Kama Luhanjo anpaswa kuwajibika kwa kumkingia kifua Jairo kwanini JK naye asiwajibike?

matongo manawa

JF-Expert Member
Apr 6, 2011
336
79
Wadau nimesikliza mjadala na michango ya wabunge ktk kamati
teule yabunge ya kumchunguza Jairo.Pamoja na mambo mengine
wabunge wameunga mkono Luhanjo kuwajibishwa.

Mh Zambi alikwenda mbali zaidi akisema alichokifanya Luhanjo
ni kulindana kwa sababu ya kufanya kazi na Jairo muda mrefu.
Sasa kama hiyo nikweli jeuri hiyo ya kukosa haya Luhanjo
aliipata wapi.

Tuwe wakweli Jk alikuwa hajui kuhusu maamuzi ya Luhanjo
mnataka kutuaminisha kuwa Luhanjo hakupewa maagizo na jk
na jk alipoona bunge limechachamaa akamtosa Luhanjo?naomba tuwe wakweli.
Kosa la Mh Raisi halina tofauti na la Ngeleja mana kam Raisi haakujua katibu
mkuu amechukua maamuzi hayo ni udhaifu wa hali ya juu.
Kwangu mimi hatuwezi kumtenganisha Luhanjo na Raisi,

Sijajua kwanini wabunge wanapindisha msitari,km jk hahusiki n basi ngeleja naye tutakuwa tunamuonea.

Naomba kuwasilisha.



 
Hoja imeungwa mkono. Luhanjo alisema alichotumwa na JK. Kumbuka maneno ya mh. James Lembeli;" RUSHWA IMEINGIA HADI IKULU". Tuliyemuweka ikulu ni JK siyo jairo,jairo ni mteule wa JK!
 
wote ni watoto watiifu wa jk, wanayofanya ni yale waliyoelekezwa na baba wa mji au waliyoona baba yao akiyafanya.
Wa kulaumiwa ni aliyewateua na ndiye anawapa kidume. Msanii number mmoja wa hayo yote.
 
Tusishangae Jairo na Luhanjo wasipoadhibiwa (kuwajibishwa) kinidhamu, maana hakuna shaka mkono wa wakuu wao ulikuwa pamoja nao. Sababu mojawapo ni kuwa Bunge halina ubavu wa kusimamia maazimio yake.

Nimesikiliza hitimisho la Makinda yaani basi; Eti "....serikali iangalie namna ya kufanya maana mambo mengine yako wazi sasa....". Pathetic.
 
.......si ndio wamemrundikia madaraka, muacheni, JK ametumia katiba kumsafisha jairo kupitia Luhanjo na CAG...
 
chadema mmemtafuta JK muda mrefu awajibike kwa kila kosa la mtu wa chini imeshindikana mtalalamika hadi 2015 ni parefu
 
kama ingekuwa kulinda kwani spika ni wa chadema? ni wa CCM mnadhani angeshindwa kumlinda Rais? tuache chiki binafsi. waliosimama kidete kummaliza Jairo, Luhanjo na kundi lake ni wabunge wa CCM kama wasingekuwa na nia ya dhati tangu awali wangeweza kukaa kama CCM na kulindana
 
mambo mengine kuropoka tu ili uonekane umeanzisha mjadala, Naibu spika Job Ndugai ni wa CCM, mkuu wa shughuli za serikali bungeni, Pinda ni wa ccm wote hawa wangeshindwaje kumlinda Rais na kuzuia kuundwa kwa kamati kama hayakuwa maagizo ya Rais kwamba endeleeni
 
tuache siasa jamani wakati mwingine wabunge wa ccm wakifanya kitu kizuri tuwaunge mkono kwani ndio wengi bungeni suala hili limetoka ndani ya serikali iliyoundwa na chama chao wangeweza kupindisha kwa maslahi yao lakini wamejari maslahi ya taifa kidudu mtu anakuja kuwakejeri
 
mama Beatrice shelukindo ni mbunge wa CCM ni mama jasiri sana akaiba barua ya siri ya Jairo na kuwasilisha bungeni na ndio matokeo haya lakini leo tunailaumu serikali ya JK kwa matokeo mabaya. nawasifu sana wabunge wa ccm kwa kusimamia haki
 
kwa hiyo unataka kusema Rais hawezi kudanganywa na wasaidizi wake wasio waaminifu? inawezekana alidanganywa na ndio maana akamsimamisha Jairo baada ya kurudishwa na Luhanjo na pengine kamati ya bunge imempa Rais majibu sahihi kutoka kwa wabunge baada ya kudanganywa awali
 
Back
Top Bottom