawa na maisha bora!. Ccm wamechukua hela kama hizo kwa miongo kadhaa! nachowaza leaders wa cdm wasiwe kama wa ccm! Waje na ideas ambazo ni endelevu, wakaweka ubinafsi wao pembeni kidogo wakatanguliza maslahi ya wananchi (na bado wakaendelea kuwa na maisha bora) pia ni kama umewekeza cdm saccos ikikua ukii mind sana hela yako utarudishiwa. Ni mtaji wa kuanzisha jambo na kusema kwa vitendo, just thinking out loud!
   
 8. F

  Fahari omarsaid Member

  #8
  Feb 15, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 93
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wajibane wawanunulie vi2 vitakavyowasaidia wananchi
   
 9. P

  Paul S.S Verified User

  #9
  Feb 15, 2011
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Kunahitajika darasa pevu hapa kuainisha kazi na wajibu wa mbunge kama tutaanza kupigia mahesabu mapato binafsi ya mbunge kwaajili ya maendeleo ya wananchi, hii ndio maana dawje na rostam ni kazi kuwatoa majimboni mwao
   
 10. S

  Sina pa kwenda Senior Member

  #10
  Feb 15, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 116
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Crap
   
 11. Goldman

  Goldman JF-Expert Member

  #11
  Feb 15, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 1,261
  Likes Received: 852
  Trophy Points: 280
  Nalo ni wazo zuri na endelevu,
   
 12. MANI

  MANI Platinum Member

  #12
  Feb 15, 2011
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,862
  Trophy Points: 280
  Ni tegemeo langu kama kila mbunge ataweza kufanya jambo la kukumbukwa na wapiga kura wake kotokana na haya mapendekezo nadhani ni nafasi nzuri ya kurudi tena ifikapo 2015.
   
 13. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #13
  Feb 15, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Mwananchi wa kawaida akitaka huo mkopo atapata?
   
 14. Pukudu

  Pukudu JF-Expert Member

  #14
  Feb 15, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 2,970
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  hv na mawaziri nao si wabunge so it means hiyo mil 90 inawahusu tena! Khaaa na tayari si wana yale mavx au yale si kwa matumizi ya majimbo? Yaani afu wajawazito vibajaj mh huu ni utani. Kwa nini wabunge wasijununulie magari kutokana na posho na mishahara yao wakati ni mikubwa? Na 'wakikopeshwa' hizo pesa mil 90 ka wanavyosema wanarudisha?
  Ukilitafakari hili kwa kina maswali ni mengi kuliko majibu. Hata na sisi walimu wangetukopesha hata mil 1 tununue Toyo coz shule ziko mbali hamna nyumba za walimu na hatunaga transport allowance, this is not fair. Wakati sisi ndo tunafanya proffesional job ambayo ina now and future impact. Haya bana waheshimiwa nyie si mmeshika mpini! Ila iko siku utavunjika wote tutashika kwenye makali afu tuone sasa!
   
 15. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #15
  Feb 15, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  umeona eeh? Halafu jamaa anasema ANGEWAAMURU.
  Utamuamuru vipi mtu na mali yake.
  Hebu wapeni uhuru na nafasi.
   
 16. Halfcaste

  Halfcaste JF-Expert Member

  #16
  Feb 15, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 973
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Umenigusa mkuu.Wakati kikwete anamnadi Rostam Aziz kwenye uchaguzi wa october 2010 alisema "Huyu hahitaji Budget" "anajitosheleza" Hivyo basi bado hata Rais wetu hajui au anapotosha kuhusu majukumu ya msingi ya mbunge ili siasa ya Tanzania imilikiwe na Mafisadi.

  Hii yote ni Justification ya Zanzibar Revolution versus Azimio la Arusha.
   
 17. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #17
  Feb 15, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Masharti ya mkopo yanamruhusu kutumia kwa shughuli tofauti na ile ya kutolewa? Ninachojua ni kwamba Mbunge anatakiwa kununua Hard Top ambayo bei yake inasemekana haizidi milioni 90.
   
 18. newmzalendo

  newmzalendo JF-Expert Member

  #18
  Feb 15, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  milioni 90 ni pesa ndefu,na ni kweli unaweza kupata 4X4 for 40mil.
  Tukumbuke kupata ubunge walitumia pesa binafsi ktk kampeni,juhudi binafsi,kulipa matangazo,kulipa wapambe,na gharama za kafara na waganga ili kufacilitate kupata ubunge.
  hiyo 90million ni kurudisha gharama kwa awamu ya kwanza,then zinakuja posho za milioni 1 moja moja za vikao,posho za safari na ukaguzi wa miradi ktk hizo kamati za bunge.
  Siyo siri kila mtanzania anajua wabunge walikopa na kutumia vyanzo binafsi kupata huo ubunge,sasa tunalalamika nini kuona wanalinda maslahi yao.

  at the end of the day, Chadema,CCM ,cuf,UDP,NCCR wote ni kitu kimoja ktk swala zima la ulaji na kukomba pesa za walala hoi na wafadhili.na tukae kimya tuone mwenyekiti wa upinzani atasema nini juu ya hili la Millioni 90,hatosema wasichukue pesa,atalikalia kimya
   
 19. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #19
  Feb 15, 2011
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Ni kweli kabisa these are interest free loans, Ila hizi pisa wanazolipwa wabunge si jasho lao ni jasho la walipa kodi. Kwa kazi gani hasa wanayofanya ya kuwatoa jasho?, Kulala, kupiga makofi, kusema ndiyo et al. Baada ya miaka mitano tutajua ni wabunge wepi waliotoka povu kwa kutetea masilahi ya wananchi waliowachagua. Nina uhakika wabunge wote wa upinzani wamechaguliwa na hivyo wanapaswa kusemea waliowachagua, ila majority ya wabunge wa CCM ni wakupitishwa na tume ya uchaguzi.

  Ila ni jinsi gani watazifanyia hilo hela hiyo mipango ya mbunge binafsi na chama hakina haki wala sababu ya kutoa mwongozo kwenye hilo. Kikubwa ni kwamba wawe transparent, watuambie kila kitu siyo kama wale wa chama tawala ambao wao wanadai kila kitu ni siri. Tunaka Transparency kwenye governance ili kuondoa mianya ya rushwa na wizi wa mali za umma. Na CDM kwa kusema kuwa wamelipwa TZAS 90M ni mwanzo mzuri wa kuwa wa kweli kwa watanzania
   
 20. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #20
  Feb 15, 2011
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Tshs. 90,000,000 / (5yrs X 12 Moons) = Tshs 1,500,000/= kila mwezi anakatwa kulipia mkopo! Mshahara wa Mwalimu wa kawaida wa miezi zaidi ya saba. Kakopeshwa hivyo halafu anapewa pesa ya mafuta ya gari hilo la mkopo, wao wakifika petro station wananunua kwa Tshs. 2,500/= kwa lita-ndiyo bei waliopangiwa! Ukipiga hesabu pesa ya mafuta kwa mwezi wanayopewa, utaona kwanini watu wenye professional zao wana kimbilia kwenye ubunge!
   
Loading...