Kama mfanyakazi akikosa kazi hasaidiwi, kwanini mkulima asaidiwe?

Jibu ni rahis tu,wakulima wasipolima au kusaidiwa mtakula mawe? Mfanyakaz anaweza jusubiri ajira hata miaka 5 lakin anakula kila siku kinachotoka kwa mkulima
 
Msemajiukweli kumbe na wewe huwa unafikira za kishirikina!
Mkuu,kadiri siku zinavyozidi kusonga mbele ndio naona ukweli wa matokeo ya ule utafiti kuwa kwa kila Watanzania wanne,basi mmoja ni "jiniasi".
"Mshike sana elimu,usimuache aende zake".
 
Hii nchi niya ajabu kweli!

Ibara ya 13(4) ya Katiba ya Tanzania inasema;
‘’Ni marufuku kwa mtu yeyote kubaguliwa na mtu au mamlaka yoyote inayotekeleza madaraka yake chini ya sheria yoyote au katika utekelezaji wa kazi au shughuli yoyote ya Mamlaka ya Nchi’’.

Tunaambiwa nchi hii niya wakulima na wafanyakazi!

Mkulima akikosa mvua anataka asaidiwe na serikali kupewa chakula.

Mfanyakazi akikosa kazi hasaidiwi hata pesa ya nauli kwenda kutafuta kazi.

Huu usawa na kutokubaguliwa tunaoambiwa ndani ya katiba uko wapi?

Kwenye nchi za wenzetu, mfanyakazi akikosa kazi anasaidiwa kwa kupewa pesa za kujikimu huku akitafuta kazi vivyo hivyo kwa wakulima ambao husaidiwa pesa za kujikimu na gharama za mazao yaliyopotea.

Kama mkulima anasaidiwa, basi hata mfanyakazi lazima asaidiwe.

Kama mfanyakazi hawezi kusaidiwa, basi hata mkulima asisaidiwe.

Hili suala lazima liangaliwe kwa upana zaidi ili kuondoa ubaguzi katika jamii.
Utakuaje mfanyakazi angali hujapata kazi...mbona mifano yako haieleweki mkuu...kajipange vizur then urudi ukiwa na usahihi wa unachotaka kusema.
 
Wafanyakazi wa sekta zote

Wakulima wengi wamelima mvua imekataa kunyesha hivyo mazao yao kuharibika. Na kumbuka huu ukame ni wa nchi nzima, kwa nneno marahisi ni baa la njaa. Je hao wafanyakazi wamefanya kazi wakaacha kulipwa mishahara yao? Je nchi nzima kuna tatizo lililoowakumba wafanyakazi wote linalofanana la kutokulipwa mishahara yao? Kumbuka hapa wakulima na wananchi hawaihusishi serekali kutokana na hasara kwani miaka yote wakulima hupata hasara achia mbali kulaliwa bei na huoni wakipaza sauti kuihususha serekali.

Hizi kejeli zenu kwa wakulima ni kwakuwa mmeajiriwa kwenye ofisi za wanaume wenzenu, huku mkiota vitambi kwa kula chakula cha bei za kutupwa kutokana na kuwalalia wakulima maskini hatimaye kuwaacha mafukara. Halafu nyie ndio mnajipendekeza kuwa ndio washauri wa rais huku mkikutana naye mnajifanya kumshauri na kutumia vijimaneno vya kiingereza chenye lafudhi ya kilugha. Acha kejeli za kishamba we mzee.
 
Hao wakulima wanalima na wanategemea hayo mazao kama chakula na kama chanzo cha kipato, hawana kingine kabisa, wakikosa mvua wamekosa kila kitu, huwezi fananisha na mtu aliyekosa kazi ambaye ana option nyingine za kujiajiri au kuishi kwa ndugu yake mwenye uwezo
Kukosa chakula nitofauti na kukosa kazi, chakula ni kati ya kifo na uhai,

Hongera dada yangu kwa kulitendea haki hili jukwaa. Huyu mleta uzi ni wale walioshiba mpaka kujisahau, hawa ndio wale wanaotulalia wakulima bei za mazao yetu huku huko maofisini wakijipangia mishahara mikubwa isiyolingana na tija yao kwenye taifa hili.
 
Hii nchi niya ajabu kweli!

Ibara ya 13(4) ya Katiba ya Tanzania inasema;
‘’Ni marufuku kwa mtu yeyote kubaguliwa na mtu au mamlaka yoyote inayotekeleza madaraka yake chini ya sheria yoyote au katika utekelezaji wa kazi au shughuli yoyote ya Mamlaka ya Nchi’’.

Tunaambiwa nchi hii niya wakulima na wafanyakazi!

Mkulima akikosa mvua anataka asaidiwe na serikali kupewa chakula.

Mfanyakazi akikosa kazi hasaidiwi hata pesa ya nauli kwenda kutafuta kazi.

Huu usawa na kutokubaguliwa tunaoambiwa ndani ya katiba uko wapi?

Kwenye nchi za wenzetu, mfanyakazi akikosa kazi anasaidiwa kwa kupewa pesa za kujikimu huku akitafuta kazi vivyo hivyo kwa wakulima ambao husaidiwa pesa za kujikimu na gharama za mazao yaliyopotea.

Kama mkulima anasaidiwa, basi hata mfanyakazi lazima asaidiwe.

Kama mfanyakazi hawezi kusaidiwa, basi hata mkulima asisaidiwe.

Hili suala lazima liangaliwe kwa upana zaidi ili kuondoa ubaguzi katika jamii.

1) Mfanyakazi anapata Bima ya matibabu, ana social security - mafao, na ana kiinua mgongo. Mkulima hana vyote hivyo.
2) Mfanyakazi hata akilala nyumbani kama anaumwa, miezi sita, analipwa mshahara kama kawaida. Mkulima akiugua imekula kwake.
3) Gharama za maisha zikipanda, mfanyakazi anapandishiwa mshahara, au marupurupu. Mkulima bei za mazao zikishuka, hivyo mapato yake kupungua, imekula kwake.
4) Mfanyakazi hawezi kupunguziwa mshahara, hata kama anashushwa cheo. Mkulima anaweza kukosa kabisa mapato kutoka mazao yake
5) Pamoja na hayo yote, mkulima anabeba uchumi wa taifa kwa mazao ya chakula na biashara. kumlinda mkulima ni kulinda uchumi wa taifa na kumsaidia mfanyakazi awe na uhakika wa kupata chakula.
6) kumlinda mkulima ni muhimu kwa sababu mara nyingi, na hasa kwa Tanzania, wakulima ndio waingizaji wakubwa wa fedha za kigeni, ambazo mfanyakazi ndio mtumiaji mkuu, anazitumia kuagizia gari, kulipia petroli na dizeli, kununulia mafriji, na vifaa vingine kutoka nje. mkulima yeye hata bia ya nje haijui, anakunywa Komoni. usafiri wake miguu. Hata kama kuna usafiri baadhi ya sehemu, na matrekta, ni kwa kiwango cha chini. hatumii bati, sehemu kubwa wanaezeka kwa nyasi. hatumii sementi bali udongo.
7) Pamoja na hayo, kama kuna njaa, misaada haiendi kwa wakulima tu. huko vijijini chakula cha msaada hata walimu, na wafanyakazi wengine walioko huko wanafaidi pia. mwaka 1974 unga wa Yanga ulikuwa kwa wote, maana njaa ilikuwa kwa wote mpaka mijini. kwa hiyo it is a matter of the seriousness of the famine.
 
Hao wakulima wanalima na wanategemea hayo mazao kama chakula na kama chanzo cha kipato, hawana kingine kabisa, wakikosa mvua wamekosa kila kitu, huwezi fananisha na mtu aliyekosa kazi ambaye ana option nyingine za kujiajiri au kuishi kwa ndugu yake mwenye uwezo
Kukosa chakula nitofauti na kukosa kazi, chakula ni kati ya kifo na uhai,
Kuna wafanyakazi wengi tu ambao kazi zao ni hand to mouth. Kama ajira ikikosekana basi hata maisha yao yanakuwa magumu.

Kujiajiri sio rahisi kama unavyotaka niamini. Kama kujiajiri ingekuwa ni rahisi hivyo basi kungekuwa hakuna waliokosa kazi wakati wana fani zao.

Hata kazi ni uhai na kukosa kazi ni kifo.
 
Back
Top Bottom