Kama Mimi ningekuwa Dkt. John Magufuli

Ne Mbwitu

JF-Expert Member
Aug 23, 2020
275
801
1. Ningeaziga jeshi la polisi na vyombo vya dola vifanye uchunguzi na kuwasaka wote waliofanya jaribio la mauaji ya Lissu.

2. Ningewaamuru Polisi wasiwapige mabomu wapinzani.

3. Ningefuta sheria zote kandamizi kwa amri ya rais (presidential decree)

4. Ningewaita viongozi wa vyama vya wafanyakazi na kuwaahidi kushughulikia madai yao

5. Ningehakikisha Lissu anapewa msafara mzito wa ulinzi katika kampeni zake

6. Ningemfuta kazi Mkurugenzi wa tume ya uchaguzi na kuteua mwingine

7. Nisingewapigia kampeni wabunge na madiwani wasiopendwa na wananchi wa eneo husika

8. Ningemwita Maalim Seif na kufanya naye mazungumzo

9. Ningemwita Mbowe na Zitto na kufanya nao mazungumzo.

10. Ningeendeleza unyeyekevu kwa kauli, matendo, na kuzungumza kwa upole.

Je, Kama wewe ungekuwa JPM!!!
 
Ningekuwa Mimi, ingewauliza washauri wapi tunakosea nakuwapima Kila mmoja uzalendo wake, halisi au la,upo kwa maslahi ya taifa au la. Na je, hawakuweza kuona mwelekeo wachama ulivyo? Je hawakuweza kuona mwelekeo was taifa ulivyo? Je ni kitu gani kifanyike kwa mustakabali mwema wa taifa letu.
 
Alipoingia tu madarakani akawaita viongozi wote wa vyama vya wafanyakazi na kuwahonga wake KIMYAA. Vyama vyote vya wafanyakazi wamejazwa mafia VIPENYO Wale wa pale makumbusho.
 
Ningekuwa Mimi,ningewauliza washauri wapi tunakosea nakuwapima Kila mmoja uzalendo wake,halisi au la,upo kwa maslahi ya taifa au la.Na je hawakuweza kuona mwelekeo wachama ulivyo? Je hawakuweza kuona mwelekeo was taifa ulivyo? Je ni kitu gani kifanyike kwa mustakabali mwema wa taifa letu.
Waliompoteza mzee # 1. Bashiru 2. Polepole.
 
JPM alidhani maflyover, mareli, ma-ndege ndio vitu vya kuombea kura. Kwa dunia ya leo hivyo vitu sio vya kutishia watu; hata watoto wanaviona kila siku kwenye Tv,simu,games nk

Watu wanataka furaha, amani, haki, heshima, shibe - kuishi bila hofu, wameyakosa haya kwa miaka mi5.
 
Lini sasa haa umechelewa tulikwambia ukatuziba midomo ukasema hujaribiwi, a country is not a company
 
Aibu kubwa, wewe unafikiri kuongoza nchi ni kama kuongoza JF (no pun intended) oops nyumba yako.
Kama Kuna MTU Alikudanganya Akakwambia Chadema Imekufa, Nikuambie Sasa Mimi Nimeshuhudia Chadema Iko Mioyoni Mwa Watu, Aseee.

Kwa taarifa yake huyo mpuuzi aliyetoa kauli hiyo ya kidwanzi, ataanza kufa yeye na Chadema ataiacha ikizidi kustawi.
 
14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom