Kama kweli wabunge wa CCM ni wazelendo kwa hili muungeni mkono Zitto

EJM_

JF-Expert Member
Jul 8, 2011
3,836
2,090
Wakati akihitimisha mjadala wa taarifa ya kamati mbalimbali hasa za Serikali za mitaa, mashirika ya umma na ile ya wakubwa, Mwenyekiti wa kamati ya serikali za mitaa Mh. Zitto Zuberi Kabwe ametoa pendekezo la kupiga kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu kama njia ya kuwawajibisha mawaziri ambao wamekuwa wakipatikana na makosa mbalimbali lakini hawachukuliwi hatua.

Mh. Zitto amesema kwakuwa mamlaka ya kuteua na kuwaondoa mawaziri ni ya rais pekee, na kwakuwa wao kama bunge hawana mamlaka yoyote juu yaom basi wao watumie rungu waalilonalo ambalo ni kumwajibisha waziri mkuu ambapo kwa kufanya hivyo wataanza kwa kukusanya sahihi za wabunge 70 ili kufikisha idadi ya wabunge wanaotosha kuunda hoja ya kupigwa kwa kura hiyo kwa mujibu wa kanuni na zaidi ya asilimia 50 ya kura kumwondoa waziri mkuu.

Kwa mtazamo wangu nadhani kumekuwa na kubebana kwa kiasi kikubwa kwa mawaziri na nashauri kama kweli wabunge wa CCM wana machungu na wanachi wanaowawakilisha, kama kweli wana mapenzi ya kweli kwa nchi hii na chama chao, basi waungane mkono na hili kwa moyo mmoja ili tuweze kuendelea kama nchi.
 
Zile kelele za wabunge wa CCM kwenye uchangiaji wa taarifa za kamati kumbe ulikuwa unafiki mkubwa baada ya mkakati mzito kusukwa juu ya namna ya kumwokoa mh Pinda kutompigia kura ya kutokuwa na imani naye.

Taarifa za kiintelijensia ambazo zimepatikana kutoka Dodoma zinaeleza kuwa wabunge wa chama tawala wanaona kuwa hilo litakuwa jambo la fedheha na hivo wanahaha kuitisha kikao cha kamati ya chama ya wabunge wa CCM ili kuweka mambo sawa. Hata hivyo taarifa za baadhi ya wabunge zinaonyesha kuwa Waziri mkuu Pinda amekuwa mpole na anafanyakazi kwa dhana ya bora liende ili muda wake uishe. Kwa vyovyote iwavyo bado mh Zito ameonyesha ukomavu na ataingia katika historia mpya na hili pamoja na kuwa litazimwa lakini ni kifo cha taratibu cha CCM kwani taarifa zaidi zinaonyesha kuwa wabunge wengi wa CCM wameamua kuwa liwalo na liwe na ikibidi watahama chama na ili kujijenga zaidi kisiasa hata wakihamia Chadema watakuwa wamejijenga kisiasa kwa kuibomoa na kuikosoa waziwazi Serikali kuitikia matakwa ya wananchi. Mfano hai ni Godrey Zambi.

My take: ngoja tusubiri tuone hata hivyo ni aibu kwa serikali na makubwa ni kesho kamati ya nishati na madini yote yataweza kumpindua kabisa Pinda mtoto wa mkulima
 
Kupata kura 70 si kazi kwani kwa hesabu zet tayri kuna kura 48, kazi ipo kwenye kupata kura 22.
CCM hata wasipotoa kura hizi bado wabunge wengine wa upinzani (CUF,UDP, TLP na NCCR wanazidi idani hiyo. Sasa issue ni mkakati wa kuwashawishi hao kwani kambi ya Upinzani haina ushirikiano.

Cha msingi ni wananchi kuwashinikiza wabunge wao kupitia njia za mawasiliano zilizopo, na wapigakura wake wafuatilie kuona kama aliwasikiliza kwani watakaounga hoja hii Mkono tutawajua kwa majina.
Tatizo nilionalo mimi ni ile 51% ya kura kama hoja ikipitishwa. Hata hivyo wakulaumiwa ni watanzania, kwani wao ndio waliowachagua wabunge wengi wa CCM, na hili litakuwa ni fundisho tosha
 
Kulindana kunalimaliza taifa! Yaani nchi itakwisha sisi tunalindana! Kweli sisi ni watu au wanyama?
 
Wasipomwajibisha waziri mkuu itakuwa mtaji mkubwa wa M4C!
Lema atajiongezea la kuwaambia wananchi jinsi ccm walivyowanafiki, kwamba hawana lengo la kuwakomboa watanzania, na kwamba kelele zao ni za kuwahadaa watanzania
 
Wamnyime kura Zitto lakini wananchi 2015 ndiyo watakuwa waamuzi wa unafiki wao.

Najua saizi mpaka Jumatatu hali ya Dodoma itakuwa ni tata, vikao visivyokwisha vitakuwa vikiendela ili kunusuri hali hii.
 
Huwajui wabunge wa CCM!!! Tatizo watamzamia tunaugua ugonjwa wa kusahau au tuna vichwa vya panzi. Zito atashangaa anapata za chadema, ya kafurila na CUF hatapata ata moja. Ataishia kati ya 56 tu. Wabunge wa CCM ni nyoka.
 
Ikifika kesho Mawaziri wa Wizara zilizolalamikiwa Bungeni wasipojiuzulu kwa uwajibikaji na Wabunge tuliowachagua wasipoweka signature zao kumwajibisha Waziri Mkuu kwa kushindwa kuwashinikiza mawaziri hao kuwajibika. Wabunge tuliowapeleka pale tuwahoji kwanini wamekuwa wanapigia kelele kutuhadaa? wakati uwezo wanao?
 
Ikinikipimo tosha kwa wananchi kuwatambua kama kweli wa bunge wa ccm wanapiga kelele bungeni kwania ya dhati kuwa tetea wananchi au wanatuzuga make tumewasikia na sasa tunataka vitendo wavionyeshe kwa kupiga kula ya kutokuwa na imani na waziri mkuu.kama watashindwa hili basi wakae kinya wasubiri 2015
 
Hivi kweli, unajua UHAINI ni nini?
Kweli forum siku hizi imevamiwa na watoto
Wa facebook. Hakuna hoja katika kujibu au
Kujadili hoja. Wengi humu siku hizi ni watu wasio makini
Katika kujikita katika michango iliyozoeleka
Hapa jamvini. Hoja ni nyepesi, michango
Haina mashiko utoto umetawala katika issue
Sensitive kwa Taifa. Nia aibu kujiita great thinkers kwa kweli kama hali ndio hii.
Naomba kuwasilisha
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom