Kama mambo yako hivi ndani ya Jeshi letu la Polisi, tunategemea kweli litimize majukumu yake ipasavyo?

Mathanzua

JF-Expert Member
Jan 4, 2017
15,841
20,687
Nakumbuka wengi tulipokuwa shuleni, Jeshi la Polisi ilikuwa sehemu ya mwisho kabisa ambayo mtu angependa kujiunga nayo kwa ajira.Wengi tuliona kwamba watu wanaoajiriwa Jeshi la Polisi hawakuwa na uwezo darasani. Kama hii inaukweli sijui, ila nadhani hii inatokana na muonekano wa ujumla wa Jeshi letu.

Sidhani kama ni siri kwamba makazi ya Jeshi letu ni duni sana, ingawa namshuru sana Rais wetu kwa juhudi zake za dhati za kuboresha makazi ya askari wetu.Kimsingi naomba juhudi hizo ziendelee. Jambo hili linadhalilisha sana askari wetu na hatimaye kuwafanya wasijiamini na kukosa ujasiri katika utendaji wao.

Ni kweli pia kwamba Jeshi letu halipati vitendea kazi vya kutosha, ikiwa ni pamoja na uniform.Pia mpaka sasa Jeshi la Polisi linatumia makaratasi kuhifadhi kumbukumbu zake mbali mbali katika vituo vyake. Hali hii ni hatari, kwa kuwa kumbukumbu mbali mbali za watuhumiwa zinaweza kupotezwa makusudi kwa nia mbaya. Hili halina budi kubalika na kutumia mfumo wa ki-electronic.Wizara ya Sheria tayari inatumia mfumo huu.


Zipo taarifa pia kwamba Jeshi halitengewi fedha za kutosha kwa ajili ya mafuta ya magari yake. Hali hii huwafanya viongozi wa maeneo husika kuomba mafuta ya magari kutoka kwa wanaoitwa "Wadau Waelewa," au kutoa hela mifukoni mwao kwa ajili ya kununulia mafuta.Ifahamike kwamba kuomba mafuta kwa mdau yeyote wa Jeshi ni sawa na kuomba rushwa na ni kitendo kinacholidhalilisha Jeshi na anayeomba. Si ajabu kwa hiyo kwamba Jeshi letu linatuhumiwa kwa rushwa, mazingira ya rushwa tunayatengeneza wenyewe. Naomba ikumbukwe kwamba mishahara ya askari wetu sio mikubwa kihivyo, kwa hiyo kumfanya askari atoe sehemu ya mshahara wake kwa shuhuli za kikazi ni kumuelemea isivyo halali, jambo ambalo linaweza kumfanya ashindwe kuhudumia familia yake ipasavyo, na hivyo kukosa ari ya kufanya kazi. Naambiwa viongozi wa Jeshi la Polisi wameridhia hali hiyo,inashangaza sana.

Kiukweli hali hii hufanya kazi ya Jeshi letu kua ngumu,hasa inapobidi kufuatilia matukio na kupeleka watuhumiwa mahakamani. Hii pia hufanya jeshi letu lidharaulike mbele ya macho ya jamii na kufanya kazi ya Jeshi letu kuwa ngumu sana, jambo ambalo viongozi wa Jeshi walipaswa kulitambua.

Hivi kweli tunategemea mamlaka ya Jeshi imkamate anayeitwa "Mdau Muelewa " au ndugu yake aliyechangia mafuta Kituo cha Polisi X, kama amehusika kwenye tukio lolote?

Jambo la kushangaza ni kwamba zipo taariifa za kuaminika kwamba askari wa kawaida wakilalamikia hali ilivyo kwenye Jeshi, viongozi wa juu wanawashuhulikia.

Swali la kujiuliza ni kwamba je, viongozi hawa wanafurahia utoaji duni wa huduma wa Jeshi letu unaotokana na matatizo yaliyopo?

Zipo taarifa pia kwamba askari wanapokwenda kwenye shuhuli za kikazi nje ya vituo vyao vya kazi kwa siku kadhaa, hawalipwi "night duty allowance(NDA)," badala yake wanaambiwa waende halafu wakirudi watadai.Hivi kweli ni mfanyakazi gani anayeweza kujilipa "night duty allowance," hata kama akirudi atadai? Kwa mshahara upi kwanza.
Hivi huku si kuwawafanya askari wetu wawe omba omba na kuhalalisha rushwa? Na kwa jinsi hii tuna sababu yeyote ya kuwalaumu askari wetu kwa kula rushwa?

Nadhani ni wakati muafaka sasa wa viongozi wa Jeshi la Polisi kupokea matatizo ya askari wanaowaongoza na kuyapeleka panapohusika,ili yapatiwe ufumbuzi, badala ya kuona kwamba askari hao ni adui. Ni wakati muafaka pia wa Serikali yetu kutatua matatizo yanayolikabili Jeshi letu,ili liwe Jeshi imara,linalotimiza wajibu wake kwa wakati na kujiamini.
 
Kipau mbele cha serekali yetu kwa jeshi la polisi ni virungu kwa wingi, mabomu ya machozi kwa wingi, magari ya washawasha kwa wingi, vingine hivyo siyo vipau mbele vya serekali yetu,askari polisi wataendelea kutumia akili zao kuvipata pamoja na maslahi yao.

Serekali ya CCM inachoangalia ni jinsi ya kumtumia askari polisi namna ya kuhami utawala wake kwa kuwapatia askari polisi zana nzito watakazo zitumia kuwadhibiti viherehere wanaojifanya kudai haki zao, ikiwa ni pamoja na kuwasweka lupango kwa kesi za kubambikizwa.
 
Wizara kutoa mgao wa kasma ya mafuta chini ya kiwango ni mbinu za kuhalalisha na kustawisha rushwa nchini Tz.

Hakuna kitendo kinacholidhalilisha 'geshi ra porishi' kama kutamka 'hatuna mafuta' kwa raia aliyeenda 'kuchoma' mharifu kituoni.

Majumba na mavazi hayafikii uozo wa polisi kushindwa kutimiza majukumu yao ya dharula kwa kukosa mafuta ama ubovu wa magari yanayoshindwa kutengenezwa hadi kupelekea amsha amsha ya Makonda yenye mrengo wa kisiasa!

Halafu ungewekwa utaratibu wa kufuatilia malalamiko halali ya raia juu ya utendaji mbovu wa jeshi la polisi, viongozi wa jeshi la polisi hadi wizara inayowasimamia ndiyo wangelionekana walivyo wazembe wasioliwajibikia jeshi na wangelimalizwa na kisulisuli cha tumbua tumbua!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama viongozi wao wameamua kuridhika na swala hilo la kugongea mafuta ilhali wanapewa na serikali,unafikiri hali iko kama ulivyoambiwa ipo?au kuna namna??

Swala ka kukubali kwenda kufanya kazi nje ya ofisi yako bila malipo,hili nalo ilaumiwe serikali au mhusika mwenyewe!!!maana taasisi nyingine utapigwa makofi na unayemtuma ukiagiza huo upuuzi.

Nyumba za kupanga zipo nyingi sana,wameamua wao kwa utashi wao na kupenda dezo kukaa kwenye hayo mabanda ya kufugia bata.

Yaani ukiangalia matatizo mengi ya jeshi la polisi ni from within,hayasababishwi kutoka nje yao bali ni ndani yao.siwezi sema sababu ni elimu,hapana.labda umasikini wa wengi wanakotoka.
 
Sakasaka Mao,
Kuna shida sana kwenye uongozi wa juu wa jeshi la polisi,niliongea na Askari mmoja akanambia zoezi wanaloliweza viongozi wake ni kukagua usafi pekee😁😁😁
 
mkorinto,
Mkuu nadhani kukaa kwenye uliyoyaita mabanda sio kupenda.Wanaona kwamba wakitumia vimishahara wanavyopata kwa pango,hali itakuwa mbaya zaidi kimaisha,kwa hiyo wanaridhika kukaa kwenye nyumba walizopewa duni.No wonder wanajihusisha na rushwa sana,ili ku-bridge the gap.

Nadhani pia ni kweli kwamba umaskini wa wengi walikotoka unachangia katika kukubali hali wanazokumbana nazo kazini.Sio siri kwamba askari wetu wengi wametoka kwenye familia duni sana.
 
Kipau mbele cha serekali yetu kwa jeshi la polisi ni virungu kwa wingi, mabomu ya machozi kwa wingi, magari ya washawasha kwa wingi, vingine hivyo siyo vipau mbele vya serekali yetu,askari polisi wataendelea kutumia akili zao kuvipata pamoja na maslahi yao.

Serekali ya CCM inachoangalia ni jinsi ya kumtumia askari polisi namna ya kuhami utawala wake kwa kuwapatia askari polisi zana nzito watakazo zitumia kuwadhibiti viherehere wanaojifanya kudai haki zao, ikiwa ni pamoja na kuwasweka lupango kwa kesi za kubambikizwa.
Mtizamo wako ni sahihi mkuu,ila hili lazima libadilike.Inahitaji courage kuwa askari Polisi Tanzania.Mimi siwezi na hata wao wanasema wapo kwa kuwa hawana alternative.Mtizamo huu sio sahihi,kwa kuwa unapaswa kufanya kazi kwa kuwa unaipenda.Hali ilivyo sasa kiukweli ni mbaya.
 
Rushwa ya ndani. Baadhi ya viongozi wa polisi wanachukua Sana rushwa kutoka kwa askari wa vyeo vya chini walio katika himaya zao. Yaani wamewafanya askari Kama misukule. Wapo wasiopenda vitendo hivyo Ila hawana pakusemea na Wapo wanaopenda kwakua wananufaika.


Hizi rushwa zinapunguza molari ya utendaji kazi wa askari.

Kanda ya ziwa siku moja nitakuja.
 
Back
Top Bottom