Kama mambo ndio haya (Tazama Video), Rais Samia aendelee kusafiri

Sep 17, 2021
39
84
Wiki tatu baada ya ziara ya Mhe. Rais Samia Suluhu nchini Misri, wafanyabiashara 111 kutoka nchini humo wamekuja Tanzania kuangalia fursa za kibiashara na uwezekaji.
Jitihada za Rais zinalenga kuimarisha sekta binafsi ili kuzalisha ajira na kupanua wigo wa kodi.

Mie naungana na wote wanaosema Rais aendelee kusafiri tupate faida za namna hii. Ni ajira zaidi zinatengenezwa, fedha mnazolalamika zinatumika kwenye safari zinarudi na kuwa na faida maradufu.

MAMA YUKO KAZINI

 
Ajira ngapi zimetengenezwa ? wanaweza wakawa wawekezaji 10,000 wakatoa ajira 100 au muwekezaji 1 akatoa ajira 1,000,000
 
Na mishahara ya laki kwa mwezi kama Wachina na WaVietnam. Mimi kwangu bora Wazungu
Pia huenda wanakuja kufanya kile ambacho waliopo wangeweza kufanya ila hawa wanapewa tax heaven, vivutio kibao kupelekea aliyopo kushindwa ku-compete....

Haya mambo bila kuyaangalia kwa undani na kufanya due diligence ni vigumu kuelewa kama yana tija au hapana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom