MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,991
Hii nchi niya ajabu kweli!
Ibara ya 13(4) ya Katiba ya Tanzania inasema;
‘’Ni marufuku kwa mtu yeyote kubaguliwa na mtu au mamlaka yoyote inayotekeleza madaraka yake chini ya sheria yoyote au katika utekelezaji wa kazi au shughuli yoyote ya Mamlaka ya Nchi’’.
Tunaambiwa nchi hii niya wakulima na wafanyakazi!
Mkulima akikosa mvua anataka asaidiwe na serikali kupewa chakula.
Mfanyakazi akikosa kazi hasaidiwi hata pesa ya nauli kwenda kutafuta kazi.
Huu usawa na kutokubaguliwa tunaoambiwa ndani ya katiba uko wapi?
Kwenye nchi za wenzetu, mfanyakazi akikosa kazi anasaidiwa kwa kupewa pesa za kujikimu huku akitafuta kazi vivyo hivyo kwa wakulima ambao husaidiwa pesa za kujikimu na gharama za mazao yaliyopotea.
Kama mkulima anasaidiwa, basi hata mfanyakazi lazima asaidiwe.
Kama mfanyakazi hawezi kusaidiwa, basi hata mkulima asisaidiwe.
Hili suala lazima liangaliwe kwa upana zaidi ili kuondoa ubaguzi katika jamii.