Kama mh. Lema amepoteza ubunge kwa kosa la lugha chafu jukwaani..je..lusinde! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kama mh. Lema amepoteza ubunge kwa kosa la lugha chafu jukwaani..je..lusinde!

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Hhm, Apr 6, 2012.

 1. H

  Hhm Member

  #1
  Apr 6, 2012
  Joined: Apr 28, 2010
  Messages: 69
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Habari za siku wana jf na watanzania wenzangu, kwakweli nilikuwa sijawahi kufuatilia kile kilichokuwa kikizungumzwa mtaani kwa masikitiko makubwa juu ya mh. Lusinde kwa kile kilichoitwa lugha chafu katika jukwaa la siasa huko Arumeru, uvumi huu ulipozidi kuenea mpaka maofisini dhidi ya mbunge huyo ilinibidi nitafute video clip hiyo ili nijiridhishe kwa kile ambacho sikuwa naamini....kwakweli nilibaki mdomo wazi baada yakuona clip hiyo kwa jinsi mh. Lusinde bila kujali hadhi na heshima yake katika jamii matusi aliyokuwa akihubiri jukwaani wala haiitaji mwanainchi aende kufunguwa kesi mahakamani ....hapo ni moja kwa moja anapaswa ashitakiwe na serikali yake kwa kuvunja katiba ya nchi...nitashangaa sana endapo serikali ya jamuhuri italifumbia macho hili ....Mbunge huyu ambae amepewa ridhaa na.wananchi na akafundishwa maadili ya kibunge na kisha kuapa mbele ya Rais kuilinda na kuitetea katiba ya nchi matokeo yake yeye amekuwa mhimili katika chama cha mapinduzi kuhubiri matusi mazito na kashfa kiasi hiki.....hii ni kuidharau katiba ya nchi na watanzania wenzake ...kwa hakika haya soyo maadili yetu.

  Nikirudi kwa mh. Lema , mahakama imeona kuwa ndg Lema anastahili adhabu ya kupoteza ubunge kwa kile kilichoitwa kutumia jukwaa la siasa kutoa kashfa dhidi ya viongozi mbalimbali wa ccm, nimejaribu sana kupata walao clip ya mikutano ya ndg Lema ili nijiridhishe kwa kile ambacho mahakama imemhukumu mbunge huyu...lakini sijafanikiwa aidha kwa anayejua link anijuze...kwa maneno haya basi mimi naamini kuwa mahakamani ni mahali pakupatia haki hivyo basi kama ni kweli mh. Lema alitenda kosa kama hili la Lusinde mimi sina pingamizi wala rufaa dhidi ya hukumu ya Lema, lakini kama ni mbinu za kisiasa zimetumika .... Haya yatawatokea puani kwa wote waliohusika kupika hili....nawapa pole sana wanainchi wa Arusha kwa kumpoteza mbunge wao waliompenda But .... Niwaase kuwa bado naiamini CDM ina hazina kubwa ya vijana wasomi na mahiri hivyo waondoe shaka...endapo italazimika kufanyika uchaguzi na endapo isipotumika mbinu yakisiasa kumwekea pingamizi mbunge wenu basi atasimama tena....kinyume na hapo still siyo mwisho wapo vijana mahiri wengi CDM. Nawatakia pasaka njema.
   
 2. M

  Mpigaji JF-Expert Member

  #2
  Apr 6, 2012
  Joined: Feb 6, 2011
  Messages: 386
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Lema amevuliwa ubunge kwa kutumia lugha ya matusi na ubaguzi katika kampeni zake akigombea ubunge.Kama LUSINDE alitukana wakati anagombea,wanaotakiwa kufungua kesi ni waliokuwa wagombea wa vyama vingine!Jaji amepokea ushahidi uliomtia hatiani LEMA,kama unataka kuthibitisha nenda kwa Jaji aliyehukumu kesi ili uone kama kuna ukweli wowote!ACHA POROJO ZAKO!!
   
 3. Nzowa Godat

  Nzowa Godat JF-Expert Member

  #3
  Apr 6, 2012
  Joined: Jun 15, 2011
  Messages: 2,630
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Tunataka watu safi, siasa safi, lugha safi, roho safi, viongozi safi, na utawala safi. Ikiwa Lusinde nae katumia lugha chafu basi audience wamfungulie kesi.
   
 4. H

  Hhm Member

  #4
  Apr 6, 2012
  Joined: Apr 28, 2010
  Messages: 69
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Asante mpiganaji...ila sijui ni kwanini unaita hii ni porojo ...huo ushahidi wewe unaufahamu?? Unaweza ukadhibitisha hoja yako humu jamvini, kwa maelezo yako unamaanisha kuwa ukishachaguliwa kuwa kiongozi basi UBS uhuru wakutumia lugha chafu katika jukwaa la siasa?? Huoni kuwa hii siyo sahihi na mh. Lusinde anastahili kufunguliwa mashtaka tena na serekali yetu?? Na adhabu aliyoipata Lema yaweza kumkuta hata yeye??
   
 5. H

  Hhm Member

  #5
  Apr 6, 2012
  Joined: Apr 28, 2010
  Messages: 69
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Hayo yote uliyoorodhesha hapo ni sahihi kabisa, huo ndio msingi wa kiongozi bora na siyo mateja....Lusinde amevunja Katiba ya nchi waziwazi tena kwa makusudi hivyo anastahili adhabu isiyotofautiana na ile ya mh. Lema
   
 6. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #6
  Apr 6, 2012
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  subiri uone kama lusinde atachukuliwa hatua yyto ila angekuwa wa upinzani zamani sana ameshachughulikiwa
   
 7. m

  mchangia mada New Member

  #7
  Apr 7, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Lusinde alizungumza hayo maneno c wakati akimnadi mgombea wa chama chake, but kwa 7bu chama chake kimeshashindwa bac hakuna kesi hapo.
   
Loading...