Kama MBIO ZA MWENGE zinahamasisha maambukizi ya UKIMWI kwanini FIESTA ISIAMBUKIZE? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kama MBIO ZA MWENGE zinahamasisha maambukizi ya UKIMWI kwanini FIESTA ISIAMBUKIZE?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Bajabiri, Sep 23, 2012.

 1. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #1
  Sep 23, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Kwa muda wa miaka kadhaa wadau wanahusiana na masuala ya ukimwi na VVU wamekua wakitoa maoni yao na kurusha shutuma kuwa mbio za mwenge ni kichocheo kikubwa cha maambukizi mapya ya ukimwi hasa linapokuja suala la mkesha wa mwenge,na hata baadhi ya kauli mbiu za mwenge zimekua ni kupiga vita maambukizi mapya ya ukimwi,
  Sote tunajua kuwa mwenge hukimbizwa karibu nchi nzima,hivyo huko kote watanzania hukutana kwa njia ya mwenge na wengine hufanya hayo wayafanyao,
  Lakini mimi najaribu kuangalia na upande wa pili,kwa sasa ni zaidi ya miaka 10 kuna hili tamasha kubwa la FIESTA ambalo nalo huzunguka sehemu mbalimbali za nchi japo si kwa kila mkoa,tamasha hili kwa sasa linanogeshwa na kampuni fulani ya bia,ambapo wanaopata bahati ya kuingia kupata burudan hulazimika kununua na bia ili kunogesha,
  Ikiwa pombe inalaumiwa hata kwenye mkesha wa mwenge hasa pombe za kienyeji kuwa huchangia ngono zembe,je kwa pombe hiyohiyo ingawa hii ni modern beer haichangii suala la maambukizi mapya ya UKIMWI NA VVU KWA VIJANA WETU??
  MTAZAMO WANGU:MBIO ZA MWENGE NA TAMASHA LA FIESTA NI VICHOCHEO VYA MAAMBUKIZI MAPYA,japo huenda baadhi ya wadau huenda wanahofia wakiitaja fiesta labda watakua wanaharibu biashara ya watu,lakini ni lazima hawa jamaa wajipange kuangalia ni kwa jinsi gani fiesta haiwez kuleta maambukizi mapya ya ukimwi,
  nawe toa mawazo labda wahusika wakisoma hapa watayafanyia kazi.
   
Loading...