Kama Maandamano ya Kumpongeza Magufuli ni sawa, Pia yafanyike ya Kumlaani kwa Mabaya!

TL. Marandu

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
3,628
2,000
Ati nimesikia Kunafanyika Maandamano ya Kumpongeza Magufuli kwa Kuzuia Mchanga wa Magwangala asilimia 5% ya Dhahabu inayoibiwa Tanzania yasisafirishwe, Wakati huo huo asilimia 95% Ikiwa inachukuliwa Jukwa juukutoka Migodini kwa Private Jets!

Mimi Nasema Wanaompongeza Wanayo haki kikatiba, Kufanya hivyo! Na Waandamane! Lakini kuna haya Machafu aliyofanya Magufuli mifano michache ni

1) Kuwafukuzia watoto 7900 wa UDOM na kisha Kuwatukana ati ni Villaza!
2) Kung'ng'ania kuweka Kaimu Judge Mkuu kwa zaidi ya miezi Sita kwa Lengo ovu la kuuchukua Mhimili wa Mahakama Msukule
3) Kumwagiza Msukule wake wa kisiasa, Ndugai awafukuze Wabunge wasiompigia Makofi Bungeni, ili aweze "kudeal" nao.
4) Kumpakata Bashite Jambazi na Mfoji vyeti wakati akifukuza Maelfu ya Wengine Waliofoji Vyeti.
5) Kuiba 2.7 Billions Hazina na Kuhonga Nazo Wabunge wa CCM 10millions @
6) Kupakata Mkuu wa Mkoa wa Arusha Gambo, Aliyepora Rambirambi, na kuwafunga walioenda kutoa Pole! Aibu na ovyo ovyo ovyo! Pia ikumbukwe huyu pia kavuruga Msiba wa Ndesamburo Mb.
7) Kwa kumsaidia Lipumba, Msukule mwingine, kuvunja Ofisi za CUF, Na pia Kutumia Walinzi aliompa Kwenda Kulabua Waandishi wa habari makofi! Huku wamevaa kininja! Ati doria unafanya doria kwenye premises za wengine, na huku umevaa kininja! Maelezo ya kunya! Na bado victims ndio wanashitakiwa!

Mimi nadhani Kwa haya Machache, watakao andamana kumpongeza Magufuli historia itawahukumu. Ingawa nawasamehe wengine Maana Zitaibiwa Billlions Kadhaa tena huko Hazina Walipwe kuandamana. Hii sio siri kuwa huyu anafanya Political Stunt!

Magufuli na Bashite akili zao zinafanana! Childish media Manipulation na Novice Political stunts ndio Trade Mark yao!

Nakumbuka hili la Michanga sio Jipya Amini Alishawafukuza Wahindi wenye Asili ya Kiingereza na Kisha Akajitapa ana Uwezo wa Kuwatumia Waingereza Chakula, Kwa Kebehi akachanga na Lori moja la Mboga mboga akamwambia Waziri Mkuu wa Uingereza alifuate! Alishangiliwa sana na Wajinga jinga aina ya Misukule na Cheerleader za kule Dodoma, Lakini yuko Wapi?

Chiluba Mlokole kama mie, (Maana mimi sichezi na kima hata kama ni kabila langu, dini yangu, au hata kama ni baba mzazi) Huyu mla aliyekuwa Corrupt to the core, Mshenzi na Mnafiki, aliyejitia Msafi akamweka Kaunda ndani kwa kufanya Political stunt ya Uwongo ya Kutaka, "Kujipindua" ili kaunda aonekane ndiye yeye alipanga Mapinduzi, ( Why he did this, uchaguzi ulikuwa umekaribia na tetesi zilikuwa Kaunda alipanga kugombea tena) akamweka Kaunda Ndani akasema Ukiua kwa Upanga Utakufa kwa Upanga, akamwachia Pale Nyerere, Mugabe na Mseven walipomwambia asilomwachia Kaunda watamtoa Utumbo! Chiluba yuko wapi?

Watch Malipo yako hapa Duniani, Ukiwa Kiongozi acha Unafiki, Hila, Uhuni na Uonezi, Tenda na Ongoza kwa haki Utapata heshima isiyofutika, hata pale itakapochelewa historia Itakuenzi tu!

Nasikia Kukerwa!
 
Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
15,102
2,000
Sijasikia ACACIA wakijitetea, bali namsikia Mtanzania mwenzetu Tundu Lissu katika maandishi na video zinazoenezwa mtandaoni kwa kasi ya ajabu akiwatetea kwa nguvu na kwa pumzi zake zote. Ni kuhusu mchanga wenye madini uliozuiwa na Serikali bandarini. Amezungumzia mambo ambayo nitayajibu hapa kwa lengo kubwa kabisa la kutaka Watanzania wafahamu.
Je, sheria inasema mchanga ni mali ya ACACIA?

Lissu anasema kuwa kwa mujibu wa sheria mchanga ule ni mali ya ACACIA na hivyo Serikali kuuzuia ni sawa na kuzuia mali ya mtu. Kuhusu hili sijui amezungumzia sheria ipi? Katika Sheria Namba 14/2010 Sheria ya Madini hakuna jambo la namna hii kama Tundu Lissu anavyotaka kuliweka.

Hakuna popote ilipoandikwa kuwa mchanga wote unaochimbwa ni mali ya ACACIA. Na hili linajulikana kwani hata leseni za uchimbaji hutolewa kwa ajili ya uchimbaji madini na siyo umiliki wa ardhi. Ardhi ambayo hujumuisha mchanga hubaki mali ya Taifa.

Lakini pia katika hilo hilo lazima ieleweke kuwa hawakuwa wakichukua mchanga kwa sababu ni mali yao kama Lissu anavyosema. Hata wao hilo wanalikataa. Wanasema wanalazimika kubeba mchanga kwa kuwa hapa Tanzania hakuna kiwanda/mtambo wa kuchenjua mchanga na kupata wanachokitaka. Hawasemi walikuwa wanachukua mchanga kwa sababu ni mali yao, hapana. Ni utetezi wa Watanzania wenzetu unaosema mchanga ni mali yao.

Je, Acacia wametenda kosa lolote?

Lissu na kundi lake wanawatetea ya kuwa hawajatenda kosa lolote. Ni hivi, ukweli ni kuwa kuna makubaliano maalumu kati ya Acacia na Serikali kuwaruhusu kuchukua mchanga kwenda kuuchenjua katika kipindi ambacho Serikali itakuwa haijajenga mtambo wake.

Hata hivyo, lazima ieleweke kuwa makubaliano haya yanakwenda sambamba na wajibu wa kisheria wa kutoa taarifa sahihi kuhusu uzito wa kile wanachochukua pamoja na sampuli zilizomo.

Kuthibitisha kuwa wajibu huu upo, ndio maana mchanga huo hukaguliwa, na wao hukubali ukaguliwe na TMAA, TRA, nk. Mchanga haukaguliwi ili kujifurahisha, hapana. Unakaguliwa ili kujua uzito na sampuli za kile kinachochukuliwa.

Basi, hatua ya wao kukubali kukaguliwa na mamlaka hizi kwa malengo haya ya kujua wanachukua nini inathibitisha hata wao kuutambua wajibu wao wa kusema ukweli kuhusu uzito na sampuli za kile wanachobeba.

Sasa swali ni kama wajibu huu upo na wao wanautambua kwa kiwango hiki; je, kuukiuka kwa kudanganya kuhusu uzito na sampuli ni kosa au si kosa? Akili ya kawaida tu ya mtu ambaye hata siyo mwanasheria itapata jibu. Halafu anatokea Mtanzania anasema hawajafanya kosa lolote.

Lakini pia ukidanganya kuhusu uzito na sampuli utatoa mrahaba ulio chini ya kiwango, chini ya kile ulichotakiwa kutoa. Bado baadhi ya Watanzania wenzetu wanasema hilo nalo si kosa! Inasikitisha sana.

Makala yaliyopita nilieleza kwa urefu kosa la udangayifu hapa kwetu na huko kwenye mahakama za kimataifa. Muda huu itoshe tu kusema kuwa, jamani udanganyifu ni kosa (fraud/deceitful).

Na ni kosa pote mahakama za ndani (local courts) na katika hizo za kimataifa (International Arbitral Tribunal). Na hakuna shaka imethibitika makosa haya wameyatenda. Haya iko wapi hiyo kesi inayopigiwa debe kwa nguvu zote kuwa lazima tunashindwa?

Je, ni kweli ripoti ya Mruma ni takataka kama inavyoitwa?

Lissu anaiita Ripoti ya Tume ya Mruma- takataka, na kusisitiza kwa Kiingereza kuwa ni ‘rubbish’. Kwanza niseme kuwa maneno haya ni ya dharau kubwa kwa Profesa Mruma na wasomi wote aliokuwa naye kwenye kamati. Lakini pia ni dharau kwa rais aliyeunda kamati hiyo.

Kwa mtu mstaarabu na msomi ingetosha tu kusema ripoti ya Profesa Mruma haina ukweli, au haina mashiko, au si ushahidi mzuri, n.k. Kuiita takataka si tu ni uhuni, bali pia ni kudhihirisha kiwango cha hila na chuki aliyonayo kwa kile alichofanya rais.

Wakati mwingine waweza kuwa na hoja nzuri, lakini ukaiharibu kwa lugha. Lazima ifike hatua tujue kuwa staha katika kukosoa ni sehemu ya msingi katika misingi inayojenga demokrasia.

Niseme tu kuwa si kweli hata kidogo kuwa ripoti ya Profesa Mruma haina maana kiushahidi. Ripoti hiyo ni ushahidi muhimu sana tena sana kuthibitisha udanganyifu wa Acacia. Kama leo kesi ya udanganyifu inasimama, ni ripoti ya kisayansi kama ya Mruma itakayotumika kuthibitisha uwepo wa udanyifu.

Lakini pia sisi huo ndio ushahidi wetu tuliokusanya, na wao kama wanao ushahidi mwingine unaosema hawajadanganya, basi watauleta- shida iko wapi? Iko wapi haja ya kuiita kamati iliyopata mamlaka ya rais takataka –‘rubbish’? Hakuna kabisa.

Je, tunayo matatizo ya sheria na mikataba kama wanavyodai?

Ndio tunayo. Yako mara mbili. Kwanza, sheria kama sheria kwa maana ya maudhui. Pili, sheria kwa maana ya usimamizi wake. Sheria kwa maana ya maudhui, yako maeneo yanayohitaji marekebisho na siyo sheria nzima.

Sheria hiyo ya Madini namba 14/2010 inaweza kurekebishwa maeneo yanayohusu leseni za madini, haki za kumiliki madini na ardhi yake, mrahaba na kodi na ile sehemu ya 10 inayoongelea adhabu, nk. Huo ni upande wa maudhui.

Kuhusu sheria upande wa usimamizi. Tatizo la usimamizi wa sheria ni kubwa kuliko upungufu ulio katika sheria yenyewe (maudhui). Kwa mfano, hii sheria iliyopo tunayosema ina upungufu, hakuna popote inaposema tuibiwe hata hicho kidogo tunachotakiwa kupata. Lakini tunaibiwa. Tatizo ni nini kama si usimamizi?

Hata tukitunga hiyo sheria mpya na kila mtu akaikubali, kama hatuna mtu wa kuisimamia ni kazi bure. Kwa hiyo tunahitaji mtu wa kusimamia sheria kuliko tunavyohitaji sheria yenyewe. Na dalili zote zinaonyesha kuwa mtu huyo tayari tumempata na sasa tunaanza kuondokana na tatizo hili. Mikataba nayo halikadhalika inahitaji kupitiwa kimaudhui pia ipate msimamizi.

Tatizo la akina Lissu katika hili ni kutaka kutwambia kuwa kwa kuwa tuna matatizo ya sheria na mikataba, basi haturuhisiwi kuzuia na kudhibiti hata wizi ambao tumebahatika kuugundua na kuuona. Ni upotofu na bila shaka ni hapana. Wizi huu tunaushughulikia na hayo mengine ya sheria na mikataba nayo muda unakuja yatashughulikiwa.

Kitendo cha rais kuunda kamati ya pili ya wachumi na wanasheria ni ushahidi kuwa tayari tatizo la sheria na mikataba limeanza kumulikwa rasmi.

Je, mchanga kuhakikiwa na TMAA kunafuta udanganyifu wao?

Lissu anasema kuwa mchanga huo ulihakikiwa na TRA, TMAA, n.k na kuwa zote hizi ni taasisi za Serikali na hivyo kuwaambia tena wameiba ni kuwakosea. Hivi kwani tunaposema kosa la ACACIA ni kutufanyia udanganyifu maana yake nini?

Maana yake si ni kwamba waliidanganya Serikali? Na Serikali si ni TRA, TMAA, nk? Sasa maajabu yako wapi? Kosa la ACACIA ni hilo kuzidanganya hizo mamlaka za Serikali wakati wa ukaguzi.

Kwa hiyo tunaposema wametuibia maana yake walizidanganya mamlaka hizo. Sisi hatujui walitumia njia gani, iwe rushwa au vinginevyo- sisi hatujui. Tunachojua ni kwamba tulichokuta wanachukua ni tofauti na kile walichosema wamechukua; jambo ambalo ni kosa. Iko wapi hoja hapo?

Mwisho ni kuwa tuache kupinga na kulalamikia kila kitu. Hili hatutaacha kulisema hata zipite karne 100. Madhali linaendelea kuwepo, tutaendelea kulikemea. Pia kurejearejea historia mara mwaka 1998 tulishauri hivi, mara vile nk. haina nafasi wala msaada kwa sasa.

Tumeshampata mtu wa kutushika mkono. Kazi yetu ni moja tu- kuungana naye kwa kuchangia utaalamu ili tutoke hapa tulipo. Kama huna utaalamu hata kumpa moyo nao ni mchango. Kama yote huwezi ni heri kukaa kimya kuliko ukabwabwaja.

Maajabu ni kutumia miaka zaidi ya 18 ukilalamikia jambo, halafu akatokea mtu wa kulitatua jambo hilo, badala ya kushirikiana naye, wewe ukafungua tena mlango mwingine wa malalamiko kulalamikia tena kile kile ulichopigania kishughulikiwe. Ni maajabu yanayostahili kuingia kwenye maajabu ya dunia!

Mwandishi wa makala hii, Bashir Yakub, kitaaluma ni mwanasheria. Anapatikana kupitia namba 0784482959
 
Ombudsman

JF-Expert Member
Apr 18, 2012
3,574

Maneno Mengii, Nilichosema, Sawa Andamaneni hata mkitaka kutembea na Kumfuata Kama mpiga filimbi wa Hamelin, Mkamfuata mpaka mkatumbukia vilindi vya Indian Ocean, sawa who will miss you! Seriously? Ila nachoshangaa kwanini ninyi mnaoandamana kumpongeza Magufuli kwa political stunts mruhusiwe lakini maandamano au Mikutano ya kumlaani kwa mabaya yake inapigwa marufuku?
Is that too much fairness to ask? Nijibu mimi nilichosema Kama ni Lissu mtafute kwa Wakati wako. I am TL. Marandu not TLissu!
 
monomotapa

JF-Expert Member
Oct 30, 2012
437
500
CHADEMA mtakuja na majaribio mengi ya kujenga chuki Nchi hii na hamtafanikiwa kamwe, bahati njema sana jamii inawaelewa vyema, mmesababisha mayatima wengi sana kwa sera zenu zisizofaa za vurugu, mnatumia migongo ya wananchi masikini kutaka kutokelezea kisiasa na kuleta tafrani katika jamii. Ila kwa awamu hii ya sasa na huyu Rais wa sasa mkajipange upya kabisaaaaaaaaa. Sidhani kama kuna mwananchi mjinga atakaye sikiliza upuuzi kama huu
 
Punainen

JF-Expert Member
Jul 19, 2013
1,159

Mkuu umeelewa mada? Ikiwa wanaomuunga mkono magufuli wana haki ya kuandamana, wasioridhishwa na baadhi ya anayoyafanya wana haki ya kuandamana au?
 
Uzi unaeleweka vyema sana, USHAURI kwa wasioridhishwa na utendaji wa Rais wanaweza kukaa majumbani mwao ama kufanya shughuri zao zingine za maendeleo, kuna shughuri nyingi sana za kufanya, hakuna maandamano yeyote duniani ambayo yanayoungwa mkono asilimia mia. Ila wazo lako la maandamano ya kumlaani sijaelewa unalaani nini??? Hayo maandamano yatahudhuriwa na nani hasa kwasasa? Labda vibaka, wezi, wapiga madili na wafuasi wa sembe kama bado wapo
 
tamuuuuu

JF-Expert Member
Mar 10, 2014
13,932
2,000
Tena yafanyike nchi nzima ya kulaani na kupinga ukiukwaji mkubwa wa sheria na utawala usiofuata katiba.

Ukiukwaji wa mikataba n.k
 
TL. Marandu

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
3,628
2,000
Uzi unaeleweka vyema sana, USHAURI kwa wasioridhishwa na utendaji wa Rais wanaweza kukaa majumbani mwao ama kufanya shughuri zao zingine za maendeleo, kuna shughuri nyingi sana za kufanya, hakuna maandamano yeyote duniani ambayo yanayoungwa mkono asilimia mia. Ila wazo lako la maandamano ya kumlaani sijaelewa unalaani nini??? Hayo maandamano yatahudhuriwa na nani hasa kwasasa? Labda vibaka, wezi, wapiga madili na wafuasi wa sembe kama bado wapo
Wewe ni Bashite bashite au? Nimeneglect mengi, Nikaweka sababu chache 7 za mambo mazito yafaayo alaaniwe hukuyaona?
 
mwanadome

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
4,086
2,000
SiasA za kijinga sana hizi,eti ukitaka kupongeza ruksa ila kukosoa marufuku!!.mkitoka hapo mmatulazimisha tuwaombee.

Jana ilikua imepangwa walemavu wafanye mkutano wa kumpongeza,mungu saidia mipango yao ikavurugwa na kipigo cha walemavu wenzao wa juzi kule posta.pamoja na posho walizo ahidiwa waliogopa kuoneka wasaliti kwa wenzao.

Isha semwa kua ukiona msomi mwenye Phd anaogopa kukosolewa/pingwa kwa hoja,basi yakupasa utilie shaka elimu yake.
 
Waziri kivuli

JF-Expert Member
Nov 30, 2016
2,989
2,000
Sijasikia ACACIA wakijitetea, bali namsikia Mtanzania mwenzetu Tundu Lissu katika maandishi na video zinazoenezwa mtandaoni kwa kasi ya ajabu akiwatetea kwa nguvu na kwa pumzi zake zote. Ni kuhusu mchanga wenye madini uliozuiwa na Serikali bandarini. Amezungumzia mambo ambayo nitayajibu hapa kwa lengo kubwa kabisa la kutaka Watanzania wafahamu.
Je, sheria inasema mchanga ni mali ya ACACIA?

Lissu anasema kuwa kwa mujibu wa sheria mchanga ule ni mali ya ACACIA na hivyo Serikali kuuzuia ni sawa na kuzuia mali ya mtu. Kuhusu hili sijui amezungumzia sheria ipi? Katika Sheria Namba 14/2010 Sheria ya Madini hakuna jambo la namna hii kama Tundu Lissu anavyotaka kuliweka.

Hakuna popote ilipoandikwa kuwa mchanga wote unaochimbwa ni mali ya ACACIA. Na hili linajulikana kwani hata leseni za uchimbaji hutolewa kwa ajili ya uchimbaji madini na siyo umiliki wa ardhi. Ardhi ambayo hujumuisha mchanga hubaki mali ya Taifa.

Lakini pia katika hilo hilo lazima ieleweke kuwa hawakuwa wakichukua mchanga kwa sababu ni mali yao kama Lissu anavyosema. Hata wao hilo wanalikataa. Wanasema wanalazimika kubeba mchanga kwa kuwa hapa Tanzania hakuna kiwanda/mtambo wa kuchenjua mchanga na kupata wanachokitaka. Hawasemi walikuwa wanachukua mchanga kwa sababu ni mali yao, hapana. Ni utetezi wa Watanzania wenzetu unaosema mchanga ni mali yao.

Je, Acacia wametenda kosa lolote?

Lissu na kundi lake wanawatetea ya kuwa hawajatenda kosa lolote. Ni hivi, ukweli ni kuwa kuna makubaliano maalumu kati ya Acacia na Serikali kuwaruhusu kuchukua mchanga kwenda kuuchenjua katika kipindi ambacho Serikali itakuwa haijajenga mtambo wake.

Hata hivyo, lazima ieleweke kuwa makubaliano haya yanakwenda sambamba na wajibu wa kisheria wa kutoa taarifa sahihi kuhusu uzito wa kile wanachochukua pamoja na sampuli zilizomo.

Kuthibitisha kuwa wajibu huu upo, ndio maana mchanga huo hukaguliwa, na wao hukubali ukaguliwe na TMAA, TRA, nk. Mchanga haukaguliwi ili kujifurahisha, hapana. Unakaguliwa ili kujua uzito na sampuli za kile kinachochukuliwa.

Basi, hatua ya wao kukubali kukaguliwa na mamlaka hizi kwa malengo haya ya kujua wanachukua nini inathibitisha hata wao kuutambua wajibu wao wa kusema ukweli kuhusu uzito na sampuli za kile wanachobeba.

Sasa swali ni kama wajibu huu upo na wao wanautambua kwa kiwango hiki; je, kuukiuka kwa kudanganya kuhusu uzito na sampuli ni kosa au si kosa? Akili ya kawaida tu ya mtu ambaye hata siyo mwanasheria itapata jibu. Halafu anatokea Mtanzania anasema hawajafanya kosa lolote.

Lakini pia ukidanganya kuhusu uzito na sampuli utatoa mrahaba ulio chini ya kiwango, chini ya kile ulichotakiwa kutoa. Bado baadhi ya Watanzania wenzetu wanasema hilo nalo si kosa! Inasikitisha sana.

Makala yaliyopita nilieleza kwa urefu kosa la udangayifu hapa kwetu na huko kwenye mahakama za kimataifa. Muda huu itoshe tu kusema kuwa, jamani udanganyifu ni kosa (fraud/deceitful).

Na ni kosa pote mahakama za ndani (local courts) na katika hizo za kimataifa (International Arbitral Tribunal). Na hakuna shaka imethibitika makosa haya wameyatenda. Haya iko wapi hiyo kesi inayopigiwa debe kwa nguvu zote kuwa lazima tunashindwa?

Je, ni kweli ripoti ya Mruma ni takataka kama inavyoitwa?

Lissu anaiita Ripoti ya Tume ya Mruma- takataka, na kusisitiza kwa Kiingereza kuwa ni ‘rubbish’. Kwanza niseme kuwa maneno haya ni ya dharau kubwa kwa Profesa Mruma na wasomi wote aliokuwa naye kwenye kamati. Lakini pia ni dharau kwa rais aliyeunda kamati hiyo.

Kwa mtu mstaarabu na msomi ingetosha tu kusema ripoti ya Profesa Mruma haina ukweli, au haina mashiko, au si ushahidi mzuri, n.k. Kuiita takataka si tu ni uhuni, bali pia ni kudhihirisha kiwango cha hila na chuki aliyonayo kwa kile alichofanya rais.

Wakati mwingine waweza kuwa na hoja nzuri, lakini ukaiharibu kwa lugha. Lazima ifike hatua tujue kuwa staha katika kukosoa ni sehemu ya msingi katika misingi inayojenga demokrasia.

Niseme tu kuwa si kweli hata kidogo kuwa ripoti ya Profesa Mruma haina maana kiushahidi. Ripoti hiyo ni ushahidi muhimu sana tena sana kuthibitisha udanganyifu wa Acacia. Kama leo kesi ya udanganyifu inasimama, ni ripoti ya kisayansi kama ya Mruma itakayotumika kuthibitisha uwepo wa udanyifu.

Lakini pia sisi huo ndio ushahidi wetu tuliokusanya, na wao kama wanao ushahidi mwingine unaosema hawajadanganya, basi watauleta- shida iko wapi? Iko wapi haja ya kuiita kamati iliyopata mamlaka ya rais takataka –‘rubbish’? Hakuna kabisa.

Je, tunayo matatizo ya sheria na mikataba kama wanavyodai?

Ndio tunayo. Yako mara mbili. Kwanza, sheria kama sheria kwa maana ya maudhui. Pili, sheria kwa maana ya usimamizi wake. Sheria kwa maana ya maudhui, yako maeneo yanayohitaji marekebisho na siyo sheria nzima.

Sheria hiyo ya Madini namba 14/2010 inaweza kurekebishwa maeneo yanayohusu leseni za madini, haki za kumiliki madini na ardhi yake, mrahaba na kodi na ile sehemu ya 10 inayoongelea adhabu, nk. Huo ni upande wa maudhui.

Kuhusu sheria upande wa usimamizi. Tatizo la usimamizi wa sheria ni kubwa kuliko upungufu ulio katika sheria yenyewe (maudhui). Kwa mfano, hii sheria iliyopo tunayosema ina upungufu, hakuna popote inaposema tuibiwe hata hicho kidogo tunachotakiwa kupata. Lakini tunaibiwa. Tatizo ni nini kama si usimamizi?

Hata tukitunga hiyo sheria mpya na kila mtu akaikubali, kama hatuna mtu wa kuisimamia ni kazi bure. Kwa hiyo tunahitaji mtu wa kusimamia sheria kuliko tunavyohitaji sheria yenyewe. Na dalili zote zinaonyesha kuwa mtu huyo tayari tumempata na sasa tunaanza kuondokana na tatizo hili. Mikataba nayo halikadhalika inahitaji kupitiwa kimaudhui pia ipate msimamizi.

Tatizo la akina Lissu katika hili ni kutaka kutwambia kuwa kwa kuwa tuna matatizo ya sheria na mikataba, basi haturuhisiwi kuzuia na kudhibiti hata wizi ambao tumebahatika kuugundua na kuuona. Ni upotofu na bila shaka ni hapana. Wizi huu tunaushughulikia na hayo mengine ya sheria na mikataba nayo muda unakuja yatashughulikiwa.

Kitendo cha rais kuunda kamati ya pili ya wachumi na wanasheria ni ushahidi kuwa tayari tatizo la sheria na mikataba limeanza kumulikwa rasmi.

Je, mchanga kuhakikiwa na TMAA kunafuta udanganyifu wao?

Lissu anasema kuwa mchanga huo ulihakikiwa na TRA, TMAA, n.k na kuwa zote hizi ni taasisi za Serikali na hivyo kuwaambia tena wameiba ni kuwakosea. Hivi kwani tunaposema kosa la ACACIA ni kutufanyia udanganyifu maana yake nini?

Maana yake si ni kwamba waliidanganya Serikali? Na Serikali si ni TRA, TMAA, nk? Sasa maajabu yako wapi? Kosa la ACACIA ni hilo kuzidanganya hizo mamlaka za Serikali wakati wa ukaguzi.

Kwa hiyo tunaposema wametuibia maana yake walizidanganya mamlaka hizo. Sisi hatujui walitumia njia gani, iwe rushwa au vinginevyo- sisi hatujui. Tunachojua ni kwamba tulichokuta wanachukua ni tofauti na kile walichosema wamechukua; jambo ambalo ni kosa. Iko wapi hoja hapo?

Mwisho ni kuwa tuache kupinga na kulalamikia kila kitu. Hili hatutaacha kulisema hata zipite karne 100. Madhali linaendelea kuwepo, tutaendelea kulikemea. Pia kurejearejea historia mara mwaka 1998 tulishauri hivi, mara vile nk. haina nafasi wala msaada kwa sasa.

Tumeshampata mtu wa kutushika mkono. Kazi yetu ni moja tu- kuungana naye kwa kuchangia utaalamu ili tutoke hapa tulipo. Kama huna utaalamu hata kumpa moyo nao ni mchango. Kama yote huwezi ni heri kukaa kimya kuliko ukabwabwaja.

Maajabu ni kutumia miaka zaidi ya 18 ukilalamikia jambo, halafu akatokea mtu wa kulitatua jambo hilo, badala ya kushirikiana naye, wewe ukafungua tena mlango mwingine wa malalamiko kulalamikia tena kile kile ulichopigania kishughulikiwe. Ni maajabu yanayostahili kuingia kwenye maajabu ya dunia!

Mwandishi wa makala hii, Bashir Yakub, kitaaluma ni mwanasheria. Anapatikana kupitia namba 0784482959
Nimesoma mpaka mwisho,nikajiuliza umepata ufahamu wapi wa kuandika kwa hoja namna hii?Daah nilipofika mwisho nikaelewa!Lumumba hamko timamu kujadili hoja!
 
Punainen

JF-Expert Member
Jul 19, 2013
1,159
2,000
Uzi unaeleweka vyema sana, USHAURI kwa wasioridhishwa na utendaji wa Rais wanaweza kukaa majumbani mwao ama kufanya shughuri zao zingine za maendeleo, kuna shughuri nyingi sana za kufanya, hakuna maandamano yeyote duniani ambayo yanayoungwa mkono asilimia mia. Ila wazo lako la maandamano ya kumlaani sijaelewa unalaani nini??? Hayo maandamano yatahudhuriwa na nani hasa kwasasa? Labda vibaka, wezi, wapiga madili na wafuasi wa sembe kama bado wapo
Mkuu ulicho quote hapo kimetaja kulaani? Hao wanaotaka kuandamana hawana shughuli za maendeleo?! Halafu mkuu, kama wewe siyo mwizi unafikiri utakuwa mwizi kwa sababu tu mimi nimekuita mwizi?!
 
TL. Marandu

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
3,628
2,000
CHADEMA mtakuja na majaribio mengi ya kujenga chuki Nchi hii na hamtafanikiwa kamwe, bahati njema sana jamii inawaelewa vyema, mmesababisha mayatima wengi sana kwa sera zenu zisizofaa za vurugu, mnatumia migongo ya wananchi masikini kutaka kutokelezea kisiasa na kuleta tafrani katika jamii. Ila kwa awamu hii ya sasa na huyu Rais wa sasa mkajipange upya kabisaaaaaaaaa. Sidhani kama kuna mwananchi mjinga atakaye sikiliza upuuzi kama huu
Nikuambie kitu? Wanaojenga Chuki, Wanakwapua Rambirambi, Wanaojenga chuki, Wanafukuza Wafoji vyeti maelfu, huku wakimbeba mwingine mbeleko, wanaojenga chuki Wanaharibu bustani za mboga zinazowapa ajira Wanakiji. Kwa sababu za Kisiasa, na kusingizi maji wanaojenga chuki, Wanauwa wananchi wasio na hatia ati wawataje wauaji kibiti. Hawa ndio wanaojenga chuki. The Hell Waliokwapua Ushindi wa Maalim Seif Zanzibar Wamejenga Nini? Just Shhhhut Up, Mnafiki mkubwa!
 
TL. Marandu

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
3,628
2,000
Mshangao wa mpumbavu haupewi attention na werevu!!!
Endelea kushangaa hivyo hivyo!!!
Yaani huoni aibu hata kuita Mtu mpumbavu, Let me tell you Ungeniita Mwerevu ningelia Literally maana ni mtu wa ajabu atapokea sifa za kichaa. Anayeshabikia CCM ni sawa na Nyoka mpuuzi anayejimeza Mwenyewe kuanzia Mkiani, digestion ikianza ndio anashtukia too late Anakufa unabaki je Umlilie au Umcheke

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom