Kama matokeo ya f4 2010 yamechakachuliwa je? Ni matokeo ya vijana ku-support upinzani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kama matokeo ya f4 2010 yamechakachuliwa je? Ni matokeo ya vijana ku-support upinzani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lu-ma-ga, Feb 2, 2011.

 1. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #1
  Feb 2, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,843
  Likes Received: 472
  Trophy Points: 180
  Kwa kuwa uchakachuaji umekuwa ni mtaji kwa serikali iliyopo madarakani ya JK,
  • Kuna baadhi ya watu wanajaribu kuhisi kuwa huenda matokeo mabaya ya mwaka huu ni mkakati uliowekwa makusudi wa kuwakomoa vijana wengi kwa kuwa hawakuwa upande wa CCM?
  • Pia kuna baadhi ya watu wanahisi kuwa, kwa kuwa serikali iko taabani kifedha imebidi kupunguza ufaulu wa wanafunzi hawa makusudi ili kuepuka kusumbuliwa na utitiri wa wanafunzi wanaojiunga vyuo vikuu kila mwaka? Na wengine wametoa matajrajio ya matokeo ya F6 mwaka huu yatakuwa mabaya pia ili kupunguza idadi ya wanafunzi watakaojiunga varsity kwa kuwa serikali haina mapesa
  Tujadili sote hili janga la kitaifa
   
 2. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #2
  Feb 2, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,919
  Likes Received: 12,106
  Trophy Points: 280
  Illiteracy analysis
   
 3. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #3
  Feb 2, 2011
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,525
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Wasahihishaji walipunguziwa muda wa kusahihi kwa madai Necta haina hela. Walichofanya ni kulipua kwa hasira . Matokeo yale sio ya kweli ,jamaa wameonyesha hasira zao tayari .Na hii ni nchi nzima .... Tunasubiri kuingia mitaani .
   
 4. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #4
  Feb 2, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280

  Hoja ya kwanza haina mashiko. ni propaganda. Kwani mitihani inatungwa na CCM?

  Tutasapoti upinzani ama kwa kufeli mitihani au kwa kufaulu mitihani.
   
 5. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #5
  Feb 2, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  walikuwa wanasahihisha mitihani ya private na shule za kata mchana kuanzia saa nane wakiwa wamemaliza kusahihisha shule zilizo chini ya wizara ya elimu na si tamisemi.
   
 6. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #6
  Feb 2, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Kila kukicha nchi hii linaibuka jambo.
  Mi nishachoka bana liwalo na liwe tuu.
   
 7. coscated

  coscated JF-Expert Member

  #7
  Feb 3, 2011
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 254
  Trophy Points: 180
  hilo nalo neno
   
 8. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #8
  Feb 3, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  "hoja na hitimisho lisilo makini". Mtihani hautungwi na ccm na wala usahihishaji haulipuliwi kama wadaivyo wasema ovyo. Usahihishaji na matokeo hufuata miongozo na uhakiki mzito kila hatua. Ukweli uko wapi? wewe unategemea vije mwanafunzi afaulu wakati hakuwa na mwalimu zaidi ya nusu ya muda wake wote wa masomo miaka 4? Afaulu vipi, wakati mtihani wa F. 2 uliondolewa hadhi yake ya kuchuja baada ya serikali kuona wameshindwa zaidi ya 80%, kwamba shule za kata zingekuwa na double madara sa ya F. 2 (wakariri na wapya) na kwamba kidato cha nne cha intake hiyo kingekuwa na watu wachache hakuna mfano wake tangu nchi ipate uhuru!!! Intake hiyo ndo F. 4 ya mwaka huu inaanza. F.4 na F6 ni mitihani usiyo wa kisiasa, unapima uhalisia bila kujali makunyanzi ya mtu, ndo matokeo hayo unayaona. Upanuzi wa shule zetu za msingi (PEDP) na sekondari (SEDP) bila mikakati mizuri zimetufikisha hapa. Tuache kujadili siasa na uongo wakati ukweli uko machoni kwetu jamani! Tunapoteza muda, au tunajifurahisha tu???!!!
   
 9. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #9
  Feb 3, 2011
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Embu tuwe wakweli kidogo watanzania tunajua sana bila ya kujua, matokeo yake mtihani unapokuja ndio umbumbu wetu unapo jionyesha. Si katai kuna suala la quality of education offered si nzuri. Lakini watanzania wa sasa ni wavivu especially vijana wa sasa, wao starehe na mambo ya miss, na kujifanya ma-celebrity.

  Kabla ya kulaumu serikali kwanza inabidi na wazazi wabebe part of the blame, and if i'm honest blame which is enough to be spread into other parts of our society. Yule binti tulie muona hapa, Mh.Kapuya kamkamata kwa fujo si ndio staili ya watoto wa sasa.

  Sasa kwanini wazazi, sehemu za starehe, vyombo vya dini kuto achiwa lawama kiasi kwa kuona hawa watoto wanavyo kuwa corrupted early in life na kubakia kimya. Kila nikifingua blog ya watanzania ni mamshindano ya ma-miss, party ya kampuni ya bia, na sherehe za harusi. Halafu mnategema wanafunzi wa faulu embu tuache kulaumu watu wengine hata kwa makosa yetu.
   
 10. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #10
  Feb 3, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Baseless imagination.

  Watoto wamefeli, tujipange upya sisi kama wazazi. Shule bora zipo ila tunang'ang'ania shule za TShs. 20,000 ili tubakie na mipesa mingi ya kuchangia harusi, mazishi, kuchoma nyama baa n.k.

  Tuwekeze kwa watoto bila kujali gharama.
   
 11. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #11
  Feb 3, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  nakuunga mkono kabisa asilimia 99
   
Loading...