Kama Mahiga, Nakubaliana na Njia ya Warioba Kwenye Serikali Tatu


M

maggid

Verified Member
Joined
Dec 3, 2006
Messages
1,084
Likes
398
Points
180
M

maggid

Verified Member
Joined Dec 3, 2006
1,084 398 180
Ndugu zangu,

Gazeti la Mwananchi leo Jumapili, mbali ya habari nyingine kemkem, libeba habari iliyonivutia kuisoma kwanza;" Dk Mahiga asema Katiba Mpya ni heshima"- ( Mwananchi, Jumapili, Juni 9, 2013).

Balozi Augustine Mahiga ambaye ni Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa UN nchini Somalia anizungumzia Rasimu ya Katiba kama jitihada za ubunifu katika kufikia mwafaka wa mazungumzo kuhusiana na kero za Muungano.

Balozi Mahiga anasema, kuwa ingawa Serikali Tatu zina gharama zake, lakini, kisiasa ina manufaa yake kutokana na mijadala ya muda mrefu kuhusiana na muundo wa Muungano. Balozi Mahiga anazidi kunukuliwa akisema, kuwa iwapo Rasimu hiyo itapitishwa na Watanzania, ni wazi kwamba Tanzania itakuwa imerekebisha kasoro za Muungano unaotimiza miaka 50 mwakani, kwa njia ya mazungumzo. ( Mwananchi, Jumapili, Juni 9, 2013, Uk 2)

Ndugu zangu,

Balozi Mahiga ameongea mengi mengine kuhusiana na Katiba, lakini, kwa mtazamo wangu, hayo ya juu yana uzito mkubwa sana. Ni maneno yaliyojaa hekima na busara nyingi kutoka kwa Mtanzania na Mwanadiplomasia mzoefu. Mahiga kwenye mazungumzo yake ametanguliza maslahi mapana na ya muda mrefu ya taifa.

Nakubaliana na Balozi Mahiga kwenye usahihi wa njia ya Jaji Warioba na Tume yake kuhusiana na Serikali Tatu.

Maana, njia ni ile ile tuliyokuwa tukihangaika kuifuata huku kukiwa na kero nyingi za njiani. Ni kwa vile njia ilikuwa nyembamba mno. Alichofanya Warioba na Tume yake ni kuipanua ili hata malori yaweze kupita.

Katiba Mpya ina maana pia ya Mabadiliko Makubwa. Ninachokiona mimi ni hofu ya mabadiliko kwa baadhi yetu. Na kwa wengine ni hofu inayotokana na sababu binafsi zenye kuambatana na kupoteza fursa hata nafasi za kimamlaka katika mabadiliko yanayokuja. Hivyo, ni sababu za kibinafsi zaidi nap engine hata kimakundi.

Ni hulka ya mwanadamu pia kuogopa mabadiliko yanapotokea. Hata kwenye nyumba yako tu. Siku ukirudi nyumbani ukakuta mfanyakazi wako wa ndani kapangua fenicha na kuziweka katika utaratibu mpya , basi, utaanza kwanza kuyaogopa mabadiliko yale. Na huenda akili yako isitulie pia. Kidogo kidogo utaanza kuyazoea.

Hili la Serikali Tatu kwa historia tu inabidi tupumue kwa akina Jaji Warioba kuja na ubunifu huu. Maana, imekuwa ni kero sugu iliyoundiwa hata Wizara. Hatuwezi kuendelea na hali hiyo mwaka hadi mwaka.

Maana, hata mimi binafsi, ningeulizwa mwaka 2000 juu ya muundo wa Muungano, basi, chaguo langu la kwanza lilikuwa Serikali Moja, pili, Serikali Mbili na tatu Serikali Tatu.

Lakini, miaka 13 baadae, na kwa kusoma alama za nyakati. Ukiniuliza leo swali hilo jibu langu liko wazi kabisa, kuwa tuwe na Serikali Tatu; Ya Muungano, Zanzibar na Tanzania Bara ( Tanganyika). Na hii si heshima tu tutakayoipata kimataifa, bali, itachangia kwa watu wa pande mbili hizi za Muungano kuheshimiana na kushirikiana zaidi.

Na tusisahu historia, kuwa Kamati ya Jaji Robert Kissanga mwaka 2000 ilikuja na mapendekezo kama haya ya Serikali Tatu.
Nakumbuka Rais Mkapa pale Diamond Jubilee akiongea na Wazee wa Dar es Salaam alionyesha dhahiri kuwa Serikali haikuyapenda mapendekezo yake.

Kukawa na hata mjadala kama Kamati inaweza kuja na mapendekezo au la, maana, ikasemwa kuwa ya Kissanga haikuwa Tume. Na Mkapa akawashambulia pia wanahabari kwa kutaka kuishinikiza Serikali kuyakubali mapendekezo hayo. Kitu ambacho hakiwezekani, maana, Serikali hata siku moja haiwezi kushinikizwa na wanahabari kama haikubaliani na inachoshinikizwa nacho. Lakini huo ulikuwa ni mwaka 2000, na sasa ni 2013. Wakati umebadilika.

Naam, na tuendane na wakati unaobadilika. Tuwe na ujasiri wa kuzipa mgongo fikra za ukale.

Maagid Mjengwa,
Iringa.
 
Nyani Ngabu

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Messages
82,399
Likes
50,141
Points
280
Age
29
Nyani Ngabu

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined May 15, 2006
82,399 50,141 280
Sikubaliani kabisa na huyo balozi!

Hilo wazo la serikali tatu ni upuuzi kabisa na sioni ni jinsi gani hizo serikali zinarekebisha kasoro za huu muungano wa kijinga.
 
m_kishuri

m_kishuri

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2010
Messages
1,493
Likes
47
Points
145
m_kishuri

m_kishuri

JF-Expert Member
Joined Jan 27, 2010
1,493 47 145
Thanks Mr. Magiid. Acha mjadala uendelee.

Binafsi ningependa kujua jukumu la mahakama kuu (Supreme Court) kwenye hili suala, hosusani itakapokuja kwenye Constitution conflicts and amendements ndani ya serikali tatu (kama zitakubaliwa). Kwani ndani ya serikali mbili tu, ilikuwa kasheshe kutatua matatizo ya muungano, sembuse serikali tatu.

Without a reliable and discplined Judiaciary system, tutakuwa tunakabana makoo kila siku. Inabidi Watanzania tuweke jazba pembeni na uzalendo mbele katika hili suala. We need to have a protocal on how to amend our constitution. Ikibidi na formula ziwekwe bayana ili kurahisisha mijadala.
 
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined
Jun 21, 2010
Messages
13,009
Likes
9,163
Points
280
Nguruvi3

Nguruvi3

Platinum Member
Joined Jun 21, 2010
13,009 9,163 280
Maggid, tatizo lako ni kuwa unapoweka mada kama hii huwa unaifanya kama taarifa na siyo majidiliano.
Kwa muktadha huo kwaweli inatia uvivu kuchangia.
Nakushauri urudi uwe unachangia na kubadilishana mawazo na watu, siyo kutupa halafu unakimbia.
 
cjilo

cjilo

JF-Expert Member
Joined
Sep 8, 2011
Messages
884
Likes
174
Points
60
cjilo

cjilo

JF-Expert Member
Joined Sep 8, 2011
884 174 60
umeongezea maoni yako kwenye uchambuzi wa mtu mwingine, lakini bado cjakuelewa, maelezo ni mengi lakini hakuna points, ungetuelezea faida za serikali tatu ni zipi na kwa nini huitaki serikali moja kidogo tungekuwa na hoja ya kujadili, serikali tatu inaondoaje kero za muungano?
 
C

Chang'o

Senior Member
Joined
Dec 21, 2012
Messages
105
Likes
1
Points
0
Age
41
C

Chang'o

Senior Member
Joined Dec 21, 2012
105 1 0
Inawezekana hata serikali 3 zisiwe suluhu ya kero za muungano, cha msingi ni wananchi kuridhia kuendelea kuwa na muungano. Ifanywe kura ya maoni wananchi wasema kama wanataka muungano uendelee au la, ndio baada ya hapo tujadili muundo wake.
 
M

maggid

Verified Member
Joined
Dec 3, 2006
Messages
1,084
Likes
398
Points
180
M

maggid

Verified Member
Joined Dec 3, 2006
1,084 398 180
Maggid, tatizo lako ni kuwa unapoweka mada kama hii huwa unaifanya kama taarifa na siyo majidiliano.
Kwa muktadha huo kwaweli inatia uvivu kuchangia.
Nakushauri urudi uwe unachangia na kubadilishana mawazo na watu, siyo kutupa halafu unakimbia.
Asante sana Nguruvi,

Huu ni mchango wangu mwingine wa fikra kuhusiana na Katiba...

Rasimu ya Katiba; Taifa linajivua gamba? ( Raia Mwema, Jumatano iliyopita)

Na Maggid Mjengwa,

MABADILIKO makubwa yamefanyika katika nchi yetu kwa mujibu wa Rasimu ya Katiba Mpya iliyozinduliwa wiki hii.

Haya ni mabadiliko makubwa kuwahi kufanyika tangu mwaka 1977. Ni mwaka ambao Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ilifanyiwa marekebisho makubwa. Mwaka huo wa 1977 yalifanyika mabadiliko makubwa pia kwenye uongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na hata ndani ya mfumo wa uongozi wa Serikali.

Naam, katika dunia hii, mabadiliko ya kijamii hupelekea mabadiliko ya kisiasa. Na Wanasholojia wanasema zipo sababu mbili zenye kupelekea mabadiliko hayo. Sababu za ndani ya jamii husika (endogenous) na sababu za nje ya jamii (exogenous).

Kwa upande wetu, tunaona kwamba sababu za ndani na za nje, kwa pamoja, zimesukuma kwenye kufikia hatua hii ya kufanyika mabadiliko haya makubwa ya Katiba.

Na kwa jamii yetu kwa upana wake, ina sababu za msingi za kuyafurahia mabadiliko haya, maana, ni sawa na mwanadamu aliyepewa kikombe chenye nusu ujazo wa maziwa.

Utafahamu kama amefurahia au amechukizwa kwa namna atakavyochagua kukielezea kikombe kile anayekiona ni ‘kikombe nusu cha maziwa' anaonyesha kutoridhika, na anayekiona ni ‘kikombe kilichobaki nusu tu kujaa' huyo amekifurahia na anaonyesha matumaini kuwa iko siku kitajaa. Inahusu kuwa na matarajio chanya (optimism) na kuwa na matarajio hasi (pessimism).

Binafsi, nichukue fursa hii kuwapongeza Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kwa kazi yao njema iliyotufikisha kwenye hatua hii ya kuwepo kwa Rasimu ya kwanza ya Katiba. Lakini, mwingine wa kupongezwa kwa ujasiri wake mkubwa wa kiuongozi, ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete.

Historia itamkumbuka Rais Kikwete kwa ujasiri wake wa kuachana na fikra za ukale na kuwa tayari, kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hii, kukaa meza moja na makundi yote, wakiwemo wapinzani wa chama chake kujadili mustakabali wa nchi yetu.

Maana, hili la Katiba halihusu mustakabali wa chama cha siasa, bali mustakabali wa nchi yetu. Vyama vya siasa vinakuja na kuondoka, lakini nchi yetu itabaki pale pale. Leo unaweza kuwa kiongozi wa chama fulani, lakini, mtoto wako au mjukuu wako, akaja kuwa mwanachama au kiongozi wa chama tofauti na chako.

Kwa ujasiri wa kuongoza mchakato huu wa Katiba, na kimsingi mabadiliko makubwa kwa maslahi ya taifa, Rais Kikwete anatupitisha kwenye ‘Jakaya-stroika' ya kwetu wenyewe, maana, kimsingi, mabadiliko mengi makubwa ya kimfumo, kiuchumi na kijamii, yanakuja kufuatia Katiba Mpya inayokuja.

Na katika dunia ya sasa, hakuna anayeweza kuyazuia mabadiliko yanayotokana na msukumo wa ndani ya jamii. Kwa mfano, Urusi ya zamani kule, Mikhael Gorbachev alipoanzisha mageuzi makubwa ya kisiasa, kiuchumi na kijamii katika Urusi, watu wake hawakuamini walichokiona.

Gorbachev aliuona wakati uliobadilika. Mabadiliko yale makubwa ya kimfumo kule Urusi yalipata majina mawili. Perestroika na Glasnot. Perestroika ina maana ya ujenzi mpya wakati Glasnot ni uwazi.

Kabla ya mageuzi yale makubwa, Urusi ilikuwa ikikabiliwa na tatizo la kuwepo na fikra za ukale na kukosekana kwa uwazi. Jamii ilijawa hofu, mambo mengi yalikuwa ya kufichaficha. Kulikuwa na usiri mkubwa!

Lakini, ndani ya kufichwa huko, kulikuwa na harufu ya uoza mkubwa. Gorbachev, daima atakumbukwa kwa kvunja ukimya na kuifanya Urusi kuwa nchi ya kisasa kama inavyoonekana sasa.

Na kwa hakika, ‘kuzaliwa' kwa Katiba Mpya yetu, ni sawa na Taifa letu kujivua gamba. Maana, kujivua gamba huku kama taifa, kunapaswa kuendane na kuanza kubadili mifumo yetu ya kifikra. Tuanze sasa kufikiri juu ya malengo ya taifa, kwa maana ya ndoto za taifa letu badala ya kutanguliza sana malengo ya vyama vyetu au zaidi malengo binafsi ya vyeo na mamlaka.

Nchi yetu ni kama nyumba kongwe. Tuendelee kwa umoja wetu kuifanya kazi ya kuikarabati upya nyumba yetu. Ipate mwonekano mpya. Kuikarabati upya nyumba kongwe, huweza pia kupelekea kuibomoa nyumba yenyewe.

Kutakuwa na fito na vipande vya matofali vya kurudishia. Kutahitajika fito na matofali mapya pia. Ndiyo, fito na matofali mengine yatakuwa ni ya kutupa tu, na ni lazima yatupwe, basi. Na hapo utakuwa umeikarabati upya nyumba yako.

Maana, katika jamii, mabadiliko yanapaswa yaendane pia na fikra mpya. Na jamii huingiwa na mashaka na kukosa imani pale fikra mpya zinapotekelezwa na watu wale wale ambao hawataki kabisa kuwaruhusu wengine kushiriki uongozi wa nchi.

Watu ambao bado miongoni mwao wanaamini kwamba tofauti za kifikra ni jambo baya. Kwamba upinzani ni uadui, ni uhaini. Kwamba wapinzani ni wa kuwakatakata na kuwatupa. Sasa, katika hali ya sasa utawachinja wangapi ukawamaliza? Ni fikra za kiwendawazimu tu!

Nchi yetu inapita sasa katika kipindi kigumu tangu tupate Uhuru wetu. Ni kipindi kinachowataka viongozi, na hususan viongozi wa kisiasa, kutanguliza hekima na busara badala ya jazba, chuki na visasi. Hayo matatu ya mwisho ni mambo maovu yenye kuambukiza kwa haraka.

Kamwe tusiruhusu jazba, chuki na visasi vitawale siasa zetu. Hii ni nchi yetu. Ni nchi yetu sote. Hakuna mtu, kikundi au chama cha siasa chenye haki zaidi ya kuongoza nchi hii kuliko wengine wote.

Na kwa mwanadamu, lililo kubwa ni uwepo wa matumaini. Na imani ya wananchi kwa taifa na viongozi wao, ni shina la matumaini yao. Inakuwaje basi mwananchi anapokosa imani na taifa, na hata kwa kiongozi? Katiba yetu iwe chachu ya kurudisha mioyo ya uzalendo kwa taifa letu.

Mungu Ibariki Tanzania. ( Makala haya yamechapwa kwenye Raia Mwema wiki jana)
 
Ngalikivembu

Ngalikivembu

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2010
Messages
1,920
Likes
364
Points
180
Ngalikivembu

Ngalikivembu

JF-Expert Member
Joined Oct 6, 2010
1,920 364 180
Kwa kweli kama rasimu hii itapitishwa na kukubaliwa serikali tatu, lazima wananchi wakubali kipindi fulani kuteseka hasa katika kuendesha serikali na kujua hasa mipaka ya serikali hizo.Kwa mfano kwenye serikali mbili watu wa Zanzibar wanalalamika kuwa wanaonewa, wakati huo huo sisi wa bara hatulalamiki zaidi ya kusema wenzetu wanapendelewa.Lakini ukitazama sana sisi hatulalamiki labda kwa sababu ya ukubwa wa eneo letu.Hatuoni tatizo.Kuna mambo ambayo si ya muungano lakini utaona wazanzibari wanaweza kushika madaraka hata kwenye mambo ambayo si ya pamoja na bado watanganyika wanakaa kimya hawalalamiki.Hili la serikali tatu lazima tutapata misuko suko.
 
Safari_ni_Safari

Safari_ni_Safari

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2007
Messages
23,232
Likes
7,106
Points
280
Safari_ni_Safari

Safari_ni_Safari

JF-Expert Member
Joined Oct 5, 2007
23,232 7,106 280
Sikubaliani kabisa na huyo balozi!

Hilo wazo la serikali tatu ni upuuzi kabisa na sioni ni jinsi gani hizo serikali zinarekebisha kasoro za huu muungano wa kijinga.

Suluhu ilikuwa ni kura ya maoni juu ya namna gani muungano uwe, na itafika siku hili litafanyika tu
 
Nono

Nono

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2008
Messages
1,347
Likes
145
Points
160
Nono

Nono

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2008
1,347 145 160
Inawezekana hata serikali 3 zisiwe suluhu ya kero za muungano, cha msingi ni wananchi kuridhia kuendelea kuwa na muungano. Ifanywe kura ya maoni wananchi wasema kama wanataka muungano uendelee au la, ndio baada ya hapo tujadili muundo wake.
MOSI:
Ndugu,
Ukusanyaji wa takwimu kwa minajili wa kujibu swali la kitafiti unaweza kuwa tofauti kujibu swali lile lile. Mathalan, unaweza kuhoji juu ya unywaji wa Bia: Wewe unakunywa bia ngapi? ________________________

Wapo watakojibu (sunywi, 0, 2, 20, nimeacha nk). Pia swali hilo lingewza kuulizwa 1)Unkunywa bia (n/h), 2) kam ndio, ni bia ngapi?.

Mwisho wa siku tutapata jibu, ila njia ya pili ni ya mzunguko na gharama ikihamishiwa kwenye kukusanya maoni ya katiba.

PILI:
Wengine wanaweza kusema serikali 3 sio tiba ya muungano. Ni kweli kama serikali 2 zilivyoshindwa kuwa tiba, huoenda serikali moja ingekidhi. Tume ile iliundwa na watu mahiri ambao walipima kwa marefu na upana wake mawazo, maoni na vionjo mbalimbali vya wanachi kutoka pande zote mbili. Hivyo, angalao serikali 3 zinaweza kutuliza kiu ya wengi, japo sio muarobani.

Mimi ningependelea serikali moja, lakini hilo kwa wengine hawatakubaliana nalo. Sasa nini kifanyike?
 

Forum statistics

Threads 1,274,693
Members 490,736
Posts 30,521,144