Kama makusanyo ya TRA yalikuwa 106% izo fedha zilienda wapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kama makusanyo ya TRA yalikuwa 106% izo fedha zilienda wapi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Njowepo, Jun 16, 2012.

 1. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #1
  Jun 16, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Tumeshindwa kuelewa inakuwaje TRA inakusanya mapato asilimia 106, yaani zaidi ya asilimia 100, wahisani tunaambiwa wametoa fedha asilimia 80,halafu eti fedha za maendeleo zilizopelekekwa wizarani ni asilimia 22 tu, haiwezekani na hapa tunataka uchunguzi ufanyike,”alisema mmoja wa wabunge wa CCM.
  MY TAKE
  Izo ni comment toka kwa mmoja wa wabunge wa CCM kwenye kikao chao jana.
  Inaonekana kuna wizi mkubwa wa fedha za serikali maana ata fedha toka sector ya madini kama 300bill haziko featured kwenye report za TRA.
  Isipofanyika special audit haya mafungu yataendelea kuliwa
   
 2. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #2
  Jun 16, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,198
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Mkuu kwenda Davos kwa kujialika unafikiri mchezo? achilia mbali safari zaidi ya kumi USA na kubembea huko jamaica na marastar hapo pata baki hata shilingi?
   
 3. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #3
  Jun 16, 2012
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Ina maaana matumizi ya kawaida ni makubwa zaidi ya budget
   
 4. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #4
  Jun 16, 2012
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,437
  Likes Received: 2,349
  Trophy Points: 280
  Wacha umanamba na wewe, jaribu kuandika kiswahili kilichonyooka.... unakuwa kama ulikimbia umande bwana. izo=hizo, ata = hata
   
 5. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #5
  Jun 16, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,800
  Likes Received: 3,884
  Trophy Points: 280
  Unataka uchunguzi upi tena ndugu yangu report ya CAG juzijuzi si iliibua uozo mwingi tu kwenye wizara na halmashauri? kilichofanyika mawaziri wakabadilishwa na wengine waliokuwa na tuhuma wakazawadiwa full minister mchezo kwisha! halafu unapoona watu wanajenga mahoteli makubwa, wantembelea hammer, pesa ndio hiyo!!
   
 6. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #6
  Jun 16, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,800
  Likes Received: 3,884
  Trophy Points: 280
  meaningless!1
   
 7. M

  Masabaja Senior Member

  #7
  Jun 16, 2012
  Joined: Mar 4, 2012
  Messages: 139
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mtu ameleta hoja nzito wewe na kichwa nazi unaona kukosea maneno ni jambo kubwa, ndiyo maana viongozi wanatudharau maana wanajua mambo ya msingi hatuyapi umuhimu tunakimbilia kwenye upuuzi kama ulivyofanya badilika.
   
 8. Mzalendo Mkuu

  Mzalendo Mkuu JF-Expert Member

  #8
  Jun 16, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 738
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Huyo Mbunge naye haelewi nini kinaendelea hapa Tanzania. Aende TRA akaulize siyo kuuliza bila mpango.
   
 9. kirumonjeta

  kirumonjeta JF-Expert Member

  #9
  Jun 16, 2012
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 3,090
  Likes Received: 499
  Trophy Points: 180
  Kweli Masabaja,Tujadili hoja jamani hayo mengine si tumeelewa lakini?
   
 10. Ciril

  Ciril JF-Expert Member

  #10
  Jun 16, 2012
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 5,536
  Likes Received: 1,468
  Trophy Points: 280
  Serikali yetu imekuwa ikilalamika na kutoa kauli zinazorembeshwa na waandishi wa habari kuwa "zimetafunwa na wajanja wachache".Sasa sie wananchi tutasema nini na kwa nani na ni nani atatusikiliza?Maisha acha yasonge vivyo hivyo mpaka siku sisi Kama wananchi tutaamua kubadilika kwa kuiondoa Serikali hii madarakani kwa njia ya kura au ya vita.
   
 11. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #11
  Jun 16, 2012
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,437
  Likes Received: 2,349
  Trophy Points: 280
  mimi na kichwa changu cha nazi nilishamkosoa na kumfundisha mara nyingi, lakini yeye anadhani kuondoa herufi za kwanza za maneno kama hizo, hata nk ni ujanja. Ndio maana sikubali kuwa amekosea ila ana tabia za umanamba. Hoja nzito ni ile inayotolewa kwa lugha sahihi.
   
 12. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #12
  Jun 16, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Inaelekea kuna fedha nyingi hapo hazina ambazo hazioneshwi kwenye mapato na matumizi ya serikali hivyo kuwa ndio nafasi ya kuziiba/kuzitumia hovyo!! Kuna umuhimu wa kufanya forensic audit pale hazina.
   
 13. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #13
  Jun 16, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,800
  Likes Received: 3,884
  Trophy Points: 280
  bila kubadili mfumo ni ngumu maana kuna mfumo dokozi uliojengeka nchi hii wanawekana kuanzia bot, hazina tra na sehemu zote nyeti hata report ya ukaguzi ya CAG naamini sii yote yanayoanikwa kuna mengi sana yanafichwa!Mimi nakuhakikishia kitakapokuja chama kingine kutawala madudu yatakayoibuliwa ya serikali hii ya sasa hayataelezeka!!
   
 14. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #14
  Jun 16, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  na kwa vile wameshaona 2015 hawana chao,basi haka kanchi katageuzwa sandakalawe hadi tukome
   
 15. Pendael laizer

  Pendael laizer JF-Expert Member

  #15
  Jun 16, 2012
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 961
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mimi naona hata CAG Wanaweza ficha uwozo kama nao watapewa fungu lao na nafkiri wanaongoza kwa kuiba ni wao manake wakipewa fungu wanapiga flat na kuisifia wizara huska. NCHI IMEOZA SANA HII
   
 16. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #16
  Jun 16, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Bwana Macho ninachoshukuru ni kuwa umesoma maneno bila shaka baada ya kuelewa!
  Mimi kama mwalimu ninalielewa ilo kuwa wanafunzi huwa wanaendaga offpoint
  Personally nilidhani la msingi ni kujadili huu wizi mwenzangu huna shida nao ila shida yako iko kwenye spelling na unajiita great thinker!
  We need to change for sure mambo ya msingi tuyape uzito na sio kuleta mzaha!
   
 17. n

  nderingosha JF-Expert Member

  #17
  Jun 16, 2012
  Joined: Mar 20, 2011
  Messages: 3,545
  Likes Received: 1,319
  Trophy Points: 280
  mizaha nchi hii ndio mfumo wa maisha ya watanzania...mambo ya msingi hufanyiwa mzaha na upuuzi ndio hupewa uzito..hili liko mpaka kwa watawala....Tukija kwenye issue hii ya mapato ya TRA...kwa kweli mi naona kama hawa wabunge wa CCM wamechelewa kuanza kuhoji hili...kwani karibia kila mwaka imekua ni kawaida kuambiwa TRA wamezidi malengo ya kukusanya kodi...lakini kila mara tunasikia matatizo kuwa pesa haziwafikii walengwa vijijini kuwaletea maendeleo...hata wahisani huwa wanatoa hela wanayo ahidi(hata kama inachelewa mara nyingine)lakini bado malengo ya kuwaletea maendeleo wananchi hayafikiwi...kwa kuwa hela zinatafunwa hazina...Nashangaa hili wanalisema sasa hawa wabunge.....

  My take:
  • Kuna haja sasa wabunge kuhoji si tu hazina kuu pesa zinaenda wapi bali hata lile fungu la ofisi ya rais....ambalo siku zote ni siri kwa wabunge....yaani mchanganuo wa fungu la ofisi ya rais(ikulu)..hili lazima wabunge wakomae nalo this time....kama watataka tuone wako serious...lazima wabunge wote...upinzani na ccm wahoji mchanganuo wa lile fungu la ofisi ya rais..ikulu...maana hutolewa kama lambsome..bila mchanganuo wa matumizi....hapa mimi nahisi nako kuna ufisadi mkubwa.....maana mafungu yote ya bajeti yana mchanganuo wa matumizi...lakini fungu la ikulu huwa halina mchanganuo....maana hapa ndipo kuna pesa za safari za rais za kila kukicha nje....wakati nchi haina pesa...Napata mashaka kuwa kuna pesa huwa zinachotwa hazina kuu kupelekwa ikulu....kwa safari za rais...maana wakati kila mwanasiasa alipokuwa analia kuwa serikali imefilisika haina hela..yeye JK alikuwa anasafikiri bila kuahirisha hata safari moja...sasa pesa zilikuwa zinatoka wapi?????wakati hata wafanyakazi kuna wakati walikuwa wacheleweshewa mishahara..yeye JK alikuwa anasafiri....pesa zilukuwa zinatoka wapi????.....wakati halmashauri zilikuwa zinalia pesa hamna..JK alikuwa anasafiri bila shida.....tena wakati mwingine na commercial flights.....Ni wakati sasa wabunge kuhoji loopholes zote za matumizi yasiyo na mpango ya hazina kuu......nina hakika ikulu wamechangia kutafuna hela hazina......i mean...kwa vimemo.....
   
 18. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #18
  Jun 16, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  kwenye blue ya kwanza si kiswahili fasaha,,,,,,kiswahili fasaha ni ACHA,kwenye blue ya 2 unajuaje kama mtoa hoja ni me???usikurupuke anaweza akawa ni ke,turudi kwenye mada ya mtoa mada,amejitahid sana kueleza,habari aliyoileta imetoka kwenye gazeti la mwananchi na mbunge aliyehoji ni ole sendeka,hili jambo lina mantiki sana wadau,pesa zinatumikaje?????
   
 19. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #19
  Jun 16, 2012
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,437
  Likes Received: 2,349
  Trophy Points: 280
  mwalimu gani kuandika kunakushinda... wewe ni hawa waandishi wachumia tumbo (zuzu magics) wa naofukuzana na vibahasha kila kukicha
   
 20. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #20
  Jun 16, 2012
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,437
  Likes Received: 2,349
  Trophy Points: 280
  Na wewe mkuu tangu uje na ule mpango wako uliotaka kunitapeli sh. milioni mbili nikakutolea nje umekuwa unaniandama andama sana. Mimi nilikataa kwa nia njema kwa sababu mradi wako ulikuwa hauna mbele wala nyume. Isitosha jamaa wengi niliozungumza nao walinipa historia yako nikaona wewe sio mtu wa kuaminika...
   
Loading...