Kama kweli wabunge wa CCM ni wazelendo kwa hili muungeni mkono Zitto

Ukiongeza na
20. Sakaya
21. Sita
22. Mwakyembe
23. Mwandosya.
70 zimefika jamani, VoNoCo itapigwa hatimae.
Tatizo ni kupata kura za nusu ya wabunge ili kumpiga chini PM.
 
Ni vile wabunge wa ccm wametawaliwa na unafiki otherwise ilikuwa wakati sahihi kuondokana na Pinda as PM. mtu gani hana hata meno,hang'ati?
 
Zitto amewashika pabaya ccm kwani wale wote walioongea kwa hasira ndio tunataka tuone kama watasaini au vp,na isipofika 70,maana yake Zambi,Kansi kaskazini,Serukamba,Bulaya na wengine watakuwa wamewandanganya umma wa watanzania kwa kauli zao.
 
Wabunge wa CUF wote je? Au wataungana na wabunge wa chama cha magamba A? make wako 34. kwa hiyo if 34+48=82
 
Huu pia ni mtihani kwa Wabunge wa CUF. Ili kufuta dhana ya kuwa wao ni CCM B inabidi waweke sahihi la sivyo hata wale wenye uchungu na nchi hii walio Pemba wataona hawana wabunge. Sidhani kama Wapemba wengi wanapenda hii ndoa yao na CCM
 
Zile kelele za wabunge wa CCM kwenye uchangiaji wa taarifa za kamati kumbe ulikuwa unafiki mkubwa baada ya mkakati mzito kusukwa juu ya namna ya kumwokoa mh Pinda kutompigia kura ya kutokuwa na imani naye.

Taarifa za kiintelijensia ambazo zimepatikana kutoka Dodoma zinaeleza kuwa wabunge wa chama tawala wanaona kuwa hilo litakuwa jambo la fedheha na hivo wanahaha kuitisha kikao cha kamati ya chama ya wabunge wa CCM ili kuweka mambo sawa. Hata hivyo taarifa za baadhi ya wabunge zinaonyesha kuwa Waziri mkuu Pinda amekuwa mpole na anafanyakazi kwa dhana ya bora liende ili muda wake uishe. Kwa vyovyote iwavyo bado mh Zito ameonyesha ukomavu na ataingia katika historia mpya na hili pamoja na kuwa litazimwa lakini ni kifo cha taratibu cha CCM kwani taarifa zaidi zinaonyesha kuwa wabunge wengi wa CCM wameamua kuwa liwalo na liwe na ikibidi watahama chama na ili kujijenga zaidi kisiasa hata wakihamia Chadema watakuwa wamejijenga kisiasa kwa kuibomoa na kuikosoa waziwazi Serikali kuitikia matakwa ya wananchi. Mfano hai ni Godrey Zambi.

My take: ngoja tusubiri tuone hata hivyo ni aibu kwa serikali na makubwa ni kesho kamati ya nishati na madini yote yataweza kumpindua kabisa Pinda mtoto wa mkulima

Magamba bwana wanatishia kubreakwind wanaishia kuharisha!
 
Yalioendelea jana na leo kwa aliyesikiliza anaweza kuona kuwa mfa maji haachi kutapatapa.Kwani hao ccm hawayajui hayo kama riport ya CAG tangu 2oo7/2008 ni hiyohiyo,leo ndio wanaona mwezi? Mimi nawaomba mbowe na Dr slaa mtu,Diwani,MBUNGE akihamia chadema aje na awe mwanachama.Chadema ina vijana sasa wakutosha.Hatutaki mabo ya shibuda tena yajirudie.
 
Mkuu mtoa mada hivi kwa hali iliyotokea leo pale mjengoni unadhani Filikunjombe na Zambi bado wapo CCM?

Mh diwani,
fili na zambi wamekuwa mzigo kwa chama chako, lakini mkisema muwaondoe kwenye chama chenu watakwenda upinzani halafu watarudi bungeni 100% kupitia cdm na mjue hawa watu ni type ya Dr P. W Slaa, Pole sana muheshimiwa diwani kwa kweli chama chenu kinapitia wakati mgumu sana.
 
Huu pia ni mtihani kwa Wabunge wa CUF. Ili kufuta dhana ya kuwa wao ni CCM B inabidi waweke sahihi la sivyo hata wale wenye uchungu na nchi hii walio Pemba wataona hawana wabunge. Sidhani kama Wapemba wengi wanapenda hii ndoa yao na CCM


hii ndoa ya cuf na ccm sidhani kama wana-cuf wanaiunga mkono, hio ilifosiwa na viongozi fulani fulani wa cuf kutokana na uroho wa madaraka. Yaani wameingia ndoa wakati hao viongozi ndo walisababisha hadi wanachama kibao wakafa wakati ule wa machafuko huku hao wakikimbiza roho zao.

Kwanza mimi huwa sipendi kuita hii ni ndoa, ktk hili suala naona kama vile cuf wamebakwa na ccm na hatimaye wakaozeshwa ndoa ya mkeka.
 
maisha lazima yaendele watanzania tumechoka sasa japo muongozo ulitakiwa pia umuendee baba mwanaasha
 
Mkuu Zitto pongezi nyingi sana kwa kutuwakilisha wananchi na huu ndio Upinzani mkuu wangu. Siku zote hao jamaa walijaribu sana kukuvuta, wakupake hadi uonekane hufai hata kwa kulumangia.. Sasa wanakiona cha moto, nakupongeza sana na chama CDM kusimama kiume ktk hili..Wananchi wamechoka! wamechoka! wamechoka!
 
Mmmh, mbona kuna mtu yupo Dodoma kaniambia kwamba Pinda ameamua kuresign kabla hajapigiwa kura? Sasa huyo anayemlinda ni nani? Labda akataliwe na Kikwete, lakini mpashaji wangu anasema hata wakati wa sakata la Jairo Pinda alitaka kujitoa maana anaona huo mzigo wa Uwaziri mkuu umemlemea.
 
Wanajamvi wenzangu, kwavyovyote vile inahitajika sahihi kadhaa kutimiza hizo 70. Na hao watakaosaini tutawakubali kuwa ndiyo wazalendo. Sasa napenda kuwauliza swali wana-JF wenzangu, hivi Lowasa akichangia sahihi mtamuweka kundi gani? Atasameheka?? Ninawasiwasi wale watuhumiwa wanaweza changia sahihi ili kujiosha/kutubu. TAFAKARI
 
Back
Top Bottom