Kama Magufuli asema kweli maendeleo hayana vyama, basi ampandishe cheo askari wa polisi aliyemkatalia kiongozi wa CCM alipoamriwa kutoa salamu ya CCM

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,143
18,769
Katiba iko wazi. Vyombo vya sualama kutia ndani Polisi hawapaswi kuwa watwana wa viongozi wa vyama vya siasa hata kama chama hicho cha siasa ndio kimeshika serikali. Polisi wanapaswa kujiendesha kulingana na kanunu za kutofungamana na chama chochote cha siasa.

Sasa inapotokea kwamba kiongozi wa CCM anamwamuru askari wa polisi, kwamba kabla ahajatoa maelezo, awasalimie kwa kutumia salamu ya CCM, huo ni ulevi, uwendawazimu na umbumbumbu wa madaraka. Unakupa taswira ni kwa nini nchi hii chini ya CCM ina migongano mingi sana ya mipaka katika utendaji wa kazi kati ya CCM kama chama kilicho madarakani na watendaji wa serikali chini ya uongozi wa CCM. Kwa kifupi, CCM, kuanzia Raisi Magufuli mwenyewe, hawajui mipaka yao ya utendaji kama chama inaishia wapi. Wanadhani kuwa chama kinachoongoza serikali kunawapa mamlaka ya kuvunja katiba pale inapotenganisha utendaji wa kazi ki-chama na ki-serikali.

Hili limetokea huko Pwani ambapo kiongozi wa CCM anamwamuru polisi atoe salamu ya ki-CCM, na askari polisi alipogoma akifafanua yeye ni mtendaji ambae hawezi kujifunga na chama cha siasa, aliamuriwa aondoke. Na kwa kiburi kabisa, huyo kiongozi wa CCM aliouliza jina lake na cheo chake bila shaka kwa madhumuni ya kumfuatilia na kumkomoa baadaye.

Sasa kama kweli Magufuli ni kiongozi makini anapaswa kufanya yafuatayo;
  1. Ampandishe cheo huyo askari kwa kuonyesha ujasiri na werevu katika kutenganisha majukumu ya polisi na chama tawala cha CCM
  2. Amchukulie hatua kiongozi wa CCM aliyekuwa akimlazimisha askari wa Polisi kutoa salamu ya CCM kwa kuleta mgongano kati ya Polisi na CCM
Video clip:
Pwani: Askari Polisi agoma kusema CCM oyee. Afukuzwa kwenye mkutano na kiongozi wa CCM, aambiwa atakiona

1565861154350.png
 
View attachment 1181960

Kama ni salaam haina madhara kwanini wewe uanze kumdhuru kwakuwa amekataa kusema vile utakavyoo, kwani kutosema vile kunakuathiri nini
 
Umeandika as if hakuna mpianzani aliyeteuliwa na kupewa cheo kikubwa.
Mpinzani akiteuliwa na kupewa cheo kikubwa lengo ni kumfanya aachane na upinzani. Unataka mifano? Na usinipe mfano wako kuwa ni Lyatonga Mrema. Yeye ni wa kuhurumiwa tu.
 
Katiba iko wazi. Vyombo vya sualama kutia ndani Polisi hawapaswi kuwa watwana wa viongozi wa vyama vya siasa hata kama chama hicho cha siasa ndio kimeshika serikali. Polisi wanapaswa kujiendesha kulingana na kanunu za kutofungamana na chama chochote cha siasa.

Sasa inapotokea kwamba kiongozi wa CCM anamwamuru askari wa polisi, kwamba kabla ahajatoa maelezo, awasalimie kwa kutumia salamu ya CCM, huo ni ulevi, uwendawazimu na umbumbumbu wa madaraka. Unakupa taswira ni kwa nini nchi hii chini ya CCM ina migongano mingi sana ya mipaka katika utendaji wa kazi kati ya CCM kama chama kilicho madarakani na watendaji wa serikali chini ya uongozi wa CCM. Kwa kifupi, CCM, kuanzia Raisi Magufuli mwenyewe, hawajui mipaka yao ya utendaji kama chama inaishia wapi. Wanadhani kuwa chama kinachoongoza serikali kunawapa mamlaka ya kuvunja katiba pale inapotenganisha utendaji wa kazi ki-chama na ki-serikali.

Hili limetokea huko Pwani ambapo kiongozi wa CCM anamwamuru polisi atoe salamu ya ki-CCM, na askari polisi alipogoma akifafanua yeye ni mtendaji ambae hawezi kujifunga na chama cha siasa, aliamuriwa aondoke. Na kwa kiburi kabisa, huyo kiongozi wa CCM aliouliza jina lake na cheo chake bila shaka kwa madhumuni ya kumfuatilia na kumkomoa baadaye.

Sasa kama kweli Magufuli ni kiongozi makini anapaswa kufanya yafuatayo;
  1. Ampandishe cheo huyo askari kwa kuonyesha ujasiri na werevu katika kutenganisha majukumu ya polisi na chama tawala cha CCM
  2. Amchukulie hatua kiongozi wa CCM aliyekuwa akimlazimisha askari wa Polisi kutoa salamu ya CCM kwa kuleta mgongano kati ya Polisi na CCM
Video clip:
Pwani: Askari Polisi agoma kusema CCM oyee. Afukuzwa kwenye mkutano na kiongozi wa CCM, aambiwa atakiona

View attachment 1181960

Kama rais mwenyewe alipokea wanaccm kwenye kamisheni ya jeshi huko Arusha, anapata wapi moral authority ya kumsifia huyo polisi? Kimsingi hiyo jeuri ya wanaccm dhidi ya vyombo vya dola inatokana na katiba inayompa rais nafasi ya kuchagua mkuu yoyote wa vyombo vya dola na taasisi mbalimbali ikiwemo jeshi la polisi. Ikumbukwe cheo cha IGP, kinatoka kwa utashi wa rais, na ni baadhi ya vyeo ambavyo unapata marupurupu mengi ya halali na yasiyo halali ambayo huondoa weledi na kutii chochote atakacho aliyekuteua, kinyume na hapo anamteua mwingine amtakaye.

Sasa kwakuwa IGP ndio boss was polisi wote anapopewa amri yoyote na mamlaka yake ya uteuzi, hana namna zaidi ya kutii ili kulinda marupurupu yake hasa yale yasiyo ya halali, kwani akienda kinyume atayakosa. Hii ndio sababu hata askari wa chini anaweza kukemewa na mwanaccm yoyote na IGP asifanye lolote kwani huo udhalilishaji una baraka za boss wake. Kibaya zaidi hata IGP akiamua kusimamia weledi, bado polisi wa chini yake anaweza kupokea amri toka juu na akatekeleza na huyo IGP akaambiwa asimguse. Hapa ndio pale kundi la watu wasiojulikana linapopata nguvu kuliko vyombo vya dola.
 
Back
Top Bottom