Kama Lowasa Atagombea Urais CCM 2015: Samuel Sitta Hama Chama. Gombea.

Ng'wanangwa

JF-Expert Member
Aug 28, 2010
10,827
4,172
Anza maandalizi sasa Mzee Chuma Cha Pua.

Take notes. Soma alama za nyakati.

Watanzania tunataka Rais asiye mlafi, asiye mbinafsi, asiye mwizi, asiye fisadi, asiye na laana ya Baba wa Taifa.
 
kama lowasa akiwa rais nchi itaingia kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe
 
Lowassa kupewa kamati ile si tiketi ya kupata urais 2015.Kumbuka hata Malecela amekaa na hiyo kamati kwa miaka 10 lakini kilichompata anakijua yeye mwenyewe.Lowassa urais basi
 
Lowassa kupewa kamati ile si tiketi ya kupata urais 2015.Kumbuka hata Malecela amekaa na hiyo kamati kwa miaka 10 lakini kilichompata anakijua yeye mwenyewe.Lowassa urais basi

malecela hana hela
 
Hivi bado Lowasa anafikiria urais kama rafiki yake JK mambo yalikuwa moto uchaguzi uliopita Lowasa atapata wapi kura za kumtosha kuwa rais na hata akichakachua ataleta fujo kama Ivory Cost
 
Hivi mnategemea nini kama zaidi ya nusu ya wabunge ni ama mambumbumbu au ni vibaraka wake akiwemo huyo mkuu wa huo Mhimili wa Bunge? Kwa kweli mapambano ya kung'oa mbegu hii yenye sumu kwa watanzania ni kubwa, ya kuchosha lakini tusiikatie tamaa. kuna siku Mungu atasikia kilio cha hawa maskini wanaonyonywa.
 
kama lowasa akiwa rais nchi itaingia kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe
Nchi imeshaingia kwenye machafuko tayari yako ndani ya roho za watu huko mnakosema (2015) hatuwezi kufika lazima tutashika mapanga tukatane. Kinachoonekana democrasia imenyimwa mkondo ndo maana hata kamati za bunge zimekuwa za kupeana. Dr Slaa kupata kura mil 2 amekuwa adui wa vyama vyote
 
Siyo Sitta tu, wapiganaji wengi tu kama Mwakyembe, etc wakiwa na nia ya dhati, wakaja upinzani....... CCM tunaizika bila kutumia nguuvu kubwa 2015...........
 
Nchi imeshaingia kwenye machafuko tayari yako ndani ya roho za watu huko mnakosema (2015) hatuwezi kufika lazima tutashika mapanga tukatane. Kinachoonekana democrasia imenyimwa mkondo ndo maana hata kamati za bunge zimekuwa za kupeana. Dr Slaa kupata kura mil 2 amekuwa adui wa vyama vyote

Kura milioni 2.5 za Dr. Slaa ni sawa sawa na Kura za Lipumba (1995+2000+2005+2010)
 
Kura milioni 2.5 za Dr. Slaa ni sawa sawa na Kura za Lipumba (1995+2000+2005+2010)

nimeipenda hii..imekaa vizuri
 
Lowasa akichukua tu fomu ya kugombea urais nchi inageuka Tunisia jioni yake. Najua ataingia kwa kujiamini kuwa jamaa wa Usalama wa Taifa watamfanyia kazi kama walivyoifanya kwa Mkwere, lakini atuonee huruma watanzania kwa nini tuuane wenyewe kwa wenyewe kati ya wanajeshi na wananchi kisa tu mtu mmoja atimize ndoto yake ya kuwa rais??? Please Lowasa huko uliko futa ndoto urais kwa maslahi nchi hii.
 
Anza maandalizi sasa Mzee Chuma Cha Pua.

Take notes. Soma alama za nyakati.

Watanzania tunataka Rais asiye mlafi, asiye mbinafsi, asiye mwizi, asiye fisadi, asiye na laana ya Baba wa Taifa.
sio atagombea yeye ndie chaguo la chama chake,kwahiyo be ready kwa mtifuano na sasa hivi anaongoza kamati ya usalama na nje kazi ipo kwa yule wa nje ambaye naye anataka kugombea
 
dr slaa hana tamaa atamwachia sitta. kwa vyovyote vile akigombea lowassa ccm chali
 
:laugh:Fisadi Lowassa tunakuomba utuachie nchi yetu imeshtunyonya vya kutosha, unachokitafuta sasa ni vita Fisadi Lowassa. ufisadi wote ulioufanya bado hujatosheka? Kama jeshi halitoilingilia kati basi naomba watanzania wenzangu tulivunjeni jeshi ufisadi wote unaofanyka katika hii nchi jeshi lipo kimya au nalo linafaidika na huu ufisadi wa kina Lowassa na wenzake? Fisadi Lowassa tunakusihii chondechonde baba unajipaka mafuta, na sisi tutakuwasha moto:twitch:
 
Sasa ngoja ninukuu hekima za baba wa Taifa Hayati mpendwa na kipenzi cha wengi Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mjukuu wa mzee Burito alisema hivi; " Kama mtu anatumia pesa zake ili kwenda ikulu basi atatumia hata RISASI ili kujisafishia njia akiwa Ikulu".

Kauli hii sasa inaanza kuleta maana kwa sisi Watanzania, mtu mbinafsi, fisadi, mbabe, mwenye visasi na ambaye yuko tayari hata kutoa uhai wake kwa mali ya dhuluma hafai kuwa rais wa Tanzania. Uamuzi wa rais ajaye wa Tanzania tunao sisi watanzania Wenyewe!.
 
Kamasi zinawatoka Wababe wa Egypt! Huyu Nunda wetu ni lazima tumche ngozi yenu akiwa Hai.

Mwizi na Jambazi Lowassa hastahili hata kuiota Ikulu
 
Sasa ngoja ninukuu hekima za baba wa Taifa Hayati mpendwa na kipenzi cha wengi Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mjukuu wa mzee Burito alisema hivi; " Kama mtu anatumia pesa zake ili kwenda ikulu basi atatumia hata RISASI ili kujisafishia njia akiwa Ikulu".

Kauli hii sasa inaanza kuleta maana kwa sisi Watanzania, mtu mbinafsi, fisadi, mbabe, mwenye visasi na ambaye yuko tayari hata kutoa uhai wake kwa mali ya dhuluma hafai kuwa rais wa Tanzania. Uamuzi wa rais ajaye wa Tanzania tunao sisi watanzania Wenyewe!.

Mzee wa viwango na spidi anza sasa kujiandaa Watanzania tuna Imani na wewe kwa maana mambo yanayotendeka sasa yanatukosesha Amani kabisa. Mzee Sitta soma nyakati ili uje kurekebisha Chama japo hata Mzee wa 120 bado busara na hekima zake pia zitatusaidia Wanzania.

ALUTA KONTINUA.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom