Kama kweli upo serious kupata Mpenzi wa kweli Mtandaoni, basi Wadada punguzeni ku-fake

myplusbee

JF-Expert Member
Jul 8, 2016
3,612
6,153
Hili naliandika kutokana na experience ya changamoto wanazokutana nazo members hususani akina dada!

Hivi ni wangapi huku mitaani tumewahi kuwasikia raia wakihoji “hivi yule kampendea nini!” Hapa ni pale unakuta mwanaume katimia kila idara, lakini mwanamke wake hata ukimwogesha kwa JIKI, hatakati! Au unakuta ni bonge la mwanamke, lakini mume wake, dah!

Hii maana yake ni nini?! Kama unadhani wewe ni mbaya, basi haijalishi wewe ni mbaya kiasi gani, lakini amini usiamini, yupo mtu mahali aliye kwa ajili yako kwa hivyo hivyo ulivyo! Huyu anayekuja kwako kwa vile ulivyo, ndie TRUE LOVER na sie yule anayekuja kwako baada ya kuwa umeji-fake!

Moja ya changamoto kubwa wanayokutana nayo wasichana walio serious kupata mwenza mtandaoni, au kwenye dating sites kama vile www.dating.co.tz ni kukimbiwa muda mfupi baada ya kukutana na wale waliodhani wangekuja kuwa wapenzi wao. Hii hutokea pale mwanaume anapoanza kumwa-approach msichana baada ya kuvutiwa na picha za mtandaoni za msichana husika! Ajabu ni kwamba, wasichana wengi wanapenda sana ku-edit picha zao kabla ya kuzitupia mtandaoni!

Hapa JF majority hatuweki picha zetu lakini hata hivyo hatupo salama! Wadada wengi wa JF wanapenda sana kuweka picha za wadada warembo kweli kweli, ambao hawafanani nao hata kwa mbali!

Mbaya zaidi, wengi wanaweka picha za wasichana warembo ambao sio maarufu na hivyo kuwafanya watu wadhani aliye kwenye avatar "anaweza" kuwa ndie muhusika! Hapa tafsri yake ni kwamba, ni bora uweke picha ya mtu let's say kama Rihana kwa sababu kila mmoja atajua hiyo avatar sio wewe!!

Au ni bora mara 1M ufanye kama my angel mmoja (huyu nahisi keshabadili ID manake tangia majuzi namtafuta simuoni! Ndo matatizo ya kuwa na michepuko mingi JF, ili kuwakwepa wengine, unabadili ID). Huyu Mrembo wangu inaelekea ana mahaba na Wakorea, na kwahiyo mara kwa mara huweka avatar za warembo wa Kikorea!

Sasa ukiweka avatar ya mtu maarufu sana au kama huyo mrembo wangu anayependa kuweka avatars za Kikorea, then 99% ya JF Users watajua hiyo ni avatar tu na sio wewe, kwahiyo hawezi ku-develop feelings kutokana na avatar yako bali kutokana na jambo lingine!

Lakini ukiweka avatar ya mrembo asiye maarufu wakati sio wewe, kuna uwezekano mkubwa sana watu wakaanza ku-develop feelings kwako kwa sababu tu ya avatar yako!! Sasa bora uwe mkali kuliko hiyo avatar uliyoweka au angalau usipishane nayo sana, kinyume chake, trust me, unakaribisha kuumizwa roho!

Lakini tukiachana na mambo ya avatar za JF, kumbuka kwamba ni kosa kubwa zaidi kuweka picha iliyo tofauti sana na ulivyo kwenye mtandao wa dating site!!! Unapojiunga na dating site lengo lako ni moja TU, nalo ni KUPATA MPENZI! Na kama wewe sio mdangaji basi lengo lako kwenye dating sites linatarajiwa kuwa ni kupata lifelong partner ambae unaweza hata kuanzisha nae familia. Tusisahau, kwa kawaida, wanaume wengi tunaanza kupenda kwa macho, na kwa muktadha huu, tutaanza ku-develop feelings kutokana na picha zako kuliko kitu kingine chochote kile!

Sasa kama umeweka picha ambayo sio ya kwako au ambayo umei-edit sana, hapo atakuwa ameanza kupendwa mtu ambae kimsingi SIO WEWE! Siku akija kufahamu ulivyo, ama kupitia picha zako zingine ambazo hujazi-edit au baada ya kukutana nae ana kwa ana kwa mara ya kwanza, my friend, amini usiamini kitakachofuata hapo ni kukimbiwa tu! Utakimbiwa kwa sababu yule ambae alimpenda awali sio wewe!! Tena bora ukimbiwe mapema manake kuna uwezekano ukakimbiwa baada ya kuwa umeshavuliwa nguo ya ndani! Kukutumia just for one time sex ambayo watu huwa wanafumba macho!!!

SASA SHIDA YOTE HIYO YA NINI?! Kwanini usijikubali kama ulivyo! Fahamu kwamba, ni bora watu wasiku-approach kwa sababu umeweka picha isiyovutia kwa sababu ndivyo ulivyo, kuliko kuweka picha inayovutia wakati haupo hivyo na mwisho wa siku unaashia kukimbiwa! Mbaya zaidi, ukiweka picha ambayo sio wewe, au ambayo umei-edit sana hadi mwenyewe akili zikikurudia huwa unajishtukia, trust me huwezi katika mazingira kama hayo katu hautakuwa na confidense ya kukutana na mtu ambae baada ya kuku-approach, tayari nawe ukaanza kumpenda! Lakini hata kama unaamini wewe ni mzuri, ukishaji-edit kwa kupitiliza tu, kumbuka atakayekuwa amependwa mtandaoni, sio wewe!

Kwa mfano, inawezekana wewe ni kisu ile mbaya lakini una ngozi nyeusi! Lakini badala ya kuweka picha inayoakisi rangi yangu, unatumia ma-filter unatokea kama Tanasha kwa weupe!! Usilojua ni kwamba, kila mwanaume ana tastes zake! Kuna wengine mwanamke awe mkali vp, lakini kama ni mweupe, hampi mizuka! Na mwingine kuwa mkali kiasi gani, lakini kama Cheusi Dawa, katu huwezi kumpa mizuka!!

Sasa wewe ni Mrembo Cheusi Dawa lakini umetumia ma-fitler na kutuwekea picha kama ya chotara la kiburushi! My friend, kwa staili hiyo utabaki kulalamika kwamba mapenzi ya mtandaoni hayaaminiki wakati ni wewe mwenyewe ndie usiyeaminika na hiyo faking life yako!

Uzuri ni kwamba, ukiweka picha ya kama ulivyo, hata ikipita mwaka hujawa approached, basi siku utakayokuwa approached, huyo aliyeku-approach atakuwa kakupenda kama ulivyo, na hapo ndipo penye uwezekano wa TRUE LOVE!

Nimeshamaliza!!!!!
 
Na hugu aliuetengeneza mafilter ameharibu hawa dada zetu yaani u akuja kutana na demu kumbe kabayaaa hababba ila mie nilishajiwekea kwamba kwenye hizi dating site wee nenda na akili moja tuu, chura ipo?
Aisee, we acha tu!! Yaani ni ngumu sana hivi sasa kuona picha ya mdada aliye chocolate color au cheusi dawa!!!
 
Ila wanao fake wengi shida yao ni kutumiwa nauli wewe hata usijichoshe.
Hivi walipo wadada 10, wasiotumia ma-filter wanaweza kuzidi watatu kweli?! Mi naamini wengine wapo serious kabisa lakini hawajiamini na muenekano wao! Ni kama ule utamaduni wao wanavyoweza kushinda lisaa lizima kwenye kioo akihangaika kujiremba au wengine wanavyohangaika kubadili rangi za ngozi zao, ndivyo hivyo hivyo wanavyohangaika kutumia ma-filter ili waonekane wazuri zaidi!
 
Aisee, we acha tu!! Yaani ni ngumu sana hivi sasa kuona picha ya mdada aliye chocolate color au cheusi dawa!!!

Yaani ata media yenyewe inatafuta totoz white 90 %ya matangazo kwa tv warembo ni weupe acha tuu. Yaani bora uzaliwa kidume maana ata ukiwa na sura mbaya angalau utasaka hela na utugegeda warembo wazuri tuu.
 
Back
Top Bottom