Kama kweli wabunge wa CCM ni wazelendo kwa hili muungeni mkono Zitto

Kupata kura 70 si kazi kwani kwa hesabu zet tayri kuna kura 48, kazi ipo kwenye kupata kura 22.
CCM hata wasipotoa kura hizi bado wabunge wengine wa upinzani (CUF,UDP, TLP na NCCR wanazidi idani hiyo. Sasa issue ni mkakati wa kuwashawishi hao kwani kambi ya Upinzani haina ushirikiano.

Cha msingi ni wananchi kuwashinikiza wabunge wao kupitia njia za mawasiliano zilizopo, na wapigakura wake wafuatilie kuona kama aliwasikiliza kwani watakaounga hoja hii Mkono tutawajua kwa majina.
Tatizo nilionalo mimi ni ile 51% ya kura kama hoja ikipitishwa. Hata hivyo wakulaumiwa ni watanzania, kwani wao ndio waliowachagua wabunge wengi wa CCM, na hili litakuwa ni fundisho tosha

good analysis mkuu! But kwenye wabunge wa CDM sio kura 48 bali kuna kura 47 kwani kumbuka kuna yule mchumia tumbo SHIBUDA ambaye huwa haeleweki ni chama gani.
 
kwa ninavyo ona mh Zitto amewashika pabaya ccm.. Ama wamue kumtoa kafara wazir mkuu au waonekane wanafik mbele ya jamii ili waache kelele bungeni
 
ivi nyie mnajua adhabu ya uhaini??nyie mpeni kichwa tu uyo zitto mtamponza.
Siku hizi mama sisi hatutishiki tena, ok tafuta kamusi ya kiswahili saka neno UHAINI ujue maana yake acha kukurupuka tu na kuwatisha makamanda, tupo makini sana MAKAMANDA
 
Huwajui wabunge wa CCM!!! Tatizo watamzamia tunaugua ugonjwa wa kusahau au tuna vichwa vya panzi. Zito atashangaa anapata za chadema, ya kafurila na CUF hatapata ata moja. Ataishia kati ya 56 tu. Wabunge wa CCM ni nyoka.
 
Kwa jinsi mambo yanavyoenda, Sisiemu itakuwa chama cha upinzani siku sio nyngi kwa hiyari bila hata kumwaga damu na bila vurugu ya namna yoyote... tusubili tuone!!! Nature will take place.
 
wasaini ama wasisaini lakini watanzania tumeshajua kwamba pinda yuko likizo na wabunge wa ccm wajue tunawasubili kwa hamu ili tuwaadhibu kwa unafiki wao. mwl nyerere alisema ccm si mama yangu wao hawaoni kama ccm imeshapoteza mwelekeo. hongera kijana zitto zuberi kabwe, hongera makamanda wote wa chadema, mungu awalinde.
 
Mkuu mtoa mada hivi kwa hali iliyotokea leo pale mjengoni unadhani Filikunjombe na Zambi bado wapo CCM?
 
Kweli forum siku hizi imevamiwa na watoto
Wa facebook. Hakuna hoja katika kujibu au
Kujadili hoja. Wengi humu siku hizi ni watu wasio makini
Katika kujikita katika michango iliyozoeleka
Hapa jamvini. Hoja ni nyepesi, michango
Haina mashiko utoto umetawala katika issue
Sensitive kwa Taifa. Nia aibu kujiita great thinkers kwa kweli kama hali ndio hii.
Naomba kuwasilisha

na wewe deal na hoja husika, achana na makablasha ya kwenye "shimo la taka". Siku hizi uchafu unaachwa ili uoze ili hali haukugusi.
 
Siku hizi mama sisi hatutishiki tena, ok tafuta kamusi ya kiswahili saka neno UHAINI ujue maana yake acha kukurupuka tu na kuwatisha makamanda, tupo makini sana MAKAMANDA

hamna kutishana mkuu,ila mtu anayefanya kampeni ya kuipindua serikali na rais wake sio wa kumwacha anataka kuleta vita..
 
wabunge wa ccm walishapanga kuyafanya aliyosema zito, ref: mbunge wa kig mjini, zambi, lusinde asubuhi tbc na jembe filikunjombe
 
Baada ya mh. Zitto kutoa azimio la wabunge kutia sahii kwa ajili kutokuwa na imani na PM, ndugu waJF tujua fika wabunge wa chadema wote 49 watatia sahihi zao. Je kuna wabunge gani tunaona kuwa huenda nao wakafanya hivyo.?
Tuwataje kwa majina na chama wanachotoka.
1. Magedelena Sakaya (cuf).
2. Godfrey Zambi (ccm).
3. Samuel Sitta (ccm)
4. Harison Mwakyembe(ccm) 5. Agustino Mrema (TLP).
6........
7.........
8....
 
Ikifika kesho Mawaziri wa Wizara zilizolalamikiwa Bungeni wasipojiuzulu kwa uwajibikaji na Wabunge tuliowachagua wasipoweka signature zao kumwajibisha Waziri Mkuu kwa kushindwa kuwashinikiza mawaziri hao kuwajibika. Wabunge tuliowapeleka pale tuwakihoji kwanini wamekuwa wanapigia kelele kutuhadaa? wakati uwezo wanao?

Hili si la kusubili, Watanzania wote tumwunge mkono Zito, kila jimbo kesho likaombe kibali cha maandamno kuwashiniza wabunge.jpili tuingie barabarani.
 
Wabunge wa Chadema ni 48 baada ya Lema kutoka. Hata hivyo sidhani kama wote wapo Dodoma.
Sina hakika na wabunge wa CCM kama wataweza kuweka sign zao ila natambua wale wanaofuata mrengo wa Ki-lowassa wanaweza kuweka sign zao.
Hao ni 1. Peter Serukamba
2. Andrew Chenge
3. Abood wa Morogoro
4. Shellukindo
5. Nyangwine
6. Shekifu
7. January
na wengineo
 
waziri wa afya na naibu wake,pamoja na watu kufa mgomo wa madaktari

wapo tele kwenye nyumba walokarabati kwa milioni 480,sembuse complain za bungeni
 
8. Zambi
9. Bulaya
10. Pindi Chana
11. James Lembeli
12. Filikunjombe
13. Cheyo
14. Hamad Rashid
15. Mkosamali
16. Machali
17. Agripina
18. Kafulila
19. Kange Lugora
Bado wa3 tu 70 ifike.
 
Back
Top Bottom