Kama kweli Wazanzibari "wengi" wanataka watoke kwenye Muungano mbona ni rahisi sana...

Kwa nini unafikiri swala la muungano na Zanzibar linatakiwa kupigiwa kura na Wazanzibari tu?

Hufikiri kwamba kuna uwezekanao Wazanzibari wengi wakasema wanataka kuwa katika muungano, ila watu wa bara wakawa hawataki muungano?

Ili kura ya maoni iwe na maana, inafaa ipigwe nchi nzima. Usichukulie for granted kwamba wabara wanautaka muungano.

Unaweza kumaliza kura ya maoni Zanzibar bila ya kuwashirikisha watu wa bara, ukapata kura za kukubali muungano nyingi sana, only to find out kuna malalamiko kutoka kwa watu wa bara kwamba hawakushirikishwa.

Hio ni ndoto, wazanzibari karibu 90% hawautaki muungano naitapotokea kupigiwa kura ya maoni mutaona.
 
Hio ni ndoto, wazanzibari karibu 90% hawautaki muungano naitapotokea kupigiwa kura ya maoni mutaona.
Haya tena, mara 'wengi' mara asilimia 90! sijui hizo statistic zinatoka wapi.
Wala humuhitaji kura ya maoni, mkiamua kwa dhati bila woga July1 2012 mtakuwa na Zanzibar yenye neema.
Mna bendera, wimbo wa taifa, BLW, katiba, Rais, baraza la mitihani, BPZ n.k mnahitaji nini ili muondoke?

Narudia, njia rahisi ni hii; Mkataeni Bilal kuwa si makamu wa Rais na Zbar haimtambui. Katazeni wabunge wasije Dodoma,
Wekeni Visa kwa wabara kuingia visiwani, acheni ajira za muungano na zote zitokanazo, wekeni ushuru kwa bidhaa kutoka bara, pelekeni mswada wa kujitoa ujadiliwe ndani ya BLW kama miswada mingine.
By July 1 2012 mtakuwa katika neema Zbar.

Kitu ambacho Watanganyika a.k.a machogo hawatakubali ni shirikisho la serikali tatu au mkataba. Tutapenda tuishi na ndugu zetu kama tunavyoishi na Wakenya au Waganda.

Labda niweke wazi kidogo kwanini mambo hayo hatutayakubali
Kwa vile wazanzibar 'wengi' au asilimia 90 hawautaki muungano ni dhahiri hakuna wanalofaidika nalo

1. Serikali ya shirikisho itasimamia kitu gani wakati asilimia 90 na 'wengi' wazanzibar hawana wanachofaidika nacho?
Serikali ya shirikisho itaendeshwajwe ikiwa wenzetu hawawezi kulipa hata deni la umeme?
Ni wazi serikali ya shirikisho ni kumbebesha mtanganyika mzigo kwa ujira wa matusi

2. Mkataba wa ushirikiano: swali linarudi pale pale, endapo wazanzibar asilimia 90 hawana faida na muungano, kuna jambo gani tunadhani linaweza kuwa la mkataba ambalo Bara na visiwani watafaidika kwa pamoja?
Tunachoelewa mkataba utahusu mambo ya ulinzi ambayo ni gharama kubwa. Utahusu ajira kwa wazanzibar huku bara, utahusu ardhi na uwekezaji, utahusu elimu ya juu n.k. sasa hapa Mtanganyika atafaidika na nini ?

Mambo haya yaliwezekana wakati tulipokuwa na maridhiano kama ndugu. Kwa vile wenzetu undugu hauna tija basi tukutane katika mahusiano kama EAC.
Ninachosema hapa zbar imefungua pandora box.

Harakisheni kabla ya July 1 2012 tutawaunga mkono! harakisheni muipate nchi yenu ya neema.
 
Wazanzibar waandae kura hiyo ya maoni wao wenyewe kama walivyofanya kwenye ile ya mabadiliko ya Katiba na lolote watakaloamua Tanzania Bara WATAHESHIMU uamuzi huo.

Mkubwa usitumbukie kule kule kwa Wazanzibari uliowasema kuwa "wanazungumza kana kwamba wanawakilisha mawazo ya wengi"

Maana hapo unazungumza kama unazungumza kwa niaba yaTanzania Bara nzima
 
Unaongelea Wazanzibari kama vile Muungano unawahusu wao tu. Wabara Jee?
 
2014? Naona ni mbali sana, labda ingekuwa December 2012 kila mtu ajue ustaarab wake.

Waliomba chama chao cha mpira, wakaweza kupata bila muungano
Wimbo wa Taifa, Bendera, na wakabadilisha katiba hata mambo yanayohusu muungano, hakuna anayewakataza

Ilikuwa ni kuamua tu, wabunge wao wasiende Dodoma, wajumbe wa tume wajitoe, Makamu wa Rais anayechaguliwa kwa kigezo cha Uzanzibar ajiuzulu, mawaziri wa muungano wajiuzulu, wafanyakazi katika taasisi za bara waache kazi.
By July 1 wangeshakuwa na Zanzibar ya neema! I wish they could pack and go ASAP

Kile kibutton cha like sijakiona ila naandika "like"

Waaache waende hata kama wakiamua kesho, lakini kwa haya wanayoyafanya kwa wabara wanaoishi Zanzibar, kuwachomea biashara, makani sana nk unadhani yataishia hapo?, ile roho ya ubaguzi itaendelea tu, kwa upande mwingine naona kunakua kama kuna mashinikizo na kukosa uelewa wa kile wanachokifanya na madhara yake baadae!

Naomba Mungu wabara tusiwe kama wenzetu wakishawishiwa hawapingi au hawajipi nafasi ya pili kufikiria, wao ni kutenda tu.

Mi ningeshauri uvunjike siku ile ile ambayo ulifanyika!!!
 
Unaongelea Wazanzibari kama vile Muungano unawahusu wao tu. Wabara Jee?

Watu wa bara hatujatoka na kutaka "kutoka kwenye Muungano" ni Wazanzibar ndio wanaotaka kutoka. Lakini historia yetu iko tofauti watu wa bara tangu uhuru tulielewa uafrika kama umoja wa Waafrika kwa asili ya taifa letu tunapenda Muungano (japo si watu wote). HIstoria yetu imejengwa kutoka kwenye Muungano...
 
Mkubwa usitumbukie kule kule kwa Wazanzibari uliowasema kuwa "wanazungumza kana kwamba wanawakilisha mawazo ya wengi"

Maana hapo unazungumza kama unazungumza kwa niaba yaTanzania Bara nzima

Ni kweli; lakini Wazanzibar wakiamua kutoka tutawalazimisha?
 
Haya tena, mara 'wengi' mara asilimia 90! sijui hizo statistic zinatoka wapi.
Wala humuhitaji kura ya maoni, mkiamua kwa dhati bila woga July1 2012 mtakuwa na Zanzibar yenye neema.
Mna bendera, wimbo wa taifa, BLW, katiba, Rais, baraza la mitihani, BPZ n.k mnahitaji nini ili muondoke?

Narudia, njia rahisi ni hii; Mkataeni Bilal kuwa si makamu wa Rais na Zbar haimtambui. Katazeni wabunge wasije Dodoma,
Wekeni Visa kwa wabara kuingia visiwani, acheni ajira za muungano na zote zitokanazo, wekeni ushuru kwa bidhaa kutoka bara, pelekeni mswada wa kujitoa ujadiliwe ndani ya BLW kama miswada mingine.
By July 1 2012 mtakuwa katika neema Zbar.

Kitu ambacho Watanganyika a.k.a machogo hawatakubali ni shirikisho la serikali tatu au mkataba. Tutapenda tuishi na ndugu zetu kama tunavyoishi na Wakenya au Waganda.

Labda niweke wazi kidogo kwanini mambo hayo hatutayakubali
Kwa vile wazanzibar 'wengi' au asilimia 90 hawautaki muungano ni dhahiri hakuna wanalofaidika nalo

1. Serikali ya shirikisho itasimamia kitu gani wakati asilimia 90 na 'wengi' wazanzibar hawana wanachofaidika nacho?
Serikali ya shirikisho itaendeshwajwe ikiwa wenzetu hawawezi kulipa hata deni la umeme?
Ni wazi serikali ya shirikisho ni kumbebesha mtanganyika mzigo kwa ujira wa matusi

2. Mkataba wa ushirikiano: swali linarudi pale pale, endapo wazanzibar asilimia 90 hawana faida na muungano, kuna jambo gani tunadhani linaweza kuwa la mkataba ambalo Bara na visiwani watafaidika kwa pamoja?
Tunachoelewa mkataba utahusu mambo ya ulinzi ambayo ni gharama kubwa. Utahusu ajira kwa wazanzibar huku bara, utahusu ardhi na uwekezaji, utahusu elimu ya juu n.k. sasa hapa Mtanganyika atafaidika na nini ?

Mambo haya yaliwezekana wakati tulipokuwa na maridhiano kama ndugu. Kwa vile wenzetu undugu hauna tija basi tukutane katika mahusiano kama EAC.
Ninachosema hapa zbar imefungua pandora box.

Harakisheni kabla ya July 1 2012 tutawaunga mkono! harakisheni muipate nchi yenu ya neema.
This is a radical solution in deed!
 
Wazanzibar inawezekana wakawa ni "muflisi" wa nini kifanyike ili kujitoa kwenye makucha ya Muungano!
 
Watu wa bara hatujatoka na kutaka "kutoka kwenye Muungano" ni Wazanzibar ndio wanaotaka kutoka. Lakini historia yetu iko tofauti watu wa bara tangu uhuru tulielewa uafrika kama umoja wa Waafrika kwa asili ya taifa letu tunapenda Muungano (japo si watu wote). HIstoria yetu imejengwa kutoka kwenye Muungano...

Unasema halafu unajichangana mwenyewe "japo si wote", Sasa na wa Zanzibari ni wote?

Historia ipi yetu inayotuonesha tunapenda Muungano? Nyerere ndiye aliyeshabikia Biafra ijitenge na Nigeria, Nyerere alihitilafiana na Nkurumah aliyetaka Afrika moja, Nyerere ndiye alivunja East African Community. Sasa hiyo ndio historia ya kupenda muungano?

Kwa Zanzibar nia siyo kuwa na Muungano ni a ni kuifanya Zanzibar iwe mkoa wa Tanzania, kama ilivyo mengine. Ni kitu hakiwezekani.

Njia moja ya kuuboresha muungano ni kuanza upya kuutazama kwa matakwa ya wengi na kwa kisheria zilizo wazi. Na sasa ni wakati muafaka tukielekea kwenye katiba mpya, si kama ulivyo sasa, Muungano wa kuburuzwa na Nyerere na Karume ambao haujafata wala hauna kanuni na sheria.

Simple solution:

1) Serikali ya Zanzibar, ambayo haitaingilia kabisa mambo ya Tanganyika.

2) Serikali ya Tanganyika ambayo haitaingilia kabisa mambo ya Zanzibar.

3) Serikali ya Muungano ambayo itakuwa inashughulikia mambo ya Muungano tu.
 
Inaonekana wewe ungepikia kura "a"; unautaka Muungano unataka mambo fulani yabadilishwe. Angalau umechagua upande.
 
Historia inaonyesha kuwa kuwalazimisha sio far fetched sana.

Jumbe alifanywa nini?

alifanywa nini ambacho Kambona hakufanywa? au Fundikira, au wengine waliotishia uwepo wa Jamhuri yetu. Angalau watu walijua jua kina kinaweza kufanyika.
 
alifanywa nini ambacho Kambona hakufanywa? au Fundikira, au wengine waliotishia uwepo wa Jamhuri yetu. Angalau watu walijua jua kina kinaweza kufanyika.

Basi usiulize kinachoweza kufanyiwa wanaodai kuvunjwa kwa Muungano, maana nao wataendelea kupachikwa "wanatishia uwepo wa Jamhuri yetu"
 
Inaonekana wewe ungepikia kura "a"; unautaka Muungano unataka mambo fulani yabadilishwe. Angalau umechagua upande.

Hakuna "a" wala "b" hapo, huo ni mfumo wa utatu. Unakusumbuwa? kama huuelewi utatu huwezi kuelewa nilichokiandika. 3 in 1.

Umekwepa ya uliyotaka kupotosha kuhusu historia.
 
This is a radical solution in deed!
Do you think so broda! I think it is the generous and fair solution. We can't tolerate UAMSHO xenophobia, discrimination, hatred and incessant name calling and abuse

I wish Zanzibarians could have their 'promised land' by July 1 2012.
They have an upper hand on union matter unlike their counterpart.
I will stand to support them 100%.

The willy nilly by UAMSHO is libertine and tedious leaving us with cession as mutatis mutandis.
My proposal is the civil solution with neither cost nor bloodshed.
Mnyisanzu, setting churches and people ablaze is the most radical solution one can imagine.

Tanganyikans need to forge ahead with other burning issues of national importance, discussing Zanzibar every other day will offer us nothing but frustration.
We have nothing to lose the least to say therefore it is time for them to pack and go!
I wish this could happen before July 1 2012.

My position on this topic is, let them go peacefully and we wish them all the best
 
aaaaaaah....
unadhani itaishia hapo??
sisi tutapiga kura nyingine kuomba COASTAL STRIP ya 16 miles tujiunge na new ZANZIBAR REPUBLICS....
ina maana miji yaTANGA, MTWARA, BAGAMOYO NA DSM....tutajiunga mso tuuu

HAPO ITAKUWA NCHI IMETENGAMAA, kama sudan , waislam na bara ya wakristu...

JE MZEE MWANAKIJIJI KUNA K2 UMEJIFUNZA HAPA?????
 
kuna maneno na kauli za baadhi ya watu wachache wakizungumza kana kwamba wanawakilisha "wengi". Utasikia mtu anayepinga muungano anasema "wazanzibari hatuutaki muungano" na wakati mwingine kudai "wazanzibari wengi hawautaki muungano". Sasa mara nyingi wanaposema "wengi" mtu wa kawaida (asiyetaka kufikiri sana) anaweza kuamini kabisa kuwa ni kweli "wengi" hawautaki muungano.

Mfano unaotolewa siku za hivi karibuni ni "sahihi 500,000" za wanaodaiwa "wazanzibari" wasiotaka muungano. Sasa kwenye mahali ambapo pana watu milioni 1.5 hivi idadi hiyo ni kubwa sana; ni theluthi moja ya watu wote wa zanzibar. Sasa kama kweli wapo watu wengi hivi njia rahisi ya kutaka kujitoa kutoka kwenye muungano siyo mihadhara wala hawahitaji kabisa kuwalalamikia watu wa bara au serikali ya muungano.

Kwa wanaokumbuka wananchi wa zanzibar walishinikiza vyama vyao viwili vya ccm na cuf kuunda serikali ya umoja wa kitaifa na waliweza kufanya hivyo baada ya kupitisha sheria ya kura ya maoni ambayo hatimaye iliandika upya katiba ya zanzibar. Wananchi wakaweza kujitokeza na kupiga kura ya maoni. Walifanya hivi bila kuomba kibali muungano na kiasi cha kuweza kuandika kwenye katiba yao vitu ambavyo ni kinyume na katiba ya muungano.

Sasa kama waliweza kufanya hili ni kitu gani kinawashinda kutaka viongozi wao wa kisiasa kuandia sheria ya kupiga kura ya maoni kama wanautaka muungano au la? Kwa vile hoja ya kupinga muungano inadaiwa inakubaliwa na watu wa vyama vyote ni wazi kuwa ni rahisi sana kwa watu wa uamsho na wazanzibari wengine kuhakikisha kuwa blw linapokaa linaazimia kupitisha kura ya maoni kuhusu muungano na kutaka sheria iletwe ya kuuliza swali la muungano.

Swali liwe rahisi tu:

je unataka zanzibar ibakie kwenye muungano wa jamhuri ya muungano wa tanzania?

A. Ndio ibakie - ikibakia kero na matatizo ya muungano kutatuliwa ifikapo julai 1, 2014
b. Hapana isibakie - isipobakia zanzibar itajitoa ifikapo julai 1, 2014

ijulikane mapema kuwa ikisemwa kuwa "ndio ibakie" manake ni kuwa masuala ya muundo na mfumo wa muungano yatajadiiliwa na kushughulikiwa kwenye katiba mpya na yatakuwa tayari kumalizwa yote ifikapo 2014

na ikisemwa hapana isibakie manae ni kuwa mazungumzo ya kuvunja muungano yataanza na ifikapo julai 1, 2014 zanzibar itajitoa kwenye muungano.

Wazanzibar waandae kura hiyo ya maoni wao wenyewe kama walivyofanya kwenye ile ya mabadiliko ya katiba na lolote watakaloamua tanzania bara wataheshimu uamuzi huo.

Ni rahisi sana kumaliza hoja ya muungano au kutokuwepo muungano. Yote yamo mikononi mwa wazanzibari. Hawahitaji kutuambia hawautaki muungano, hatuhitaji watuambie tunawakandamiza kama wanataka kutoka kweli na siyo mikwara mbuzi njia nyeupeeeee!!! Andikeni sheria, itisheni kura ya maoni, pigeni kuchagua 'b' and then mambo yatakua yameiva ifikapo 2014 tutawasaidia kufunga mizigo.

mwanakijiji sijui hata kama unaweza tena kula na kulala vizuri . Akili yako imeshapata ugonjwa wa uzanzibari,

kila siku mara magazetini zanzibari hivi zanzibari vile , humu jf ndio huondoki kwenye keyboard unawaza zanzibari

hivi kitu gani kinakufanya upate ugonjwa huu????

Kama kweli wewe na wenzako munazo hoja madhubuti kuhusu muungano ,kitu gani kinawashinda kutumia haki yako/yenu ya kikatiba kutayarisha muhadhara iwe tanganyika au zanzibari kutoa hoja zako/zenu .

Kumbuka si watu wote wanaubavu wa kununua gazeti au kuingia kwenye internet

wengi ni walalahoi ambao mtu hufikiria mlo wake wa siku kwanza

au kama mnao ubavu waiteni muamsho mufanye mdahalo nao msikimbilie kwenye magazeti na internet tu
 
Katika mgawo wa vitu, tutagawanaje JWTZ? Wlau Sudan ya kusini walikuwa na jeshi lao la ukombozi. Nadhani Wazanzibari wanatakiwa wawe na utulivu ili busara itawale. Maoni yangu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom