Kama Mawaziri, Makatibu wakuu, wakuu wa mikoa na wilaya wanafanya kazi kulingana na utashi wa kiongozi wao, tunahitaji wasomi wa kazi gani?

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Yapo Mambo yanaenda kinyume na sheria na taratibu na bila kuona Nani anaelekeza yafanyike.

Yakitokea wasomi wanaulizwa mbona hapa sheria zetu hazisemi hivi? Wanajibu wameelekezwa kufanya na maelekezo ya mkubwa ni amri, ukiwauliza wakubwa wapo wengi, ni yupi mmoja wapo? Kimya

Kama nchi ndo inavyokwenda, kwamba ninavyojisikia leo ndivyo mtakavyokwenda wote, je wasomi Kama maprofesa wanahitajika kwenye nafasi kubwa? Au anayehitajika Ni mtu wa kusoma na kuandika ambaye ataenda kutekeleza?

Sidhani Kama tunahitaji kuwa na PHD kwa ajili ya kupokea na kutekeleza maagizo, ila tunahitaji phd kwa ajili ya kusoma na kuelekeza njia sahihi ya kwenda.
 
Kusoma siyo sana haimaanishi mtu anakuwa anauwezo wa kupambanua mambo,uongozi ni inborn.........
 
UJINGA ni adui mkubwa sana dunia hii. Ignoramus kwa domo lake anaweza kutamka KUNYWENI JIKI iwakinge na CORONA. Hayo hutasikia kamwe kutoka kinywani kwa MSOMI. Kasoma na kaelimika. Sio LUMPENI. Kauli za ku-lumpeni siyo za kubahatisha. Ni kotokana na UJINGA. No wonder!
 
Back
Top Bottom